Yamenifika shingoni sijui la kufanya mimi

Wazee wengine nuksi tu kama wote ni wazaz halisi sepa kakae mbali kama ni mama wa kambo basi ndo sababu uzilazimishe kupendwa we kafanze yako wakizeeka hao itakuwa zamu yako kupeta nawe utakuwa umeshika mpini
 
Ni story ya kutunga au ni uhalisia? Kama ni uhalisia hao ni wazazi walio kuzaa au sio?

Na je ulishawahi kuongea nao ukaeleza duduku zako juu yao?

Asilimia 90 ya Wazazi wàpo hivyo.

Màtukio ya namna hiyo yanawapata Watu wengi Sana hasa kutoka bara la Afrika.

Mzazi anayetegemea kupata chochote Kwa Mtoto hana tofauti na mfanyabiashara.

Mungu pekee ndiye wakumtegemea, yeye hahitaji chochote kutoka kwako
 
Pole Sana Ila wazazi ni watu muhimu you need to respect them haijalishi wanaku-treat vipi.

Kama unapitia haya mambo

Financial broke
@clonical disease

Lazima hizi hali zitakufanya uwachukie WATU Sana .


Ushauri .

Be positive
Love ur parents
Jiandae kwa lolote don't afraid kuhusu kufa au kuishi.


Pambania Afya yako .

Umesema kuhusu sherehe, sherehe ni mambo madogo Sana in our life.


Pia jaribu kuwa giver na sio taker.
 
Mara nyingi huwa naandika kuwa tatizo namba moja la waafrika ni ujinga...

Pindi waafrika watapoacha kukumbatia ujinga, hakika mambo mengi yatabadilika...

Ndugu mleta mada , acha ujinga...
 
We piga chn huyo otherwise unajtafutia laana pga chn wote wawili tembea zako mi mzee nlishatemana naye kbs stak anijue na stak nimjue kila mtu apambane kivyake na nnahisi iktokea ametangulia uwenda kama taenda bs taenda kama mtu baki tu au staenda kbs. Pga chn kapambane kwngne badili namba waskupate kwsha.
 
Ndio wazazi wengi wa Kiafrika walivyo mkuu, sisi kule kwetu tunawaita
Wajerumani. Yani ni wazee wenye ukatili fulani hana muda wala
urafiki na watoto. Na mara nyingi ni wabinafsi na vitu vyao,

Wanataka ukatafute vitu vyako sio ufanye maendeleo kwenye
eneo lake. Hivyo bora uelewe tuu hivyo.

Wewe kama upo mikoa ya kusini sijui ni Mtwara au Lindi nyie si
Mjomba ana nguvu sana ulishaongea na mjomba?
 
Pia ni wewe mwenyewe ndio unajua ukweli. Nikuulize je wazazi wako wana viashiria vya kuwa washirikina? Nimeona mikasa kama hii ya wazazi kukataa watoto na kuwa wakatili sana kwa watoto wao wengi wa wazazi hawa unakuta ni wachawi na wamejaribu kuwashawishi watoto wao wawe wachawi ila wamekataa sasa wazazi wanawatesa ili kuwashinikiza wakubali.
 
oya dogo
hapo hauna wazaz aiseee hap ni wachawi yani kiufup wanatabia za wachaw maana hata mama mzaz huwa hawez kumfanyia mtoto wake wa kumzaa hivo hata kama utamkosea nn yan hawez kabsa sasa hao unaokaa nao huenda walkuzaa baat mbaya na hawana mpango na ww kwaio kua makn na hata uo ugonjwa huenda wanaujua ndo mana hawakup sapot upone
kwaio dogo tembea fanya mamb yako haina haja ya kuongea nao na kutia uluma amua maamuz magumu we mwanaume toka magetoni
kwanza nashangaa umemalza chuo ela umepata et bado unakaa nyumban yan we jamaa ni mfnyu. wa akili na degree yako
ama hapo kwenu ondoka kabsa na kajtafute hao wenyewe watakufata aiseeee
kaaa nao mbali sio wema kwako hata kama walkuzaa au huenda bmkubwa wako japo aliolewa akachepuka faza akajua sasa katka.kutunza heshima akaamua kuvunga ndo mana au almkuta mamako na ujauzto nn
sema kikubwa jitafute na je hauna ndugu kwan mbona unahangaika huku jf akat ndugu zako wapo upande wa mamako na babako emb watafute uwaulze juu yako toka utoto wako mpaka sasa wana kipi wanafaam pia uulize juu ya wazaz wako kwa wao huwa wanawafaam vp toka huko mwanzon mpaka sasa
ACHA KUTIA ULUMA DUNIA YA SASA HAINA HURUMA NA VJANA WANYONGE KAMA WW
JARBU KUJFUNZA NJIA NGUMU YA MAISHA NA UKFANKIWA N WW UKSHINDWA PIA N WW WAO NDO KWANZA UKISHNDWA WATAENDELEA KUKUCHAWIA UKFANIKIWA WATAKUJA NA BADO WATATAKA KUKUDIDIMIZA
Kwaio amua acha kulialia we wakiume
 
Hapo mwisho kwenye hujawahi kufanyiwa sherehe nimecheka sana.
Nikirudi kwenye mada,binafsi nimepitia hali kama yako,mzee wangu hajawahi kunipa senti kumi yake licha ya kuwa alikuwa mwalimu mwenye mshahara.
Alipostaafu 2006 akaniambia anataka anipe 5m nifanyie mtaji kwasababu hajawahi kunisadia.Hakunipa chochote ni porojo.

Nilipambana biashara hapa na pale nikanunua daladala route ya Mwenge _Bagamoyo mwaka 2008.
Hapo ndoto yangu ya kusoma ikarudi,nikajisomesha QT namshukuru Mungu nilitoboa kote,2012 nikaingia chuo kikuu na mkopo nikapata (BAED)
Baada ya kumaliza chuo nikapata kazi ,nikafundisha miaka 3 nikaacha kwasababu sikuona kama ndoto zangu zitatimia kwenye kada ya ualimu,hivyo nikarejea kwenye biashara.

Wakati wote huo mzee wangu amejiweka mbali na mimi hata nikimpigia simu anaongea ile kimachale haraka haraka ili nisimuombe kitu kumbe hajui niko vizuri wakati huo.

Point ambayo ndio tuliagana rasmi na sidhani kama nitapiga u turn, ni wakati nataka kuoa,nikamtaarifu kwa heshima tu akasema ni jambo jema tuko pamoja atanipa ushirikiano nk.Kinyume chake hakufanya chochote hata kwenda ukweni alipiga chenga akidhani kwamba nitamuambia atoe mahari (kama ilivyo desturi ya kwetu )
Kutoka hapo hatuwasiliani kabisa zaidi ya miaka 3 sasa.Habari zangu anasikia kwa ndg zangu,kijana kajenga ghorofa pale,kijana kanunua gari ya mbunge 😂 nk.Roho inamuuma lakini hawezi kuniambia nimsaidie amepigika mbaya.

Nimetoa huo ushuhuda mrefu kuwatia moyo wale wote wanaopitia hali ya kukataliwa na wazazi hasa baba zao, wapambane kana kwamba mzazi alishafariki.Hiyo hasira ya kukataliwa igeuze kichocheo cha kuchapa kazi kwa bidii na ubunifu ili siku moja uwaoneshe kwamba walibet vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…