Uchaguzi 2020 Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za CCM jijini Mwanza - Septemba 7, 2020

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za CCM jijini Mwanza - Septemba 7, 2020

Mwambieni aombe kura sio kulazimisha kura ? Sasa mbona mnajaza watoto Tena chini ya miaka kumi na nane ? Aiseee mmeishiwa , mgombea wenu mwingine huko Zanzibar Hussein Mwinyi kasusiwa msikiti ,watu hawataki kuswali na mnafiki .Angalieni kwenye michoro vitoto vilivyojazwa CCM Mpaka huruma.View attachment 1561522
Unaifahamu CCM Kirumba kweli wewe?
 
bila usafiri kubeba walioko nje ya miji tunahutubia 30% ya watz....
ukikusanya na mabasi unawafikia 70%.

leo tunabeza kwa ujinga wetu ... soon tunalia tumeibiwa kura
Tunasubiri usafiri tuje tujaze uwanja
 
Leo mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli yupo jijini Mwanza baada ya kuwasili jana ambapo yeye na chama chake wanatarajia kuzindua kampeni zao jijini humo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza serikali.

Mwaka 2015, Dkt Magufuli na chama chake walipata ushindi mnono jijini Mwanza na viunga vyake. Je, wapiga kura wataendelea kuwaamini na kuwapa ridhaa? Kuwa nami kukujuza yatakayojiri leo kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi jijini Mwanza.

=====

Yaliyojiri

Dkt. Magufuli amesema: Tumefanya ukarabati wa Meli 5 na tumejenga Meli mpya kwa gharama ya Bil 152. Tumejenga vivuko vya MV Mwanza na MV Ilemela kwa Bil 2.7

"Nataka Meli zetu za MV Mwanza, MV Victoria na nyingine ziwe zinasafiri hadi Bukoba, Uganda, Musoma na kuja Mwanza"

Tumeanza kujenga Reli ya umeme na ili ikamilike ndiyo maana tumekuja tena kuwaomba kura. Mnaona Ndege kubwa za abiria na mizigo zinaondoka moja kwa moja hadi Ulaya.

"Inawezekana mkachagua wengine tutakuwa tumepoteza mipango ya kuiendeleza Mwanza"

Zamani maeneo ya huku ikiwemo Chato ilikuwa ukitaka kwenda DSM lazima upite Bukoba hadi Uganda, ukazunguke Kenya ndio uende DSM

"Yaani unaenda Makao Makuu ya Nchi yako ila lazima uzungukie Nchi mbili za jirani, haya sasa hayapo. Ukiona vyaelea vimeundwa"

Tunaupanua uwanja huu wa Mwanza, ndege yoyote kutoka nchi yoyote itatua hapa, tuongeze watalii, tukuze uchumi wetu.

Wapo wanaobeza atapigiwa kura na madaraja, watu wanaopita kwenye hayo madaraja, wanaotibiwa kwenye hospitali tulizojenga watanipigia kura Okt. 28.
======

Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha kofia Msanii wa Bongo Flavor Nasib Abdul Diamond ambaye alikuwa akitumbuiza katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza

Hili swala la kujaza watoto wadogo kwenye kampeni limekaaje??
Screenshot_20200907_174846.jpg
 
Ndiyo
Mwanza ndipo sehemu pekee ambayo hawapaswi kuiangusha CCM

✓ Barabara nzuri
✓ Wamenunuliwa meli
✓ Daraja la juu
✓ Uwanja wa ndege umepanuliwa vizuri
✓ Biashara za samaki zimeboreshwa siku hizi wanasafirisha kwenda nje ya nchi

Na mengineyo
Barabara nakataa
 
Mimi naona wanaomshauri JPM awaangalie kwa jicho la tatu, Mimi ni CCM lakini hii ya kuachisha watoto shule ili tuwajibu wapinzani kwamba tumejaza halileti picha nzuri maana inaonyesha Sasa tumekosa hoja, wanaopiga Kura wapo majumbani na kwenye kazi wakiwa wanasubiri hoja siyo sindimba za upinzani za kujaza watu.
 
Kwanza mnamchosha hata Raisi maana Mwanza ni kubwa kwelikweli Sasa kumsimamisha mtu aongee sehemu zilizokaribiana inamaanisha nini, igoma, nyakato, buzuruga, mabatini ni sehemu zilizokaribu Sana watu wangeweza kukaa sehemu moja wakapewa hoja.
 
CDM walidai Lissu kaondoka na kijiji mwanza, wakaonywa Magufuli akitua hapo anaondoka na jiji zima la mwanza.

Halafu huo umati wa Mwanza cha mtoto ngoja Magu afike Dar alipowagusa watu wengi zaidi ndio tutaelewa nini maana ya umati kufurika.
Kama dar nita ondoka niende moro nikae siku mbili kisha nirudi dar maana jam ya hapo sijui itakuwaje.
 
Acheni basi kujaza watoto wadogo na kulazimisha watumishi kuja kungeza idadi ya watu ,muwe na aibu nyinyi kijani kibichi , Mara
IMG_20200907_190746.jpg
IMG_20200907_165823.jpg
mumulazimishe mama Maria Nyerere mna laana nyie , yeye ndio aliwatuma msiajiri , msiongeze mishahara , msipandishe madaraja , msilipe wastaafu kwa miaka mitano ?
 
Watanzania tumeshuhudia maiti za Watanzania wenzetu zikiokotwa kwenye fukwe zikiwa zimefungwa mawe na vyuma na nyingine zikiwa kwenye viroba...
Ana visasi,siyo kiongozi bali mtawala katili kwa watu/raia wenzake.
 
Back
Top Bottom