Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu Mkoani Katavi na Kigoma, azungumzia Katiba Mpya

Inapendeza na ina tupa matumaini sanasana
 
Anajisumbua tu hawezi kuwa raisi,hakuna mtu atakae mchagua,hata mwenyewe yuda iskariote anajua hawezi kuwa raisi

Kuna avatar mwonekano tu unaakisi nini mwandishi alipata kabla ya kuandika alichoandika.

Tumekusikia Rastafarian.
 
Wewe ni mpuuzi mmoja tu hujitambui kama wewe hutamchagua ni wewe ila sisi na mke wako tutamchagua lisu
Mkuu, huyo ni mdada asiyejitambua. Ameshindwa kujenga hoja ameishia kuleta MIPASHO tu humu, mume wake ni lazima atakua anapitia wakati mgumu sana huko kwao.
 
19 September 2020
Kigoma, Tanzania

Kigoma-Ujiji imepigika kiuchumi na CCM Mpya ikatubatiza uraia wa Burundi , 2020 sasa basi CCM Mpya

Mwaka 2015 baada ya Uchaguzi tuliambiwa ni 'Warundi' lakini wakati wa Uchaguzi CCM mwaka huu 2020 uwanja wa Tanganyika jana CCM inatutambua ni waTanzania kwa kuwa wanataka kura zetu.
 
Hana uwezo wa kushinda toka lini yuda iskariote akafanikiwa
Yuda Iskariote ndiye tuliye naye sasa hivi.

Watanzania walimchagua ili awalinde, lakini akaanza kuwateka, kuwatesa na kuwamiminia risasi wanaomkosoa.

Watanzania walimchagua ili awastawishe, yeye akaanza kuwafilisi, kuwabambikia kesi na kisha kuwafilisi.

Watanzania walimchagua ili alinde haki zao za kiraia, lakini akageuka na kufuta haki zao za mikutano ya siasa, haki za maoni, uhuru wa kuwachagua viongozi wanaowataka.

Watanzania walimchagua ili aimarishe demokrasia, yeye akaua demokrasia kwa kuwateua wasimamizi wa uchaguzi makada wa chama chake, akaufuta uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwaondoa wagombea wa vyama vya upinzani na kuwatangaza wagombea wa chama chake kuwa ndio washindi.

HUYU NDIYE MSALITI MKUU, DIKTETA, MUONEZI, NA DHULUMATI WA HAKI ZA WATANZANIA ANAYEZIDI HATA ULE USALITI WA YUDA ISKARIOTE. SASA AAMWAMBIWE KUWA IMETOSHA. MHALIFU HASTAHILI KUABUDIWA BALI KUKARIPIWA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa hiyo mkuu umeridhika na hila wanazofanya ccm au wewe ni sehemu ya wanufaika??
Waliwarubuni wafanyakazi wakawachinjia kule...
Wanajisifu elimu ni bure wakati vyuo vikuu mikopo imeongezewa tozo...
Wamepora haki ya wastaafu kupata na kufaidi mafao yao...
Hivi unajua kuwa maendeleo kamili ni yale ya kuwawezesha watu waweze kukutegemea na kujiendeleza wenyewe bila kutegemea juhudi za serikali...??
 
maneja kampeni wa lissu, nakukumbusha tena ,usisahau kumkumbusha lissu, atakapo fika kanda ya ziwa asisahau kuzungumzia kuhusu kitendo cha magufuri na serikali yake kuchoma zana za uvuvi pamoja na mitumbwi yao ameshiriki kuwafilisi wavuvi

Pia kuongeza ushuru wa dagaa Hadi wacongomani wakahadimika njaa ikaingia ziwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…