Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu - Januari 19, 2022

Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu - Januari 19, 2022

Shahidi wa Leo ni wa upande gani?Mbona Naona kama vile ni wa upande wa utetezi?Maana kasema kwenye uchunguzi wake hakuona jinai kwenye hizo simu!

Sasa ameletwa na upande wa mashtaka kuja kufanyaje?
Nimeshangaa sana ushahidi wake kwa kweli! Kwenye uchunguzi hakuna jinai yoyote iliyoonekana yet wapuuzi wanafungua kesi.

Mungu wa mbinguni hutenda kazi zake kwa namna ya ajabu sana. Kamwibua huyu kunguru miongoni mwa watesi kumwokoa Mbowe na watu wake; leo milango ya gereza imefunguka yenyewe.
 
Hati ya mashitaka inasema kuwa na mipango ya na nia ya kufanya vitendo vya kigaidi. Bahati mbaya nyie mmeaminisha muuliza na mnauliza magogo yako wapi? Vituo gani vililipuliwa? Laki 600, 000 inaweza kufanya ugaidi? sawa lakini kosa na kuw na nia ya kutaka kufanya ugaidi?

..mimi sio Polisi au mwanasheria lakini naona hayo mashtaka yako too general.

..watu wana mipango mingi, sasa mipango ya kufanya ugaidi ikoje? Vigezo vyake ni vipi?

..nikiweka vigezo ninavyovifikiria mimi sioni mipango ya kigaidi, na sioni upande wa mashtaka ukijitahidi kufikia kanuni ya " beyond reasonable doubt."

..kuhusu kipengele cha nia, hicho nacho kinathibitishwa vipi?

..Unaweza kweli kuthibitisha nia ya kuweka magogo barabarani bila kumkuta mtuhumiwa na magogo? Hayo magogo yalikuwa yatoke wapi? Walipanga kuyanunua, au kukata wenyewe?

NB.

..kama Mbowe alikuwa na mipango au nia ya ugaidi kwanini hakutumia vijana au wanachama wa Chadema?

..Kwa kawaida magaidi huwa hawakodiwi. Magaidi huwa ni watu waliokuwa indoctrinated.

..Na kuweka magogo barabarani sidhani kama kunahitaji makomandoo.
 
GOOD OBSERVATION
Ila huu sio ushahidi peke yake. Nikurudishe nyuma kwenye ushahidi wa Kaaya. Kaaya alimuunga Mbowe, Adamoo na Sabaya, adamoo alikabidhiwa kazi ya kushughurika na Sabaya na akasema hiyo ni kazi ndogo sana kwake. K wa hiyo kama na kwenye mawasiliano ya simu ya Mbowe yumo- kazi kwisha

Ni kweli usemavyo. Lakini inatakiwa prosecution waje na sms angalau moja ya kudhibitisha kuwa Kuna maelekezo ya kumdhuru Sabaya yapo.
 
Wakati mwingine mjinga unamjibu kijinga
Rejea Yesu na Pilato
Pilato- wewe ni mwana wa Mungu
Yesu- WEWE WASEMA
Kesi ya Yesu ilikuwa ya kubambika Kama hii, PILATO alipokosa ushahidi, akawauliza wabambika kesi: Sioni kosa, ila Kuna desturi ya kumwachia mmoja, nimwachie Nani, Yesu au Baraba? Wabambika kesi(CCM),Mwachie Baraba(ambaye alikuwa jambazi).

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli usemavyo. Lakini inatakiwa prosecution waje na sms angalau moja ya kudhibitisha kuwa Kuna maelekezo ya kumdhuru Sabaya yapo.
wana mashahidi 28 bado 18 ngoja tuone wnavyoenda ila so far so good
 
Sasa huyo shahidi aliyeulizwa amejubu nini? Au ni nani atakayekuja na haya majibu iwapo forensic expert hajayajibu...!!

Mimi na wewe tusubiri, maana huyu shahidi ndio alikuwa the sucker punch kwenye hii kesi. Kama hatapatikana was kuyajibu haya maswali basi sidhani Kama Kuna kesi ya kujibu hapo. Hata confession ya kina lingwenya itakuja kuonekana haina nguvu kwasababu wanakirije kosa ambalo halipo?
 
Tusubiri- we are just half way. Ila utetezi walipewa kila kitu kwenye committal - wanajua kinachokuja mbele yao ila wameamua kudhalilisha mashahidi badala ya kushughurika na ushahidi dhidi yao.
 
Nina mashaka na uelewa wako
  1. kazi ya shahidi ilikuwa kuunga mkono ushahidi wa wataalam wa Tigo na Airtel na amefanya hivyo
  2. kazi ya shahidi ilikuwa kuwaunga pamoja urio na Mbowe na wenzako na kwa kufanya hivyo anaunga mkono ushahidi wa shahidi anaitwa Kaaya
  3. kazi ya shahidi ilikuwa kuunga mkono ushahidi wa Kingai ambaye aliwakamamata baadhi ya watuhumiwa na simu
Bado atakuja mtu atakaye chunguza computa za watoto wa Mbowe maana Mbowe alijiona mjanja ila msemo wa Kiswahili- NDEGE MJAJA HUNASWA NA TUNDU BOVU.
Tundu bovu ndio hawa polisi mnao wadhihaki mkisau mlisoma wote; wao wako kazini nyie mnatembeza bahasha na kushinda mahakamani.
Je baada ya kuunganisha ushahidi wa tigo na airtell pamoja na msg alizohack amepata mazungumzo yoyote yenye viasharia vya kufanya uhalifu kupitia fedha hizo zilizotumwa kwa njia ya simu alizochunguza ??🤣🤣😂

FJeuh7RXIAASOQh.jpeg

Huyu Hacker amelivua nguo jeshi la polisi na CCM kwa ujumla
 
..kinachozingatiwa mahakamani ni USHAHIDI usio na mashaka.

..hizo Software hazisaidii chochote kama hakuna ushahidi unaowa-link watuhumiwa na jinai / ugaidi.

..mpaka sasa hivi hajatokea shahidi anayewa-link watuhumiwa na mashtaka yaliyoko mbele yao.

..Ndio maana hata maswali ya mawakili yanaonekana hayana uzito au maana. Ni hili unaweza kuliona kwa mawakili wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi.

..Polisi hawajapeleka ushahidi mzito. Hivyo wanafanya kazi ya waendesha mashtaka kuwa ngumu.

..Utetezi nao wana wakati mgumu, kwasababu mashtaka dhidi ya wateja wao ni mabaya na ya hatari. Lakini ushahidi so far hauonekani. Kwa hiyo wako in limbo.

..Shahidi wa leo sioni hata ana maana gani ktk kesi hii. Sijaona akitaja jambo lolote linalowaunganisha washtakiwa na tuhuma zilizoko mbele yao.

..Shahidi anazungumzia simu za watuhumiwa na Software zinazotumika ktk uchunguzi. Nilitegemea aende hatua moja zaidi kusema amebaini kitu gani kinachowaunganisha watuhumiwa na njama za ugaidi.

..At least yule Mama toka Airtel alizungumzia miamala. Sasa ni jukumu la upande wa mashtaka ku prove pasipo na shaka kwa miamala ilitumika ktk njama za ugaidi.
Wakati mwingine akili inakurudia, mara inapotea! Hueleweki.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
..mimi sio Polisi au mwanasheria lakini naona hayo mashtaka yako too general.

..watu wana mipango mingi, sasa mipango ya kufanya ugaidi ikoje? Vigezo vyake ni vipi?

..nikiweka vigezo ninavyovifikiria mimi sioni mipango ya kigaidi, na sioni upande wa mashtaka ukijitahidi kufikia kanuni ya " beyond reasonable doubt."

..kuhusu kipengele cha nia, hicho nacho kinathibitishwa vipi?

..Unaweza kweli kuthibitisha nia ya kuweka magogo barabarani bila kumkuta mtuhumiwa na magogo? Hayo magogo yalikuwa yatoke wapi? Walipanga kuyanunua, au kukata wenyewe?

NB.

..kama Mbowe alikuwa na mipango au nia ya ugaidi kwanini hakutumia vijana au wanachama wa Chadema?

..Kwa kawaida magaidi huwa hawakodiwi. Magaidi huwa ni watu waliokuwa indoctrinated.

..Na kuweka magogo barabarani sidhani kama kunahitaji makomandoo.
Nakushauri usome sheria ya ugaidi- nimeiweka in one of my post kwenye post hii- kesi iko clear na ushahidi to the point vinginevyo kesi isingefika huku. SIKIA serikali ina maguvu makubwa sana - ikitaka kuweka Mbowe ndani hata bila kesi inaweza- kutakuwa na kelele sawa lakini atakuwa yuko huko. Hivi unajua sheria ya kuweka watu kizuizini ipo na haijafutwa ila kwa sababu viongozi wetu ni waungwana hawaitumii- kama ile sheria ya kunyonga- ipo ila hakuna anayeyonyongwa.
SASA KAMA NI HIVYO KWA NINI HII KESI IPO NA ITAKUWEPO MPAKA 2025 KWA HUU MWENDO WA MAPINGAMIZI SIJUI KESI NDOGO NDANI YA KESI KUBWA?
IGP alisema Mbowe si malaika ni mtu na ushahidi tunao- twende mahakamani
CHADEMA
1. Mbowe hawezi kukamatwa- kakamatwa
2. Mbowe hawezii kufikishwa mahakamani- kesi ipo
3. Kesi haina ushahidi- leo tuna shahidi wa 10
4. POLISI hajui PGO- BLAH BLAH
 
Je baada ya kuunganisha ushahidi wa tigo na airtell pamoja na msg alizohack amepata mazungumzo yoyote yenye viasharia vya kufanya uhalifu kupitia fedha hizo zilizotumwa kwa njia ya simu alizochunguza ??🤣🤣😂

View attachment 2088500
Huyu Hacker amelivua nguo jeshi la polisi na CCM kwa ujumla
atakuja mtu wa sauti mtashangaa ila hamwezi kumkana Mbowe NAJUA mtasimama naye mpaka mwisho maana nyie ni kupe
Ng'ombe anapelekw a mnadani- kupe yupo
ng'ombe anauzwa- kupe yup tu
ng'ombe anachinjwa - kupe anabaki na ngozi
Ngozi inapelekwa kiwanda cha ngozi- kupe yupo tu mpaka amwagiwe acid
 
Mimi na wewe tusubiri, maana huyu shahidi ndio alikuwa the sucker punch kwenye hii kesi. Kama hatapatikana was kuyajibu haya maswali basi sidhani Kama Kuna kesi ya kujibu hapo. Hata confession ya kina lingwenya itakuja kuonekana haina nguvu kwasababu wanakirije kosa ambalo halipo?
In my opinion, mpaka sasa serikali imeshindwa kuleta ushahidi wa kutosha. Inakuwaje mpaka shahidi wa10 anashindwa Kuja na ushahidi wa kujitodheleza? Kitendo cha shahidi wa kwanza kujikanyaga tayari ilikuwa ni walakini mkubwa.

Hii aibu kwa serikali itaokolewa na Jaji. Halafu wayamalize kwenye Mahakama ya Rufaa.

In my analysis, Mbowe lazima atoswe ili kuficha aibu kwa serikali halafu ataachiwa kwenye rufaa.

Inachofanya hii kesi iendelee ni mhimili ule uliojichimbia zaidi ya ile miwili.
 
Back
Top Bottom