Uchaguzi 2020 Yaliyojiri mkutano wa kampeni za Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli akiwa Bukoba, Kagera

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri mkutano wa kampeni za Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli akiwa Bukoba, Kagera

Screenshot_20200917-014458.png
Screenshot_20200917-013805.png
 
Ama kweli nabii hana heshima kwao.
Hata akishinda Lissu mtampa kazi sana sababu sijui atawafanyia nini mridhike.
Kila la heri JPM tano tena.
 
Baadhii tu ni kama yafuatayo:
1. Kugeuza mapori yaliyotumika kwa uhalifu na ujambazi kuwa hifadhi ya taifa ( Burigi; Chato; Ibanda na Lumanyika)
2. Kulipa madeni ya kahawa kwenye vyama vya ushirika.
3. Kukarabati shule za sekondari za Kagemu, Bukoba, Rugambwa na Kahororo.
4. Kujenga shuke mpya za sekondari mbili; Nyakato na Ihogo kwa gharama ya shilingi bilioni 14.
Kwenye namb 2 na 4 ujiridhishe tena.
 



MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 16, 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo baada ya kumaliza wilayani Chato, mkoani Geita, Muleba leo yupo Bukoba Mjini mkoani Kagera Uwanja wa Gymkana.


MGOMBEA Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuhakikisha wanajenga mnara wa mawasiliano kati yao na Rais Dk.John Magufuli kwa kuchagua Rais, Mbunge , madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi( CCM).

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Byabato amesema katika uchaguzi hakuna sababu ya hao kufanya makosa kama yaliyofanyika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuchagua mbunge na madiwani wa upinzani.

"Bukoba Mjini tulikosea mwaka 2015 kwa kuchagua upinzani , na hivyo kukata mawasiliano kati yetu na Rais Magufuli.Huu ni mwaka wa kujenga mnara wa mawasiliano,naomba wote tumchague Dk.Magufuli kwa nafasi ya urais,mnichague mimi kwenye ubunge jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wabunge wote wa CCM,"amesema Byabato.

Amefafanua kuwa ni kweli maendeleo hayana Chama na ndio maana Rais Magufuli amefanya maendeleo makubwa bila kuombwa na mtu yoyote lakini kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Bukoba Mjini na Kagera Mjini ameleta maendeleo.

Ameongeza katika miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Magufuli wananchi wa Bukoba Mjini kunamaendeleo makubwa yamefanyika na kwamba Sh.bilioni 158 zimetumika kwa maendeeleo."Tunatambua kwamba yote hatukuomba lakini tumezipata fedha hizo kwa upendo mkubwa alionao kwa ajili yetu."

Amesisitiza Bukoba Mjini kuna taa za barabarani wamepata kilometa 13 za lami, wamepata mradi mkubwa wa maji wenye kuzalisha lita milioni 18 wakati mahitaji ni lita milioni 15 kwa siku na hivyo kubaki na ziada ya lita milioni tatu na kwamba yote hayo yamefanyika sio kwasababu waliomba bali yametokana na Rais Magufuli na mapenzi yake kwa wananchi.

Pia Sh.milioni 500 zimetolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya vituo vya afya na leo, miundombinu katika sekta ya afya imeboreshwa na kuimarika sana."Hayo yote hatukuomba katika miaka mitano lakini tumepewa.Nawaombeni wana Bokoba, tusifanye makosa tena.Tumchague Dk.Magufuli kwanza jina lake ni kubwa hata ukilitaja unasikia raha.

"Tujenge mnara wa mawasiliano ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kati ya wananchi na Rais wetu.Tunataka tukipiga simu kwa Rais tunaambiwa mawasiliano yapo na tunayoomba yanafanyiwa kazi, Bukoba iwe na mawasiliano mazuri na sio ukipiga unaambiwa Not reachable,"amesema Byabato.

----
Sehemu ya Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.24%2BAM.jpeg


WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.25%2BAM%2B%25281%2529.jpeg
Hivi CCM kwa nini mnapenda kusema kwa upendo wa Magufuli wakati aliomba kazi wananchi wakampa na analipwa kwa ajili ya hiyo kazi? Eti kwa upendo wa Magufuli wakati huo ni wajibu wake kisheria na tena hajafanya vya kutosha.
Upendo ni pale unafanya ajambo ambalo halipo kisheria unafanya kwa hiari yako. Kama Yesu alivyofanya kwa ulimwengu. Yesu akuomba kura za kuja duniani kuja kupata mateso kwa ajili ya watu. Ila alijitolea kufa kwa ajili ya watu. Huyo anatetea ugali wake mnasema eti kwa Upendo wa Raisi. Semeni anatimiza wajibu wake kisheria. Au mnataka asiwanyenyekee waliomchangua?
 
Ee bhana na leo Wana Kagera wamedhihirisha wazi kabisa wanampenda Magufuli na wanaipenda CCM na hata Kama mnafanya propaganda za kuwafanya wamchukie kwa sababu ya tetemeko wamewapuuuza

Check huo umati

Hakika Bukoba mmetisha sanaView attachment 1571714
Pole sana, unadhani hao waliokuwa hapo wote ni wenzenu, narudia tena pole sana. Magufuli hana hamu na Kagera. Cheki vidole viwili hivyo anavyooneshwa live bila chenga.
EiCTW4LXYAIOXsM.jpg
 
Hizo ndio Kiki ambazo mnatumia ili muelewele. Hizo picha ni za Jana je mbona hujatuma picha zote za Jana je kulikuwa na watoto? But also watu wanampenda Mheshimiwa Rais na baadhi ya sehemu watu hawajawahi kumwona Rais so Kama watu wamesikia Rais anakuja kwa Nini wasije kumwona????

Jana Lissu alituma picha za sehemu alipokwenda na kuambiwa katika kata ile hajawahi kumwona Mgombea urais so hata Jana watu hata Kama ni wanafunzi wanaenda kumwona Rais anayewasomesha bure
Inabidi mkubali tu kuwa ccm sasa hivi ndiyo inachukiwa kuliko kipindi chochote kile tangu tupate uhuru.
 
Inabidi mkubali tu kuwa ccm sasa hivi ndiyo inachukiwa kuliko kipindi chochote kile tangu tupate uhuru.
Kama huitaki si ukae kimya kelele za nn kelele nyingi haya imba sasa kila mtu na mapenzi yake
 
Bukoba hakuna shule ya msingi wanafunzi wanavaa sketi za rangi ya kijani, kama ipo shule hiyo naomba unitajie ni shule gani? Sitetei CCM bali huwa sipendi uongo
Kitu kama hujui siyo lazima u comment
 
Anaglia usije jinyonga baada 28 October Mzee atakapo tangazwa na kuapishwa
Mnadhani October 28 haifiki?

Tundu Lissu ndio Rais tupa kule huyo mshamba na limbukeni wa ndege
 
Watu wanampenda Magufuli Hadi basi na tarehe 28 utashuhudia Kama upinzani mtapata hata Jimbo moja Kagera

Hadi pale nchi hii itakapokuwa na tume huru kauli kama hizi zitaendelea kuwepo tu kwa sababu tume ndio ccm. That's all.
 
Back
Top Bottom