Hauelewi kinachoendelea afadhali utulie unyamaze tu.
Kila kituo kikimaliza kuhesabu kura kinapiga picha hio fomu ya matokeo na kutuma Nairobi.. Ikituma Nairobi vyombo vya habari na wanasiasa wanaziona na wanaeza kujumlisha wenyewe. Hichi ndo kimekua kikifanyika.
Lakini IEBC kutangaza mshindi ni lazima form zote original zisafirishwe hadi Nairobi na kukaguliwa kwamba kweli ni zile form zilizopigwa picha alafu ndo hesabu ya 'kikweli' itangazwe rasmi...
Kwahivyo hakuna 'hesabu mpya' inayofanywa hapa, IEBC tayari inajua mshindi ni nani, wanachofanya sahii ni ukaguzi wa form original kuhakikisha data iliotumwa mtandaoni inafanana na iliojazwa kwa form.
Hata we mwenyewe ukiwa na raslimali unaweza hesabu matokeo yote mwenyewe ukitaka (hili halijawahi tokea hapa Africa) enda kwa hii tovuti
https://forms.iebc.or.ke/#/ utapa form zote na unaweza jumlisha kivyako, kwa mfano naeza kwambia tafuta kura za diaspora ndo ni kidogo download na uanze kupiga hesabu alafu baadae utuambie kama hesabu hio itakua imetofautiana na ile ambayo iebc itatangaza rasmi..