Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu - Januari 19, 2022

Shahidi wa Leo ni wa upande gani?Mbona Naona kama vile ni wa upande wa utetezi?Maana kasema kwenye uchunguzi wake hakuona jinai kwenye hizo simu!

Sasa ameletwa na upande wa mashtaka kuja kufanyaje?
Nimeshangaa sana ushahidi wake kwa kweli! Kwenye uchunguzi hakuna jinai yoyote iliyoonekana yet wapuuzi wanafungua kesi.

Mungu wa mbinguni hutenda kazi zake kwa namna ya ajabu sana. Kamwibua huyu kunguru miongoni mwa watesi kumwokoa Mbowe na watu wake; leo milango ya gereza imefunguka yenyewe.
 

..mimi sio Polisi au mwanasheria lakini naona hayo mashtaka yako too general.

..watu wana mipango mingi, sasa mipango ya kufanya ugaidi ikoje? Vigezo vyake ni vipi?

..nikiweka vigezo ninavyovifikiria mimi sioni mipango ya kigaidi, na sioni upande wa mashtaka ukijitahidi kufikia kanuni ya " beyond reasonable doubt."

..kuhusu kipengele cha nia, hicho nacho kinathibitishwa vipi?

..Unaweza kweli kuthibitisha nia ya kuweka magogo barabarani bila kumkuta mtuhumiwa na magogo? Hayo magogo yalikuwa yatoke wapi? Walipanga kuyanunua, au kukata wenyewe?

NB.

..kama Mbowe alikuwa na mipango au nia ya ugaidi kwanini hakutumia vijana au wanachama wa Chadema?

..Kwa kawaida magaidi huwa hawakodiwi. Magaidi huwa ni watu waliokuwa indoctrinated.

..Na kuweka magogo barabarani sidhani kama kunahitaji makomandoo.
 

Ni kweli usemavyo. Lakini inatakiwa prosecution waje na sms angalau moja ya kudhibitisha kuwa Kuna maelekezo ya kumdhuru Sabaya yapo.
 
Wakati mwingine mjinga unamjibu kijinga
Rejea Yesu na Pilato
Pilato- wewe ni mwana wa Mungu
Yesu- WEWE WASEMA
Kesi ya Yesu ilikuwa ya kubambika Kama hii, PILATO alipokosa ushahidi, akawauliza wabambika kesi: Sioni kosa, ila Kuna desturi ya kumwachia mmoja, nimwachie Nani, Yesu au Baraba? Wabambika kesi(CCM),Mwachie Baraba(ambaye alikuwa jambazi).

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli usemavyo. Lakini inatakiwa prosecution waje na sms angalau moja ya kudhibitisha kuwa Kuna maelekezo ya kumdhuru Sabaya yapo.
wana mashahidi 28 bado 18 ngoja tuone wnavyoenda ila so far so good
 
Sasa huyo shahidi aliyeulizwa amejubu nini? Au ni nani atakayekuja na haya majibu iwapo forensic expert hajayajibu...!!

Mimi na wewe tusubiri, maana huyu shahidi ndio alikuwa the sucker punch kwenye hii kesi. Kama hatapatikana was kuyajibu haya maswali basi sidhani Kama Kuna kesi ya kujibu hapo. Hata confession ya kina lingwenya itakuja kuonekana haina nguvu kwasababu wanakirije kosa ambalo halipo?
 
Tusubiri- we are just half way. Ila utetezi walipewa kila kitu kwenye committal - wanajua kinachokuja mbele yao ila wameamua kudhalilisha mashahidi badala ya kushughurika na ushahidi dhidi yao.
 
Je baada ya kuunganisha ushahidi wa tigo na airtell pamoja na msg alizohack amepata mazungumzo yoyote yenye viasharia vya kufanya uhalifu kupitia fedha hizo zilizotumwa kwa njia ya simu alizochunguza ??🤣🤣😂


Huyu Hacker amelivua nguo jeshi la polisi na CCM kwa ujumla
 
Wakati mwingine akili inakurudia, mara inapotea! Hueleweki.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nakushauri usome sheria ya ugaidi- nimeiweka in one of my post kwenye post hii- kesi iko clear na ushahidi to the point vinginevyo kesi isingefika huku. SIKIA serikali ina maguvu makubwa sana - ikitaka kuweka Mbowe ndani hata bila kesi inaweza- kutakuwa na kelele sawa lakini atakuwa yuko huko. Hivi unajua sheria ya kuweka watu kizuizini ipo na haijafutwa ila kwa sababu viongozi wetu ni waungwana hawaitumii- kama ile sheria ya kunyonga- ipo ila hakuna anayeyonyongwa.
SASA KAMA NI HIVYO KWA NINI HII KESI IPO NA ITAKUWEPO MPAKA 2025 KWA HUU MWENDO WA MAPINGAMIZI SIJUI KESI NDOGO NDANI YA KESI KUBWA?
IGP alisema Mbowe si malaika ni mtu na ushahidi tunao- twende mahakamani
CHADEMA
1. Mbowe hawezi kukamatwa- kakamatwa
2. Mbowe hawezii kufikishwa mahakamani- kesi ipo
3. Kesi haina ushahidi- leo tuna shahidi wa 10
4. POLISI hajui PGO- BLAH BLAH
 
atakuja mtu wa sauti mtashangaa ila hamwezi kumkana Mbowe NAJUA mtasimama naye mpaka mwisho maana nyie ni kupe
Ng'ombe anapelekw a mnadani- kupe yupo
ng'ombe anauzwa- kupe yup tu
ng'ombe anachinjwa - kupe anabaki na ngozi
Ngozi inapelekwa kiwanda cha ngozi- kupe yupo tu mpaka amwagiwe acid
 
In my opinion, mpaka sasa serikali imeshindwa kuleta ushahidi wa kutosha. Inakuwaje mpaka shahidi wa10 anashindwa Kuja na ushahidi wa kujitodheleza? Kitendo cha shahidi wa kwanza kujikanyaga tayari ilikuwa ni walakini mkubwa.

Hii aibu kwa serikali itaokolewa na Jaji. Halafu wayamalize kwenye Mahakama ya Rufaa.

In my analysis, Mbowe lazima atoswe ili kuficha aibu kwa serikali halafu ataachiwa kwenye rufaa.

Inachofanya hii kesi iendelee ni mhimili ule uliojichimbia zaidi ya ile miwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…