Kwangu mimi Buhari ni failed president kwa muda mrefu. Ukianza kumfuatilia Buhari miaka miwili hii kabla ya uchaguzi ambapo yeye na genge lake walishtuka wanaweza poteza urais ndio utaona anafaa ila ni hafai kabisa.
Buhari ni retired General, alishaongoza nchi baada ya kufanya mapinduzi miaka ya 1980s akafanya transformation kwa civilian leadership. Alishindwa nini kupambana na Boko Haram na jeshi la Nigeria lote na uzoefu wake serikalini na jeshini?
Buhari na Boko Haram ni kabila moja la Fulani. Hao ndio tuseme Wamasai + Wakurya wa Nigeria ila wana fujo sana na wengi Waislamu kama walivyo raia wengi wa Kaskazini. Buhari na Boko Haram waliongea lugha moja wakaelewana, magaidi hawakupigwa na hawakufanya mashambulizi wakati Goodluck Jonathan alivyokuwepo mara nyingi tu wanateka wanafunzi na kuwaficha Sambisa forest. Boko Haram ilitumika kuidestabilize Nigeria GJ aonekane hawezi. Btw alikuwa mnyonge kama ilivyo kwa makamu wa Rais wa Kiafrika, alikuwa makamu wa Umaru Yar'Adua ambaye asingekufa Nigeria walikuwa wamepata the best president mgumu kupatikana.
Niliandika humu siku moja, ukitaka kujua Nigeria ni wapuuzi huyo Abubakar Shekau katafutwa na jeshi miaka sijui mingapi eti hawajui alipo, kila wakifanya operation anajua kabla. Wakaja ISWAP baada ya ISIS kupigwa pale Syria na Iraq, ISWAP hawakuwa zaidi ya 2000 kipindi wanamuua Shekau. Yani kundi halikukaa zaidi ya mwaka likamuua wakati jeshi lenye maelfu, silaha nzito na bajeti halikuweza muda wote huo. ISWAP walipigana na Boko Haram baada ya kutofautiana kwenye msimamo mkali, BH ni wahuni tu wanalipwa hela na ni biashara ya watu kwa namna fulani. Kuna maeneo ya Nigeria hawajawahi kanyaga.
Chad inazidiwa uchumi na Tanzania, inazidiwa na Nigeria zaidi ya mara kumi na imewapiga magaidi. Cameroon ilikuwa na performance nzuri kuliko Nigeria inaowazidi kila kitu. Ghafla mwaka jana mashambulizi dhidi ya Boko Haram yakawa makubwa, ghafla jeshi likawa na performance nzuri dhidi ya magaidi. Sasa ngoja uchaguzi uishe hizo nguvu za jeshi utashangaa zimeishia wapi.