Yamenifika shingoni sijui la kufanya mimi

Wewe ondoka hapo kwenu sio kujiliza jiliza,kama unataka kuwasaidia utawasalimia na kuwasaidia Ukiwa mbali
Sawa mkuu,,, ila mimi nia yangu nilikuwa napenda tu ushirikiano wa kifamilia ndugu,,,imagine hela ni yako alafu wewe unamuomba tu kukusaidia labda akanunue huko anakojua ni rahis kupata icho kitu anakukunjia
 
Umri wa miaka 26,,,
Acha kulaumu chukua hatua
Hatua nimechukua mkuu ila ivo vitu ninavyofanya ananikunjia kiufupi ni mtu hataki ushirikiano na mimi,,,huyu mshua anafani moja ivi namimi najua iyo fani kwa kuwa yeye yuko bize mda mwingi nikasema bas akipata kazi ya iyo fani akutage nimeweka sawa ivyo vitu akakunja labda ukimuuliza hiki kifaa vipi napataje anakwambia katafute vyako wakati mi nilikuwa najua yeye ni mzoef anajua wap vinapatikan kirahis,,,mwisho wa siku akanambia niache kutengeneza vitu walivyomletea yeye kwa kuwa alikuwa anajua mimi sijulikani wanaleta ivyo vitu kwa sababu yake
 
Pole mkuu.Sasa inakuwaje mpaka mama unakosa sapoti yake?Hii inafikirisha kidogo.Au wali ku adopt bila ya wewe kujua ?Mana wakina mama huwa wako tayari kufa na watoto wao,sasa kwako inakuwaje baba na mama lao liwe Moja?
Ni watu wa kurushiana mpira kila mtu anasema huyo ndo inabidi awajibike huku mimi ninayetakiwa nitimiziwe nabaki njiapanda pasipo msaada wowote
 
Ahsante mkuu,,,ila najua ningeweka wazi sana kuna watu watajua tu ni mimi hii kitu known sana mkuu
 
Ahsante ndugu hata hapa nilipo asset zangu zinaniwezesha kujitegemea kinachonitesa ushilikiano na aman na wazaz haipo
 
Ahsante ndugu ubarikiwe kwa ushauri wako nimeupokea kwa mikono miwili
 
Kwa nilivyosoma baba yako kuna namna anazingua ila wewe pia nawe unazingua sana.

Umeshakuwa sasa pambania maisha yako, ukitaka kuijenga kesho yako achana kabisa na kuwaza yaliyopita kwa sababu hutobadili kitu utaishia kulaumu tu.

Be a man, be strong hao ni wazazi wako kumbuka msaada sio lazima wewe ni mtu mzima unapaswa ujitegemee kwenye mambo mengi. Ukingoja upewe sapoti kwenye kila linaloendelea kwenye maisha yako kuna siku haitokuwa hivyo kutokana na uhalisia wa maisha. Ukishavuka miaka 18 wazazi utawaonea bure kuwabebesha lawama.

Ishi na hili kichwani mwako "HAKUNA WA KUJA KUKUSAIDIA KUISHI MAISHA YAKO". Pole sana kwa unayopitia usikate tamaa.
 
Ahsante mkuu ubarikiwe nimekuelewa
 
Acha kulalamika humu watu wanapitia magumu lakini wameamua kukomaa kulalamika hakusaidia hata kama huna kitu Ondoka tafuta ustaarabu wako tu. Kulalamika hakukusaidii wala hakubadilishi kitu. Ondoka hapo nenda kwingine kaanze maisha mapya. Usilazimishe mahali ambako hupendwi. Mimi nilitelekezwa nimetoka kupata skull fracture na nilipambana tu. Ondoka hapo
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako ubarikiwe sana mkuu
 
Ahsante ndugu ubarikiwe umenena vizuri kinachoniumiza niyeye kutokufurahia ninavyovifanya yan anakunja sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…