Chief Kabikula
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 7,567
- 9,037
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye namb 2 na 4 ujiridhishe tena.Baadhii tu ni kama yafuatayo:
1. Kugeuza mapori yaliyotumika kwa uhalifu na ujambazi kuwa hifadhi ya taifa ( Burigi; Chato; Ibanda na Lumanyika)
2. Kulipa madeni ya kahawa kwenye vyama vya ushirika.
3. Kukarabati shule za sekondari za Kagemu, Bukoba, Rugambwa na Kahororo.
4. Kujenga shuke mpya za sekondari mbili; Nyakato na Ihogo kwa gharama ya shilingi bilioni 14.
Bukoba hakuna shule ya msingi wanafunzi wanavaa sketi za rangi ya kijani, kama ipo shule hiyo naomba unitajie ni shule gani? Sitetei CCM bali huwa sipendi uongoYaani ccm wacheni vichekesho mnawakusanya wanafunzi kibao ndiyo mnajisifu mafuriko? Shame on you guysView attachment 1571667
Hivi CCM kwa nini mnapenda kusema kwa upendo wa Magufuli wakati aliomba kazi wananchi wakampa na analipwa kwa ajili ya hiyo kazi? Eti kwa upendo wa Magufuli wakati huo ni wajibu wake kisheria na tena hajafanya vya kutosha.
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 16, 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo baada ya kumaliza wilayani Chato, mkoani Geita, Muleba leo yupo Bukoba Mjini mkoani Kagera Uwanja wa Gymkana.
MGOMBEA Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuhakikisha wanajenga mnara wa mawasiliano kati yao na Rais Dk.John Magufuli kwa kuchagua Rais, Mbunge , madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi( CCM).
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Byabato amesema katika uchaguzi hakuna sababu ya hao kufanya makosa kama yaliyofanyika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuchagua mbunge na madiwani wa upinzani.
"Bukoba Mjini tulikosea mwaka 2015 kwa kuchagua upinzani , na hivyo kukata mawasiliano kati yetu na Rais Magufuli.Huu ni mwaka wa kujenga mnara wa mawasiliano,naomba wote tumchague Dk.Magufuli kwa nafasi ya urais,mnichague mimi kwenye ubunge jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wabunge wote wa CCM,"amesema Byabato.
Amefafanua kuwa ni kweli maendeleo hayana Chama na ndio maana Rais Magufuli amefanya maendeleo makubwa bila kuombwa na mtu yoyote lakini kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Bukoba Mjini na Kagera Mjini ameleta maendeleo.
Ameongeza katika miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Magufuli wananchi wa Bukoba Mjini kunamaendeleo makubwa yamefanyika na kwamba Sh.bilioni 158 zimetumika kwa maendeeleo."Tunatambua kwamba yote hatukuomba lakini tumezipata fedha hizo kwa upendo mkubwa alionao kwa ajili yetu."
Amesisitiza Bukoba Mjini kuna taa za barabarani wamepata kilometa 13 za lami, wamepata mradi mkubwa wa maji wenye kuzalisha lita milioni 18 wakati mahitaji ni lita milioni 15 kwa siku na hivyo kubaki na ziada ya lita milioni tatu na kwamba yote hayo yamefanyika sio kwasababu waliomba bali yametokana na Rais Magufuli na mapenzi yake kwa wananchi.
Pia Sh.milioni 500 zimetolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya vituo vya afya na leo, miundombinu katika sekta ya afya imeboreshwa na kuimarika sana."Hayo yote hatukuomba katika miaka mitano lakini tumepewa.Nawaombeni wana Bokoba, tusifanye makosa tena.Tumchague Dk.Magufuli kwanza jina lake ni kubwa hata ukilitaja unasikia raha.
"Tujenge mnara wa mawasiliano ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kati ya wananchi na Rais wetu.Tunataka tukipiga simu kwa Rais tunaambiwa mawasiliano yapo na tunayoomba yanafanyiwa kazi, Bukoba iwe na mawasiliano mazuri na sio ukipiga unaambiwa Not reachable,"amesema Byabato.
----
Sehemu ya Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
![]()
![]()
Pole sana, unadhani hao waliokuwa hapo wote ni wenzenu, narudia tena pole sana. Magufuli hana hamu na Kagera. Cheki vidole viwili hivyo anavyooneshwa live bila chenga.Ee bhana na leo Wana Kagera wamedhihirisha wazi kabisa wanampenda Magufuli na wanaipenda CCM na hata Kama mnafanya propaganda za kuwafanya wamchukie kwa sababu ya tetemeko wamewapuuuza
Check huo umati
Hakika Bukoba mmetisha sanaView attachment 1571714
NonsenseHayo ni maendeleo maana watu wanapita sehemu yenye mwanga ambapo hawawezi kutana na wahuni wowote barabarani
Inabidi mkubali tu kuwa ccm sasa hivi ndiyo inachukiwa kuliko kipindi chochote kile tangu tupate uhuru.Hizo ndio Kiki ambazo mnatumia ili muelewele. Hizo picha ni za Jana je mbona hujatuma picha zote za Jana je kulikuwa na watoto? But also watu wanampenda Mheshimiwa Rais na baadhi ya sehemu watu hawajawahi kumwona Rais so Kama watu wamesikia Rais anakuja kwa Nini wasije kumwona????
Jana Lissu alituma picha za sehemu alipokwenda na kuambiwa katika kata ile hajawahi kumwona Mgombea urais so hata Jana watu hata Kama ni wanafunzi wanaenda kumwona Rais anayewasomesha bure
Kama huitaki si ukae kimya kelele za nn kelele nyingi haya imba sasa kila mtu na mapenzi yakeInabidi mkubali tu kuwa ccm sasa hivi ndiyo inachukiwa kuliko kipindi chochote kile tangu tupate uhuru.
Kamshauri chakubangaKama huitaki si ukae kimya kelele za nn kelele nyingi haya imba sasa kila mtu na mapenzi yake
Kitu kama hujui siyo lazima u commentBukoba hakuna shule ya msingi wanafunzi wanavaa sketi za rangi ya kijani, kama ipo shule hiyo naomba unitajie ni shule gani? Sitetei CCM bali huwa sipendi uongo
Mwambie huyo debe tupuPole sana, unadhani hao waliokuwa hapo wote ni wenzenu, narudia tena pole sana. Magufuli hana hamu na Kagera. Cheki vidole viwili hivyo anavyooneshwa live bila chenga.View attachment 1572009
Hao wote ni umoja wa Vichaa ccm (UVCCM)Naona ID mpya tupu hapo juu.
Mnadhani October 28 haifiki?Anaglia usije jinyonga baada 28 October Mzee atakapo tangazwa na kuapishwa
Watu wanampenda Magufuli Hadi basi na tarehe 28 utashuhudia Kama upinzani mtapata hata Jimbo moja Kagera
Tundu Lissu ndio Rais tupa kule huyo mshamba na limbukeni wa ndegeLabda Rais wa TLS sio wa Tanzania
Watu wanasombwa ahead of time. Tunaona yote.Hii ni ya Muleba watu walitoka wapi? Na alikuwa anapita tu Jana hiyoView attachment 1571649