Yaliyojiri: Mapokezi ya Tundu Lissu Jijini Arusha - Ijumaa 14 Agosti, 2020

Yaliyojiri: Mapokezi ya Tundu Lissu Jijini Arusha - Ijumaa 14 Agosti, 2020

Kwa nini chadema wasiweke walinzi kwenye hizi ofisi?ata ccm wao wana walinzi ofisi zao zote,au wanataka zichomwe moto ili walielie kupata huruma za wananchi?

Jamani chadema kuna wasomi pls onyesheni tofauti kati ya chama chenye vijana wasomi na vyama vingine vinavyotafuta huruma ya magufuli mkate uende tumboni
Mbwa atabaki kua mbwa tuu hata Dodoma panakebinet yote ya mawaziri na ulinzi lkn lisu alimiminiwa risasi kwahiyo mbwa akilitaka lake lazima atafanikiwa
 
kweli CCM wameishiwa sera!

mwaka huu mtaambia nini watu????
 
kweli CCM wameishiwa sera!

mwaka huu mtaambia nini watu????
 
Ni Ijumaa tulivu.

Kama kawaida jiji la Arusha Kuna ubaridi asubuhi hii.Jiji likiwa katika hekaheka tangu Jana za Maandalizi ya mapokezi ya Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu.

Kanda ya Kaskazini hususan Jiji la Arusha ni ngome Kuu ya Chadema na akitoa salaam za kunikaribisha jijini humo Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Godbless Lema alisema mapokezi ya Mgombea wao wa Urais yatazidi Kanda nyingine zote alizokwishatembelea.

Tayari Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe akiongozana na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu hapo Jana walimlaki Lissu maeneo ya mkoani Manyara tayari kuongozana naye kuingia Arusha leo.

He kweli jiji la Arusha litavunja rekodi leo? Tusubiri tuone.

Molemo Media imekwishawasili jijini Arusha kuwaletea moja kwa moja kitakachojiri katika mapokezi hayo ya kihistoria.

Karibuni...

Taarifa za hivi Punde

Ofisi za Chadema Kanda zachomwa Moto.

Kuna taarifa zilizotujia hivi Punde kwamba ofisi za Chadema Kanda ya Kaskazini zimechomwa Moto usiku wa kuamkia Leo na watu wasiojulikana.Hapa ndipo mgombea wa Urais Tundu Lissu alipaswa kupokelewa kwa ajili ya kudhaminiwa.Tunatarajia kupata taarifa kwa kina zaidi asubuhi hii kutoka kwa viongozi wa chama.

Taarifa ya Awali kutoka Ofisi ya Chama Arusha.

*TAARIFA YA AWALI*

Usiku wa leo, watu ambao hawajatambulika hadi sasa, wamevamia ofisi zetu za Chadema Kanda/Mkoa na Wilaya Arusha, wamechoma moto kwa petrol na kufanya uharibifu mwingine. Tumeshirikiana na jeshi la zimamoto, polisi na wadau wengine hadi sasa.

Taarifa zaidi zitatolewa.

*KATIBU WA MKOA ARUSHA*
*[Ijumaa, 14 Agosti 2020.]*

Saa 3 Asubuhi

Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Godbless Lema anajitokeza mbele ya wanahabari na kutoa masikitiko yake kuhusu kuchomwa Moto ofisi za chama katika Kesha la ujio wa mgombea Urais Tundu Lissu.

Lema amesema hujuma hizo zinaashiria lengo moja kuvuruga ujio wa mgombea Urais hata hivyo akawatia moyo wananchi wasiyumbishwe na waendelee na mapokezi ya Mgombea Urais Kisha baada ya kuondoka kwake ndiyo chama kitatoa tamko rasmi.

Lissu azungumzia tukio akiwa Karatu.

Akihutubia umati mkubwa wa watu mjini Karatu akiwa njiani kuelekea Arusha Lissu amesikitishwa na vibaka waliotumwa kuchoma Moto ofisi za Kanda ya Kaskazini na akasema mkutano wake wa kusaka wadhamini jijini Arusha utafanyikia hapo hapo ofisi zilipochomwa Moto.
Kwani wanaochoma taasisi za serikali na shughuki za watu Arusha mbona wana jukikana? Ninaibu tuu serikali ina wafumbia macho..
 
Kwa nini chadema wasiweke walinzi kwenye hizi ofisi?ata ccm wao wana walinzi ofisi zao zote,au wanataka zichomwe moto ili walielie kupata huruma za wananchi?

Jamani chadema kuna wasomi pls onyesheni tofauti kati ya chama chenye vijana wasomi na vyama vingine vinavyotafuta huruma ya magufuli mkate uende tumboni
Nani kakuambia hakukuwa na mlinzi? Unapokea taarifa juu juu kisha una comment
 
Molemo,

Hiyo ofisi mmeichoma wenyewe ili kuweka hadithi zenu kwenye vyombo vya habari wazungu wenu mabeberu yaone kua mnaonewa,maana ofisi zenu hamuoni shida kuzichoma kwa kua ni kama tuvibanda twa kuuza juice na vocha.

Kama ni rahisi kuchoma vibanda vya vocha na juice, mbona hatuoni hivyo vibanda vikichomwa hapa Dar ili tujue ni rahisi hivyo?
 
We fala mbona umeshaambiwa mlinzi hajulikani alipo ama ulitaka uambiwe kipi ndo uelewe? Na pale area D mbona mwana alioga mvua ya risasi licha ya kuwepo walinzi tena mchana kweupe? Acha utoto.
asante ipo siku nitakuwa mkubwa na ndio utakuwa mwisho wa utoto wangu,tujadili oja,mazingira ya area D ni tofauti sana na hapo arusha,naamini wangekuwepo walinzi wa kutosha lisingetokea
 
Nipe wewe taarifa za uhakika vinginevyo ni walewale kutwa kulalamika kutafuta public sympathy
Sympathy itatafutwa kwako fala we!
Acha kuuzi watu kwa hoja za kijinga. Mlinzi umeambiwa alikuwepo na alitekwa na habari zake wataziongelea polisi wanaochunguza tukio, nini huelewi?
 
Back
Top Bottom