Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Asante mmekitendea HAKI chama na Wanachama, sasa kazi imeanza[emoji123]
 
Hivi we kwa akili yako unadhani lissu anaweza kuwa Rais??
 
Updates:

3 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Toka Mlimani City : mkutano wa Baraza Kuu wa Chadema:

Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA wamepiga kura kupendekeza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapigia kura ifuatavyo :

Wajumbe 442 wa Baraza Kuu wapiga kura :
Matokeo: Tundu Lissu 405 , Lazaro Samuel Nyalandu 36 na Dr. Mayrose Kavura Majinge 1.
 
Updates:

3 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Toka Mlimani City : mkutano wa Baraza Kuu wa Chadema:

Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA wamepiga kura kupendekeza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapigia kura ifuatavyo :
wajumbe wanazidi kutrend
 
HABARI MPYA: Tundu Lissu amependekezwa na wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema kuwa mgombea urais wa Chadema kwa kupata kura 405 sawa na asilimia 91 ya kura zote 442. Lazaro Nyalandu amepata kura 36 na Dk.
 
Hotuba ina spana kibao
mimi kwa uzalendo wangu naomba hotuba ya Mbowe isisambazwe wala kutafsiriwa kiingereza na kifaransa, itamuaibisha sana mtu flani, pease please kuweni wasiri, mambo ya chumbani msitoe
 
Ndoto zetu za kuiona Tanzania salama, Tanzania isiyo na WASIOJULIKANA Tanzania ya Watanzania wanaoishi kwa furaha kubwa na kupendana si hii iliyojaa HOFU, CHUKI za KUTISHA, KUTEKANA, KUTESANA, KUUANA inaanza kupata matumaini kwamba inaweza kabisa kuwa KWELI. Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana.

Shida ya viongozi wa Chadema si kwenda Ulaya na Marekani, shida yao ni kuwatumikia wananchi.

Jibu ni TAL kama hutaki kunywa sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…