Kwema Wakuu!
Funga ni yako na dini yako na Mungu ni wako. Funga yako sio funga ya taifa au ya dunia. Ni yako wewe binafsi na Watu wanaoamini katika kile unachokiamini. Huyo Mungu unayemuamini usidhani kila mtu anamuamini kama wewe.
Waislamu ni moja ya Watu wasio na uvumilivu katika kuishi na jamii zingine hasa wakiwa wengi. Ni wabinafsi Sana. Wanapenda attention na kujiona wanahaki kuliko wengine. Jambo ambalo ni tafsiri halisi ya ubinafsi.
Waislamu huwa waungwana pale wanapokuwa wachache. Ukiona muislamu ni muungwana mara nyingi jua ni dhaifu, yaani wapo wachache.
Wakari nipo Advance, Waislam hawakuwa wengi walikuwa kama robo tuu ya Advance wote. Shule haikuwa ya dini lakini wao wanaleta mambo ya Dini. Wao kila kitu wanaona kama wanaonewa.
Ishara nyingine ya kuwa uislamu ni ubinafsi ni pale ambapo hawataki Quran yao ikosolewe. Wao wanadhani wanavyoamini Quran iko PERFECT basi kila mtu anaamini hivyo. Kitendo cha kutotaka kukosolewa ni ishara kuu ya ubinafsi. Hata Mungu muumbaji mwenyewe kama hataki kukosolewa naye ataingia katika kundi la wabinafsi.
Ni kama mwanaume aliyeoa ambaye hali nyama basi atataka nyumba yake wasile nyama. Huo si wendawazimu na ubinafsi uliopitiliza.
Kwa nini Watu wasile hadharani?
Huo mwezi wa Ramadhani ni mtukufu kwa Waislamu na sio kwa Watu wote. Yaani watu wasile kisa kuna Watu fulani wapo kwenye mfungo? Ni vioja na Viroja.
Huwezi ita dini ya HAKI wakati kuna ubinafsi unaoendelea katika dini hiyo. Haki ni pamoja na kuheshimu imani na mitazamo ya Watu wengine.
Fikiria mwezi wa Ramadhani alafu kwenye nchi ambazo Waislamu ni wachache waambiwe hakuna Watu kufunga, hiyo inakuja akilini? Yaani kisa ninyi msiowaislamu ambao ni wengi hamfungi basi mnataka waliowaislam wasifunge kama ninyi. Huo ni wendawazimu.
Dini ni yenu na familia zenu. Sio dini na imani ya Watu wote.
Ati sio uungwana mtu kula mbele ya mtu aliyefunga. Hizo akili niza wapi? Sidhani hata Quran imeandika vitu vya hovyo namna hiyo.
Elimu ya Haki na kujitambua ni muhimu. Kama mtu anaweza kumpiga mtu kisa anakula siku ya mfungo wa ramadhan atashindwa vipi kumuua kisa Dini?
Hao vijana waliofanya huo uhalifu washughulikiwe mapema, waache kuchafua amani ya nchi na kuleta malumbano na vita vya kidini. Pia wasiwachafue Waislamu wema ambao kila siku wanahitaji kuonyesha uislamu ni haki na Amani.
Ijumaa Kareem.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.