Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Kati ya makosa makubwa ambayo CHADEMA wanapaswa kuyaepuka kwa gharama yoyote ni kuacha kumpitisha Lissu.

Muda wa majaribio uliisha kipindi cha Lowassa hivyo makosa ya 2015 yasijirudie tena. Mbali na uwezo wa kifedha Nyalandu hana ushawishi wowote ndani ya Chadema ,kwa kifupi hakuna mtu wa kumpa Nyalandu kura.

Naamini Nyalandu yupo kwa ajili ya kumsafishia Jiwe njia apite bila kipingamizi na mwisho wa siku Nyalandu maslahi yake yanalindwa.
Asante mmekitendea HAKI chama na Wanachama, sasa kazi imeanza[emoji123]
 
Hongereni wajumbe wote CDM na wagombea wote...
Kazi sasa inaanza... hakuna kulala..
Nchi inahitaji mabadiliko makubwa... liwalo na liwe--- NEC heshimuni haki sawa kwa wagombea wote wa vyama vyote. wapeni uwanja sawa..hizi habari za kuwaengua watu kwa technicality ziishie huko huko kwenye coridors zenu... Tanzania ni yetu sote, watoto wa nyumba moja - tupendane na tuijenge nchi yetu kwa kadri ya ushindi wa halali..

Wote CCM na CDM Wamefanya kura za wazi- hakuna namna, tuleteeni njia ya uhesabuji wa kura kama wa CCM na CDM- uwazi na Ukweli- namna bora ya kumuenzi mkapa...
Hivi we kwa akili yako unadhani lissu anaweza kuwa Rais??
 
Updates:

3 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Toka Mlimani City : mkutano wa Baraza Kuu wa Chadema:

Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA wamepiga kura kupendekeza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapigia kura ifuatavyo :

Wajumbe 442 wa Baraza Kuu wapiga kura :
Matokeo: Tundu Lissu 405 , Lazaro Samuel Nyalandu 36 na Dr. Mayrose Kavura Majinge 1.
 
Updates:

3 August 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Toka Mlimani City : mkutano wa Baraza Kuu wa Chadema:

Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA wamepiga kura kupendekeza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapigia kura ifuatavyo :
wajumbe wanazidi kutrend
 
Hayo ndiyo matokeo halisi mkuu tayari ishajulikana
Sijasema sitaki ila yale siyo matokeo halali.
Screenshot_20200803-201612.jpeg
 
HABARI MPYA: Tundu Lissu amependekezwa na wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema kuwa mgombea urais wa Chadema kwa kupata kura 405 sawa na asilimia 91 ya kura zote 442. Lazaro Nyalandu amepata kura 36 na Dk.
 
Hotuba ina spana kibao
mimi kwa uzalendo wangu naomba hotuba ya Mbowe isisambazwe wala kutafsiriwa kiingereza na kifaransa, itamuaibisha sana mtu flani, pease please kuweni wasiri, mambo ya chumbani msitoe
 
Ndoto zetu za kuiona Tanzania salama, Tanzania isiyo na WASIOJULIKANA Tanzania ya Watanzania wanaoishi kwa furaha kubwa na kupendana si hii iliyojaa HOFU, CHUKI za KUTISHA, KUTEKANA, KUTESANA, KUUANA inaanza kupata matumaini kwamba inaweza kabisa kuwa KWELI. Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana.

Shida ya viongozi wa Chadema si kwenda Ulaya na Marekani, shida yao ni kuwatumikia wananchi.

Jibu ni TAL kama hutaki kunywa sumu.
 
Back
Top Bottom