Uchaguzi 2020 Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za CCM jijini Mwanza - Septemba 7, 2020

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za CCM jijini Mwanza - Septemba 7, 2020

Meko kakaliwa kooni uchaguzi huu. Mwenyewe alijua kampeni za mwaka huu zitakuwa mteremko kwake, kumbe sivyo ilivyo. Anavuja jasho utadhani mtu aliyefumaniwa.

Huyu ni mkuu wa kaya atakayeweka rekodi ya kutawala kipindi kimoja pekee.
Naona Kampeni zinamshinda Mkulu .... anahutubia badala ya kukampeni. Kwa kweli hotuba zinaboa na hazina mvuto. Hazungumzi na wananchi kama anavyofanya Lissu .... Kama hatabadili mkakati, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi!!
 
Toka kampeni zianze nimekuwa nikisikia maoni ya watu kuhusu hotuba za Rais Magufuli.

Baadhi ya maoni yalikuwa yanataja mapungufu na kasoro kadhaa katika hotuba zake. Leo nimechukua mda wangu kumsikiliza na nimefurahishwa na ubora wa hotuba yake leo; ama amejifunza kama wakosoaji walikuwa sahihi au wakosoaji walikuwa wanamsingizia.

Au pengine Mwanza ndiyo Game changer ya uchaguzi huu na bahati ya JPM.
NI MOJA KATI YA HOTUBA ZAKE BORA KABISA, UKIWA MWANZA NA UNAOMBA KURA YOU GOT TO BE VERY VERY SMART, MAANA MWANZA NDIYO DECIDING FACTOR YA URAIS WA TANZANIA, LEO NI RASMI MAGUFULI NI TANO TENA 2020-2025. Ni machungu upande wa pili, umati ule Tundu lissu itamchukua miaka 30 kuupata ndani ya mwanza na sehemu nyingine. hAHAHAHAHAAH Mbeya tunakuja kuwashika
 
Porojo tu za ndege na fiesta hamna kitu sifuri kichwani
 
Meko kakaliwa kooni uchaguzi huu. Mwenyewe alijua kampeni za mwaka huu zitakuwa mteremko kwake, kumbe sivyo ilivyo. Anavuja jasho utadhani mtu aliyefumaniwa.

Huyu ni mkuu wa kaya atakayeweka rekodi ya kutawala kipindi kimoja pekee.
Mtabaki kufoka lakini ndiyo hivyo tena subirini 2025-2030 mjaribu bahati yenu, siyo sisi ni wana Mwanza ndiyo wamesababisha.
 
Naona Kampeni zinamshinda Mkulu .... anahutubia badala ya kukampeni. Kwa kweli hotuba zinaboa na hazina mvuto. Hazungumzi na wananchi kama anavyofanya Lissu .... Kama hatabadili mkakati, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi!!
Kampeni zimeisha leo bwashee, impact ya mkutano wa leo hata asipopiga kampeni tena, achiwe lisu ahangaike peke yake hatapata pumzi ya bridge kilichofanyika. Mkutano umeangaliwa hadi na WHITE HOUSE kule marekani, chezea chuma wewe
 
Kazi tu kusomba watu kwenye malori na kuwalazimisha wanafunzi ,wafanyakazi na wanachuo kwenda kiwanjani
Screenshot_20200907-135929.png
Screenshot_20200907-135855.png
 
Meko kakaliwa kooni uchaguzi huu. Mwenyewe alijua kampeni za mwaka huu zitakuwa mteremko kwake, kumbe sivyo ilivyo. Anavuja jasho utadhani mtu aliyefumaniwa.

Huyu ni mkuu wa kaya atakayeweka rekodi ya kutawala kipindi kimoja pekee.
Dr.Bashiru alimdanganya wanunue wapinzani wakadhani wamemaliza kazi kumbe ndiyo kwaanza shuhuli inaanza upya
 
Mungu Hoyee
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Angalia hapo ITV wamemquote mzee baba- Ndege yeyote itatua CCm Kirumba Mwanza
View attachment 1561595

Bwaaaa bwahaaa, yaani nimecheka kwa nguvu ile mbaya. Naomba nisife ndani ya hii miaka mitano iwapo jiwe ataendelea kuwa rais wa nchi hii, sina hakika kama vichekesho hivi vipo huko ahera madukani
 
Leo mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli yupo jijini Mwanza baada ya kuwasili jana ambapo yeye na chama chake wanatarajia kuzindua kampeni zao jijini humo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza serikali.

Mwaka 2015, Dkt Magufuli na chama chake walipata ushindi mnono jijini Mwanza na viunga vyake. Je, wapiga kura wataendelea kuwaamini na kuwapa ridhaa? Kuwa nami kukujuza yatakayojiri leo kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi jijini Mwanza.
=====
Yaliyojiri

Dkt. Magufuli amesema: Tumefanya ukarabati wa Meli 5 na tumejenga Meli mpya kwa gharama ya Bil 152. Tumejenga vivuko vya MV Mwanza na MV Ilemela kwa Bil 2.7

"Nataka Meli zetu za MV Mwanza, MV Victoria na nyingine ziwe zinasafiri hadi Bukoba, Uganda, Musoma na kuja Mwanza"

Tumeanza kujenga Reli ya umeme na ili ikamilike ndiyo maana tumekuja tena kuwaomba kura. Mnaona Ndege kubwa za abiria na mizigo zinaondoka moja kwa moja hadi Ulaya.

"Inawezekana mkachagua wengine tutakuwa tumepoteza mipango ya kuiendeleza Mwanza"

Zamani maeneo ya huku ikiwemo Chato ilikuwa ukitaka kwenda DSM lazima upite Bukoba hadi Uganda, ukazunguke Kenya ndio uende DSM

"Yaani unaenda Makao Makuu ya Nchi yako ila lazima uzungukie Nchi mbili za jirani, haya sasa hayapo. Ukiona vyaelea vimeundwa"

Tunaupanua uwanja huu wa Mwanza, ndege yoyote kutoka nchi yoyote itatua hapa, tuongeze watalii, tukuze uchumi wetu.

Wapo wanaobeza atapigiwa kura na madaraja, watu wanaopita kwenye hayo madaraja, wanaotibiwa kwenye hospitali tulizojenga watanipigia kura Okt. 28.
======

Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha kofia Msanii wa Bongo Flavor Nasib Abdul Diamond ambaye alikuwa akitumbuiza katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza

View attachment 1561615

View attachment 1561614

View attachment 1561616

Ametamka popote uhuru au haki? Amesema atafanya nini kuhusu hayo? Kama hakuna bora angejipitia kimya kimya tu.
 
Ndiyo
Mwanza ndipo sehemu pekee ambayo hawapaswi kuiangusha CCM

✓ Barabara nzuri
✓ Wamenunuliwa meli
✓ Daraja la juu
✓ Uwanja wa ndege umepanuliwa vizuri
✓ Biashara za samaki zimeboreshwa siku hizi wanasafirisha kwenda nje ya nchi

Na mengineyo
MELI IPI ILIYONUNULIWA?>
 
Bwaaaa bwahaaa, yaani nimecheka kwa nguvu ile mbaya. Naomba nisife ndani ya hii miaka mitano iwapo jiwe ataendelea kuwa rais wa nchi hii, sina hakika kama vichekesho hivi vipo huko ahera madukani
Ndiyo kazi mliyobakiza Mzee baba kawatuliza, bado Mbeya kwenye kambi yenu ya ukimbizi mwaka huu lazima muombe poo na kazi ndiyo kwanza imeanza. Kampeni za ccm zilianza rasmi pale uwanja wa kambarage SHYTOWN, sasa ni bandika bandua hadi 28 October, hadi mpoteane makamanda
 
Toka ameingia madarakani mkuu, mpaka ninasema ni bora ajirecord kama vile vispika vidogo vya kuuzia dawa ya mende na simu za kichina. Na kuhusu nyomi hamna shida maana nyomi linafuata fiesta.
😂#nakazia ajirekodi kbs
 
Huwezi kusema haya yalikuwa mafuriko,hapana ni shukrani za wananchi wa Mwanza kwa mambo mazuri aliyowafanyizia JPM kwa miaka minne na nusu Maana 2010- 2015 ulikuwa huwezi kumwambia mwananchi wa Mwanza juu ya Ccm akakusikiliza. Ccm ilikuwa imewakera watu wa mwanza. Chadema ilikuwa na nguvu mithili ya mamba. Lakini kazi nzuri ya JPM imeisafisha Ccm Mwanza. Na hii iliyokuwa ngome ya Chadema ndio waisahau tena.

Ccm ya JPM imewafanyia makubwa watu wa Mwanza kuanzia kuimarisha miundo mbinu,afya, elimu na kuhakikisha wakazi wa milimani aka golani wanauhakika wa makazi badala ya kubomolewa nyumba zao.

Achana na hayo madogo makubwa kabisa kumbe yale makubaliano ya ya Barrick na serikali ya Ccm ambayo Tundu Lissu na Chadema yake alikuwa anayapinga yanaenda kunuifa Mwanza kwa makubwa mno. Mojawapo ni kuimarisha barabara toka Mza mpaka Bulyanhulu.

Kwa ufupi tu ni kuwa Chadema Mwanza sidhani kama mtapata hata Diwani maana JPM amewakonga moto wanaMwanza. Na ninyi ndio mlikuwa na kiherehere kupinga Twiga Minerals Ltd isianzishwe ili watanzania na watu wa Mwanza wasipate manufaa.
 
Back
Top Bottom