Wakili JOHN MALLYA: Hizo ni fact Mpya
Jaji: alisema Jana kuwa Wana Extract na Kuprint, haiwezi kuzichanganua
Wakili JOHN MALLYA: Sawa Mheshimiwa Jaji
Wakili NASHON NKUNGU: Mheshimiwa Jaji nina maswali na majibu ya Mtobesya ya jana
Jaji: Umesoma wapi?
Nashon Nkungu: Wenzangu walikuwa wame rekodi
Jaji: Umetoa wapi, Naona una refer kwenye simu, wala huna karatasi
Nashon Nkungu: Basi Mheshimiwa Jaji naomba nikae.
Jaji: Inavyoonekana ni kama kuna source nyingine, Maana proceedings bado sija' certificatify, sasa huyo ana refer kwenye simu, inaonekana kuna source nyingine kwenye simu zaidi yangu....
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Technology imekuwa Kubwa Pia, maana hata sisi mawakili tuna Group la WhatsApp na tuna' share Taarifa na nyaraka mbalimbali humo ndani..
Jaji: Ndiyo Nimeona yeye kashika simu na ninachojua Mtobesya atakuwa kaondoka na simu yake, sasa yeye (Nashon Nkungu) anatoa wapi au ana source nyingine?
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naona tusifungue mambo mengine, itoshe tu kusema, hakuna wakili atavunja kanuni za Mahakama wala Kwenda Nje ya utaratibu wa mahakama au Taaluma yake, mengine ni mambo ya kibanadamu tu...
Jaji: tuendelee...