Yamenifika shingoni sijui la kufanya mimi

Huyo amaweza akuwa sio Biological father wako,muulize vizuri Mama yako.
 
I’m
upo sahihi jana kuna mtu alimieleza mama yake alimtelekeza kwa bibi yake bila sababu na yupo hai
Akaona haitoshi akamtumia na majini
Yaani ulimwengu huuu
Wazazi wengine sio kama wazazi
 
I’m

upo sahihi jana kuna mtu alimieleza mama yake alimtelekeza kwa bibi yake bila sababu na yupo hai
Akaona haitoshi akamtumia na majini
Yaani ulimwengu huuu
Wazazi wengine sio kama wazazi
Alimtumia majini?
Japo sio jambo zuri, ila lazima huyo mtoto alipatikana kwa majuto sana.
 
Sasa mkuu mwantumu kafikaje hapa😅
Kina mwantum ndio wana hurka za kulia lia.
Ila kina hamdala kiuno kazi yetu ni kuamua panapostahiki.
Umri wake jamaa mie nishaoa na natizama maisha mengine.
Yeye anakaa kulialia nini afanye!??
Anatakiwa atambue anapaswa kujenga maisha yake na legacy yake kuanzia sasa.
Maana hapo anaishi katika legacy ya wazee wake achomoke akajenge legacy yake awe na uhuru wake.
Wakimtaka watamtafuta,haina haja ya yeye kukaa nao kikao wala nini.
Ila akiondoka aondoke kwa wema tu.
 
Nilitaka kutumua lugha ngumu sana, ila kwa vile umesema unaumwa ngoja niache.

Muhimu, sepa hapo home. Kama umekaa kwa wazazi wako, ukala na kukua mpaka kufikia miaka 26 unawadai nini hao watu?

Sio kila mtu anaweza kukuonyesha upendo, na sio lazima, Amini ya kua washatimiza majukumu yao na kilichobaki ni wewe kuamka na kutimiza majukumu yako no matter how hard they are.

Workup nigger, Acha kulia lia, acha kubembeleza hao wazee washenzi, Huenda unavo teseka wao ndo wanapata relief.
 
Alitokea folk alikuwa anaumwa pancreatic cancer ambayo imefika stage four
Moja ya AHADI aliyo iacha hapa jf ni kuwa akipata dawa kutoka Kwa mtu humu atampa 1M folk

Umesema kuwa vipimo vyako vinachukua more than 5 days

Je! Ni wewe tukujuaye umerudi kutoka kuzimu??
 
Muhimu ni kukubaliana na Hali iliyopo, halafu jipange uweze kusonga mbele, watu wa muhimu katika maisha yako wanaweza kukufanya ukayachukia maisha lakini kama una afya nzuri jikung,Ute nyanyuka uende zako,maana mpaka kufika umri wako hakuna kitu usichokielewa.
 
Mkuu pole sana na huo mkasq uliokukuta ndio familia za Kiafrika zilivyo huwa hazieleweki kabisa, Kwanza jikubali na jiamini kwamba unaweza. Mimi nilishawahi kuandika mkasa wangu humu mbona weww unachopitia ni cha kitoto sana ?
Maisha sio kulia lia na kutaka huruma, ukitaka uonewe huruma maisha yatakunyanyasa sana na dunia utaiona chungu.
Jikubali kwa sababu harakati za kupambana unaziweza na vile vile una nguvu na uwezo wa kufanya shughuli basi hilo ni jambo zuri.
Jenga mahusiano mazuri na watu, kuwa mnyenyekevu na usijifanye kwa sababu ni graduate basi unajua kila kitu hapo utaiona dunia chungu.
Siki nzuri zitakuja kwako naada ya hayo magumu unayopitia. Kikubwa Imani, jitihada na adabi mbele za watu mbona nuru ipo tu.

Folk Part II hebu angalia background yangu hii hapa utajiona kumbe wewe una nafuu mara elfu 10000

Maisha sio kulalamika, ni kupambana tu...
 
Kumbe umesoma hadi chuo kikuu?! Achana na hao wazazi wasiokujali kata mbuga nenda popote kaanze maisha wala usichague kazi. Usihangaike nao sio wewe wa kuwatafuta wao bali wao ndio wa kukutafuta wewe. Inasikitisha sana ila hakuna jinsi sio watu wazuri hao ondoka hapo nyumbani katafute maisha tena mbali kabisa. Pia kaa vizuri katika maombi na sala isijekuwa wazazi wako ni washirikina au wachawi kwa maana watu hao hawana huruma hata kwa watoto wao. Jihadhari sana!
 
Pole sana mkuu kaa nae chini ongea nae kwa upole umueleze hisia zako, Je mama yako nae
wanafanana tabia.

Je vipi kwa ndugu zako wengine wao wanapitia hali hiyo hiyo?
Kiufupi hata nao hawaelewani kivile ninachopitia mama naye anahis ivoivo huku naye baba anahis kupitia magumu kiufupi ni visa juu ya visa ,,, mshua anapenda kujiongeza negativity sana hata kama wewe unamshilikisha mfanye kitu cha maana unaweza shangaa kakuzushia unataka kumuibia kupitia icho kitu na hataki kuonyesha ushilikiano wowote ilitakiwa wajenge nyumba sehemu fulani nilikuwa naamini yeye atakuwa wa kwanza kufuatilia ila hana mda kabisa na tanulu linamongonyoka tofali zinazid kuteketea ukijikologa umuulizie tunafanyaje wewe ujue unajitafutia matatizo
 
Ahsante sana mkuu ubarikiwe kwa ushauri wako,,,kinachonitesa apa ni mambo ya haso zangu zipo sehemu anayokaa bas ni mtu wa kunisemea ubaya kwa watu wanaonizunguka kiufupi watu wanaishi na mimi kwa maneno ya baba ndo kinachoniuma
 
Ahsante mkuu ubarikiwe,,,ingekuwa tu mtu mwenye roho nyepesi angekuwa ashawatamkia labda ni nyie mmeniroga na mnafurahi kuniona nateseka ivi mimi kuna sehemu moja ya mgongo pananisumbua ila huwezi amini baba alishusha mifuko yake mi6 ya mbolea mbali kidogo na home akaniambia niitoe pale njian niipeleke home wakati alikuwa na uwezo wa kusogeza gari likatua karibu na home nilijikaza nikabeba huku nikifikilia kwa hii hali ananichukuliaje nikafunika kombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…