Yanayoendelea katika uwanja wa uhuru katika kuaga mwili wa Rais Magufuli

Yanayoendelea katika uwanja wa uhuru katika kuaga mwili wa Rais Magufuli

Utakuwa umebarikiwa Madam. Mana Sisi wakina baba hata kama tuna ukomando mbele yenu hatuwezi kitu. Pale kila mtu alitaka aonekane a Gentleman. Mkate mbele ya chai.
Hivoooo??[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Afadhali huyo Lisu ni muwazi sana na ndiye aliyetujuza kuwa Rais wetu anaumwa.

Mbona Ikulu haikusema mapema ili tumuombee. Kuaga gani huku kwa wiki nzima, mbona Nyerere na Mkapa haikuwa hivi?
Mkuu kumbuka vizuri kwa Nyerere
 
E

Kwa lipi mkuu Mimi na siasa mbalimbali...ndiyo tupo na utawala mwingine ila kwa sasa tunaongelea kilichopo.
.note that. Mzee amepewa heshima sana sana kuliko mlivyotegemea.
Ukisha kufa utapewa heshima maana ndio utamaduni wetu, then watu watasema tuanze upya yakale tuyaache.
 
Afadhali huyo Lisu ni muwazi sana na ndiye aliyetujuza kuwa Rais wetu anaumwa.

Mbona Ikulu haikusema mapema ili tumuombee. Kuaga gani huku kwa wiki nzima, mbona Nyerere na Mkapa haikuwa hivi?
habari alizipata wapi, hizo habari alizozipata alizipata kwa njia gani, kama ikulu hawatoi habari hovyo hovyo kwanini yeye baada ya kuzipata hakunyamaza na kuwasubiri ikulu watangaze wenyewe.
Kama kweli Lissu ni mtu mwema awaeleze watanzania mtu aliyempatia hizo taarifa za mzee kuumwa.
 
Tundu Antipasi Lissu amehoji kutembezwa kwa mwili wa Hayati Magufuli kuagwa kwa heshima wakati ati ugonjwa wake ulifichwa (ona kiambatanisho)!

View attachment 1730949

Je, yuko sahihi au Hayati Magufuli anastahili heshima kubwa zaidi kama inavyoelezwa kwenye Video clip - kiambatanisho?
View attachment 1730954
Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
 
Hayo siyo maisha, ni kifo. Nimesema mwenzio hakutulia nyumbani, amekanyagwa pale Uhuru akafa, wewe unasema maisha!
Okay lets say ni kifo...wewe kifo chake kinakuhusu nn?his life, his death...its his and his maker....acheni ushamba wa kupangia watu maisha.
 
Hv mbona mitandaon hakuna hata picha ya uso wake jamani?
Hii kitu hata mimi nimeuliza bila majibu,
Nikasema ngoja nisubiri leo Dodoma sababu ni ya kitaifa na viongozi ndio wanaaga, nashangaa nako ndio kabisaa ndani ya bendera,
Mkapa kama sikosei zilionekana.
 
Naandika tena JPM akiwa ndani ya jeneza halafu LISSU akiwa pembeni yake likawekwa sanduku la kupigia kura kuchagua nafasi yoyote ya kisiasa naamini hayati ataibuka kidedea kwenye uchaguzi huo.
Labda kwa zile kura zilizozoeleka za kwenye mabegi.
 
Hii kitu hata mimi nimeuliza bila majibu,
Nikasema ngoja nisubiri leo Dodoma sababu ni ya kitaifa na viongozi ndio wanaaga, nashangaa nako ndio kabisaa ndani ya bendera,
Mkapa kama sikosei zilionekana.
Dah..mie mkapa sikujishughylisha kbs...yaan walaaaa...kisa kutuita malofa?
 
Back
Top Bottom