Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika viwanja vya Zakheim Mbagala, TBC Wafukuzwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Salaam Mkuu,

leo Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kinafanya uzinduzi wa kampeni za urais wa Tanzania zinazofanyika, Uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Tundu Lissu ndiye anayepeperusha bendera ya Chadema kwenye nafasi ya urais na Salumu Mwalimu mgombea mwenza.

Kampeni za Uchaguzi Mkuu zilifunguliwa rasmi tarehe 26 Agosti na zitahitimishwa tarehe 27 Oktoba 2020 ambapo kesho yake yaani Jumatano itakuwa ni siku ya uchaguzi. Katika uchauzi huu, Lissu atachuana na wagombea wengine 14 akiwemo Dk. John Magufuli, mgombea wa Chama cha Cha Mapinduzi (CCM), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi).


Nitawaletea Kila kinachojiri.


Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema bara na Mwalimu, naibu Katibu Mkuu-Zanzibar tayari wamewasili uwanja hapo.

Ulinzi umeimarishwa katika viwanja hivyo, ambapo kuna baadhi ya askari polisi wa kawaida na wale wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).

Pia, kuna walinzi maalum wa Chadema ambao wanafanya kazi ya kuongoza watu waliofika katika kampeni hizo.

======

UPDATES: 1600HRS

Mkutano Umeanza kwa Kuimba Wimbo wa Taifa na kufuatiwa na Maombi kutoka Madhehbu mbalimbali

1621HRS: Utamburisho wa Wagombea Ubunge Mkoa wa Dar Es Salaam

- Mgombea Ubunge Ilala - Hashim Mussa Juma. Anasalimia amesema anaenda kuchukua jimbo la Ilala na Ikulu itakua chini ya CHADEMA. Majimbo yote kumi tutachukua kwani tunaenda kuungana. Watanzania wamechoka na wewe, ahadi zako zote za Uongo. Miaka Mitano rais Magufuli hajaongeza Mishahara.

- Ibrahim Hassan Mbunge wa Mkuranga amepanda jukwaani Kusalimia.

- Suzan Lymo Mbunge wa Kinondoni. Nataka niwaahidi kwamba tunaenda Kushinda.

- Asia Msangi wa Jimbo la Ukonga. Sasa baasi

- Sina Manzi Temeke: Anasema tunakwenda kushinda Jimbo la Temeke na Mbagala na Tunaenda Kushinda.

- Hadija Mwago wa Jimbo la Mbagala: Mkono unaolea MWana ndio unaolea taifa

- John Mrema Mgombea wa Jimbo la Segerea: Tutakutana Segerea Jumapili

- Godlbess Lema anasalimia...(TBC Wamekata Sauti)

Lema anasema: Nmekuja Kumuunga Mkono Mgombea Urais. Mbagala Dar Nchi hii inaendeshwa kama Getto la Wahuni, NEC imeengua wagombea wa Udiwani 16 katika jimbo la Mbeya Mjini. Wanaofanya Serikali inakuwa na Mambo ya Kihuni sio wanaokuwa Madarakani bali Wananchi Waoga. Kuliko kuendelea na kampeni na upumbavu huu unavyoendelea ni Muhimu CHama chetu kikatisha Mkutano wa Kamati kuu itoe kauli juu ya haya yanayoendelea. NI heri shari inayotafuta haki na Usawa kuliko amani inayopumbaza utu haki ya BInadamu. Upumbavu umezidi, Nchi nzina lazima tuzuie Upumbavu. Tunamtaka Mwenyekiti wa Tume,IGP na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wajue kuchezea Uchaguzi ni kuchezea amani ya Nchi. Asanteni sana.

(Wananchi Wanamtaka Halima Mdee)

Wanaambiwa kwamba Mdee, Jacob na Mbunge wa Kibamba wapo wanaandaa Mkutano wa Kawe unaofanyika Kesho.

Anakaribishwa Alshia Magabe Tundu Lissu(Mke wa Lissu

Alshia anasema
: No hate no fear. Mimi kwa leo sitakuwa na mengi ya kusema si nafasi yangu kusema ila tu nawashukuru wote kwa support yenu kipindi chote Mume wangu kipenzi alipokuwa akiumwa. Asanteni

1640HRS: Anaongea Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika....(TBC Wamekata sauti)

Mnyika: Mimi jukumu langu mwaka ni kupokea Maelekezo kutoka kwenye Uongozi wa Chama na Maelekezo ya rais ya kuhakikisha CCM inatoka Madarakani. Huu umma umenikumbusha tulipokuwa kwenye Mazungumzo ya Katiba Mpya. Nakuombe sana Mheshimiwa rais Lissu, Utuletee Mchakato wa katiba Mpya. Neno moja ambalo unaweza kumzungumzia Lissu ni haki haki haki tu.

Lissu atahitaji kuunda Serikali, Waziri Mkuu, Halmashauri nyingi, lakini Magufuli baada ya kuona dalili za kuondoka Ikulu zipo wazi yeye na Vibaraka wake wanaosimamia chaguzi, wanataka Lissu awe rais halafu awe na Wabunge Wachache ashindwe kuunda Serikali, eti Serikali iongozwe na Wabunge walio wengi wa CCM kwa kuwaengua Wabunge wa Chadema Sehemu Mbalimbali ya Nchi yetu. Jambo hili haliwezi kukubalika

MKutano wa leo ilikuwa Tuzindue Ilani ya chama chetu, lakini naomba ajenda hii tuiweke pembeni. Ni vizuri kwanza tudai haki, haki ya kugombea na kushinda majimbo mbalimbali. Tunasubiri maelekezo yako mwenyekiti ili nini tufanye kudai haki.

1643HRS anaongea Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anasema:

Namshukuru Mwenyezi Mungu anatupa nafasi ya Kuzungumza baada ya Miaka mitano. Serikali ilikataza vyama vya siasa kujijenga, UHuru wa Wananchi Umeporwa. Miaka mitano ya risasi, Miaka mitano ya vifungo, miaka mitano na kila aina ya Mateso. Tuliamini kwa muda, wenzetu waliopo kwenye madaraka, Pengine watatambua kila mtanzania ana uhuru wa kusema na kuamini anachokiamini.

Vyombo vya habari vinafungiwa Vyombo vya habari vinatishwa. Ni rahisi kufungia gazeti TV na Radio. Wananchi wananyimwa Uhuru wa kupata habari nini kinaendelea katika nchi yao.

Wachache waliopo madarakani halitakuwa na Uhuru ambayo Wazazi wetu walipigania.

Tutafanya makosa ya kimsingi kama tukizungumzia Ilani za Uchaguzi wakati Wagombea wameenguliwa.

Tumeona Serikali za Mitaa waliondoa Wagombea wote waienguliwa wa Upinzani.

Uhuni uleule wanataka kuurejesha tena mwaka huu. Haki ya Mungu nasema, Bora Watuue Bora Watufunge. Ni lazima tutoke na Kauli.

Ndugu zangu wa Dar Es Salaam, katika hatua hii sisi kama chama pamoja na maumivu tuliyopitia kwa miaka mitano, tuliandaa Wagombea ubunge katika Majimbo yote na kwenye Kata zote za Tanganyika na Visiwani.

Tuliandaa madiwani katika kata 3958 zinazounda Tanganyika hali kadhalika Visiwani.

Watumishi wa Serikali wakishirikiana na vyombo vya Polisi wanawaondoa Wagombea wa Upinzania hususani chadema. Sisi hatutakubali kushiriki Uhuni na Hatutajitoa

Tunamuambia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, amani ya nchi hii ipo Mikononi mwake.

Namwambia rais Magufuli haya yanayofanyia anayajua na ameyabariki.

CCM wanajua hawachaguliki tena, Watanzania wamewachoka, Kama wanajiamini, Waruhusu Wagombea wetu tushindani kwenye sanduku la Kura.

Leo asubuhi nmeongea na Mazungumzo na Viongozi wa chama cha ACT. Kule Zanzibar katika majimbo 50 hadi muda huu, wameengua Wagombea Ubunge zaidi ya 40. Hapo kuna Uchaguzi kuna Uhuni?

Kama Zanzibar yenye Wagombea 50, mpaka dakika hii wameshaengua 42 na sisi tuseme eti kwa sababu wameenguliwa wa chama kingine na sisi tuendele hakunashida, tunasema Kwenye Uchaguzi huu hatujitoi, kama ni noma na iwe noma. Wenzetu Zanzibar ACT wanaonewa sisi tukae Kimya? Sasa basi.

Namshukuru Maalim Seif ametoa Kauli nzito Zanzibar leo, na sisi leo tumebadilisha ratiba za Uchaguzi. Makamu mwenyekiti(Lissu) atasema.

Naomba Sasa niwalete Kwenu Tundu Lissu na Salim Mwalim

Wakati tunaanza kuzungumza, TBC walikuwa wanarusha mazungumzo haya, nlipoanza kuzungumza wamekata Mawasiliano wakidhani wao ni chombo cha CCM, Tukiongea mambo ya Muhimu Wanakata mawasiliano.

Waondoke Wasiondoke?

TBC nawapa dakika 15 kuondoka Kwenye Uwanja huu. Na wataondoka
(Baada ya dakika 4)

Wakati wakiondoka tuendeee na mkutano wetu.

1658HRS: Mbowe anamkaribisha Salum Mwalimu
Salim


Watu wa Mbagala, Hawa TBC wasitutoe kwenye focus. Wameshapewa amelekezo waondole naona ndo wanajikunjakunja kule. Haina maana tuangalie kule wakati huku mambo ya Msingi yanatupita

Mimi naitwa Salim Mwalimu, ni Mgombea Mwenza katika nafasi ya Urais.

Tupo tayari kupokea tamko la Lissu? Karibu issu

1704 HRS: Tundu Lissu anaongea


Naomba niwasaimu.

Nawasalimu wote vyombo vya habari vya mtandao, nasikia TV wamefanya wanayo yafanya,

Tarehe nne ya mwezi huu nlipoteuliwa kuwa Mgombea, Nlianza kuandika Hotuba ya Ufunguzi wa Kampeni ya leo

Kutokana na mambo ambayo yamefanyia naomba mnisamehe kwani sitaisoma. Ntaisoma mahali popote pale hata kama hatuna mgombea hata mmoja.

Ambayo nataka nliseme la Kwanza ni Shukurani

Tarehe 07.09.2017 Mnafahamu yaliyonikuta na yaliyoikuta nchi yetu. Sasa siku hiyo sikuapswa niwe hai. Lakini miaka mitatu baadae, nmesimama mbele yenu nikiwa hai, nachechemea chechemea Kidogo. Kwenye mwili wangu kuna risasi imebaki mahali, lakini kikubwa nipo hai. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.

Siku ile ya tarehe 07, baada ya kuumizwa vile nlikimbizwa hospitali na watu watatu. Gari zilizokuwa jirani zote zilipigwa risasi. Hadija akukweti alikuwepo pale kwenye nyumba ya Naibu Spika na Adam Bakari Amina Kanyama Walinipakia kwenye gari na kunikimbiza Hospitali. Wasingekuwa wao labda nisngepona. Nawshukuru na Wao.

Pale Dodoma Wauguzi na Madkatari walinihudumia pale sababu nlipoteza damu sana. Nawashukuru Madaktari na Wauguzi kwa kuokoa Uhai wangu. Nakumbuka maneno ya Mwisho, Nimwambia Mwenyekiti Hawa watu wameniumiza sana,

Nlikuja kuambiwa kwamba Uamuzi wa nairobi ulikua na Mvutano sana. Kuna watu waileta Ndege nipelekwe Muhimbili. Mwenyekiti wetu Mbowe alisema hatuna UHakika na Muhimbili akasema kwa vyovyote vie huyu mtu apelekwe nairobi. Wale walioeta ndege Wakazira, Wakamziria Mwenyekiti

Ninachotaka kusema kwamba Mwenyekiti aliweka Msimamo, hakutaka kwenda Muhimbili. Nawashukuru wote. Nakushukuru sana Mwenyekiti.

Kuna mtu alikuwa katibu Mkuu wa Wizara ya afya Mpoki. Alisaini nipelekwe Nairobi. Namshukuru sana. Hatukua na hela kukodi ndege. Kuna mbunge mmoja wa CCM naomba nisimtaje jina wasimfanyie figisu. Hela za kwanza za ndege ndiye alitoa, Namshukuru sana. Baada ya hapo kuna Wabunge wa CCM walikuja kuniona pamoja na kupigwa Marufuku. Nawashukuru sana. Wabunge wawili wa CCM waikuja kuniona Nairobi na Mmoja Ubelgiji. NAwashukuru sana. Mlinifanyia maombi na maombi yenu yalijibiwa. Nawashukuru

Nlinyimwa fedha za tiba, pamoja na Sheria inasema Mbunge atibiwe, lKini Serikali na BUnge hawajatoa hata senti kumi. Lakini Watanzania Mlinichangia. Mlikatazwa kunitolea damu, lakini wakenya walijotolea damu. Nliongezewa damu mara tatu ya damu yangu ya wakenya. Serikali ya Kenya ilitoa Ulinzi wangu wa masaa 24 kwa miezi yote minne.

Nawashukuru Wabelgiji kwa kunipokea na kunitibu na walitoa damu yao. NAwashukuru wote mlionisaidia. Mungu awabariki sana.

Nlisema haya ningeyasema sehemu yoyote hata kama hakuna Uchaguzi

Nlitengeneza hotuba ya kurasa 24. Tutayazungumza kwa muda mwafaka. kwa leo hapana, Wagombea Udiwani tuliowaweka 3754 Wagombea 3955. Hatukiweka wagombea katika kata 201 tu. Hapa tunapoongea Wagombea 1,020 Wameenguliwa kwa sbabu za kihuni na Uonevu. Hata Kampeni hazijaanza kumeshapoteza Wagombea asilimia 30.


Kweye Ubunge tuliweka Wagombea 244 kati ya Majimbo 264. Wagombea Majiimbo 20 ya Pemba tu ndio hatukuweka. Hadi sasa Wagombea wetu 53 Wamekwisha enguliwa. Wamenguliwa Kihuni na sababu za kipuuzi na za hovyo.

Chama kingine cha Upinzani ACT, mpaka hapa tuliposimama wamenyangyanywa Wagombea 47, na 16 kutoka Pemba yenye Majimbo 18

CCM haijawahi kushinda kiti hata kimoja Pemba tangu 1995.

Katika majimbo ya Unguja 34 wameonyofoa Wagombea 33 na amebaki mmoja tu,

Uchaguzi mkuu uliopita CCM walishindwa Uchaguzi Zanzibar. Wameondoa Chama kikubwa Zanzbara ACT Wazalendo.
Engua engua inaendelea.

Katika historia ya vyama vingi, haijawahi kutokea Wagombea kuenguliwa kama safari hii.

Wanataka Waongoze bila kupigiwa kura

rais Magufuli alisema hawezi akawapa Wakurugenzi magari mazuri, MIshahara Mikubwa harafu wawatangaze wapinzani kuwa wameshinda Uchaguzi. Wale aliyewateua yeye hawapaswi kutangaza wapinzani. Wagombea wetu wameenguliwa na watu aliowateua.

Mkisema sio rais ntawaambieni. Katiba ya Tanzania inasema aliyeteuliwa kuwa rais ataendelea kuwa rais mpaka rais mwingine atakapoapishwa. Mkisema sio rais hamuoni Mnakosema?

Wagombea wetu wameenguliwa kwa sababu alitamka hata Wanaompinga yeye na CHama chake Washinde Uchaguzi. Haya ni matokeo ya kauli ya rais.

Tuna Wenyekiti wa Mitaa, Wenyeviti wa vijiji ambao hawajachaguliwa na mtu yoyote. Yanayotokea leo ni muendelezo wa huo msimamo wa rais wetu.

Tume yetu ye Uchaguzi imeteuliwa na Magufuli.

Juzi mimi nmemuwekea rais Magufuli pingamizi kisheria. Nmemuwekea pingamzi ukweli wa Mungu hakupaswa kuwa mgombea. Anatakiwa akathibitishwe na Mkurunzi wa Uchaguzi.Mimi pekee ndiye wadhamini wangu walithibitishwa na Tumeya Uchaguzi kisheria. Nliwapelekea Tume tulikaa mpaka saa sita za Usiku. Wakakubali Wadhamini wangu wawathibitishe. Wagombea wote hakuna waliothibitishwa na Tume.

Kwakuwa Tume imechaguliwa na Magufuli, Usiku kucha wamebadilisha nyaraka chamwino. Na wakatangaza Usiku Mapingamizi yametupiliwa Mbali, Uongo

Tutatokaje hapa?

Kama wanategemea tutajitoa kwenye Uchaguzi Wasahau

Tutakachofanya kuanzia leo nchi Nzima katika kila Mkutano wa Kampeni, Hoja yetu ni Wagombea wetu walienguliwa kinyume na Sheria warudishwe bila mashariti

Tutaenda Kesho Kawe, Segerea na Nchi nzima tukidai wagombea wetu warudishwe. Tunawaomba Mchi nzima Muandamane kwa amani mchukue hatua ya kudai wagombea wetu warudishwe. Sisi hatutasababisha Umwagaji wa damu. Ndo maana nikasema maandamano ya amani. Hatutarusha jiwe, hatuna bunduki. KIla kampeni ianze na maandamano ya Mani Nchi nzima. Zanzibar andamana, bara andamana.

Haiwezekani na haitawezekana sisi tuwe wa kulia kila Uchauzi, hatulii, tuchukue hatua. Haki hailetwi kwenye kisahani cha fedha kama kichwa cha yohana Mbatizaji. Haki inapiganiwa na kudaiwa. Mgombea wetu wa Udiwani, cha kwanza ukaandamane kwenye Ofisi ya Msimizi wa Uchaguzi warudishe Wagombea wetu, hata wewe Mbunge fanya hivyo. Hatuwezi kuwa taifa la kupiga Magoti

Hata Mimi sitaanza Mkutano wa kuomba kura bila maandamano ya amani. SIsi ni watu wa amani, hatutakubali kuonewa. Kuwa Mtu wa amani haimanishi shavu lipigwe mara mbili.


Tunataka tupambane nao hoja kwa hoja sio Uhuni wa Mezani.

Nawaombeni vyombo vya Usalama. Msitumie Silaha zenu dhini ya Wananchi wanaodai haki. Waondo wamezinunnua. Msije kutetea waovu.

Tunataka tushindane, hatuwezi kushindana wakati mshindani ameondolewa.

Tumeweka Wagombea kila Mahali halafu tunafanyiwa Uhuni

Kuanzia sasa ni kufanya maandamano. Watufunge au watupige risasi kama wanataka.

Nawaomba Jumuia ya Kimataifa watuunge Mkono kwenye hili. Nchi rafiki za Tanzania wamuambie rais wetu hili jambo analotaka kufanya halikubaliki. Masharika na Kimataifa na Umoja wa Mataifa wamuambie hili analotaka kulifanya halikubaliki.

Ukaidi ukiendelea Jumuia ya kimataifa ichukue hatua Serikali ya Magufuli. Waofanya mambo haya wasipate mahali pa kujificha wala MSaada/

Imeandikwa haki Huinua taifa. Tunataka tutendewe haki, Wenye haki wakipata amri watu hufurahi na wasio na haki wakipata amri watu huugua. Tunataka watu wetu kwenye Uchaguzi huu wawaondoe waovu ili waache kuugua

Tunataka Wagombea wetu Warudishwe bila Marariti.

Hatujiondoi. Kama wanafikiria tutakimbia hatutakimbia cha kufanya ni maandamano.

Tunahitaji vitendea kazi. Mtusaidie tuweze kufanya kazi ya kufanya kampeni na kudai haki.

Wamekuwa wanasema huyu Lissu kwenye Hoja hatumuwezi ila hana hela, Wanasema huyu mbowe tumeshamchakaza Kiuchumi, Wamemvunja. CHADEMA Haina hela. Mtuchanngie. (Anaelezea jinsi ya kuweza kuchagia chama kwa kutumia simu)

#Wananchi Wanadai network imekatwa.

1800HRS: Anamaliza kwa Kushukuru. Anasema Nawaombeni watanzania muendelee kutuombea. Nawashukuruni sana kwa Kunisikiiza.

Kamaliza

Unapigwa wimbo Maalum wa CHADEMA

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…