Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika viwanja vya Zakheim Mbagala, TBC Wafukuzwa

Kutokana na ubaguzi wa kuripoti kampeni zenu lazima muachane nacho kwani kinaendelea kuonyesha ubaguzi wa wazi kuripoti kampeni zenu kama tunavyo shubu
 
watu ni wengi ila TBC wanachakachua. wanatakiwa wachukue aerial view ndiyo itaonyesha uhalisia!
acha uongo embu tuma picture km hii hiz
 

Attachments

  • Screenshot_20200812-151627.png
    181.3 KB · Views: 2
🤣 🤣🤣 unajitahidi sana ku prove.
Kuna aina tatu za picha;-
Horizontal, Oblique na Vertical.
Hiyo uliyopiga na Horizontal.
Sasa jaribu kupiga hizo mbili. Watu hawajai hata kwenye sahani.
Hatushindani na mabwege wabishi
 
Sisi tunstaka tuwasikie Chadema badala yake mmeuteka mkutano na nyie kuanza kututangazia kampeni yenu, hatutaki kuwasikiliza nyie labda ndiyo kazi mliyotumwa.
 
Acheni kuchambua tunataka tusikilize hoja za upinzani kama hamtaki tusikilize ni bora msionyeshe kabisa ,mnachofanya ni ukajanja
 
Nashangaa TBC imekwenda kurusha kampeni lakini badala ya kurusha hotuba za watu haswa zile zinazochallenge namna Magufuli anavyoendesha nchi wao wanakatakata.

TBC wajue kuwa kampeni ni pamoja na kujinadi na kukosoa namna nchi inavyoendeshwa na utawala uliopo. Sasa TBC yenyewe ndo wamegeuka wahutubiaji kila mtu huko kwenye kampeni anapopiga nyundo kali!

TBC kama mmegeuka nyie ndo wahutubiaji basi rudini studio mkatengeneze documentary.

Yaani hakuna matusi, wala kitu kibaya lakini kwa sababu wanachallenge namna serikali ya Magufuli ilivyoshindwa katika angle mbalimbali wanakata!

Mnaboa sana!
 
Ile ilikua nguvu ya pesa baba sasa hawa sijui kama wamejiandaa kwa pesa
Aise mkutano umepowa km maji yaliyoko kwenye mtungi. yaan yale ya hamna lowassa hamna kabisa. ila hakuna atakayekuja kufikia Lowassa
 
Mimi nilifikiri ni mkutano wa Chadema kumbe ni tv talk show yao TBC.

Lema amesema nchi hii inaongozwa kama geto la wahuni wamemkatia sauti wakati anaelezea udhalimu wa tume ya uchaguzi.

Sipati picha chuma Tundu Lisu kikipanda jukwaani wanaweza wakazima jumla matangazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…