Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

4000×30=120000
 
Mkuu unawatetea kuumiza na kuwauwa nduguzetu sasa 400 kwa saa hii hela watanunuwa nini?? Na mbona Zanziber tu hapo hakuna hayambambo.. hivi huoni kama watu wetu wanaangamia, kazi ngumu bila kura vizuri au kulala pazuri?? Serikali inawajib wa kuangalia watu wake,hebu njoo Mkuranga viwandani ujionee utumwa uliokithiri,jifanye mfanyakazi kama Huna kitambi uone uonevu. Ni watu wetu hawa. Hiyo energy drink ipande bei kwa kuwalipa 20,000 kwasiku?? Ingekuwa hivi viwanda vinatoka Europe, wananch wa huko ndio wangekuwa mstari wa mbele kuliongelea hili. 400 au 350 kwa saa ??? No no noo kunaulazima wa watuwetu kujitambua na kutupia mabom ya petrol kwenye hivi viwanda sasa.
 
Wanaowaajiri watu hao

Kwenye kampuni yangu

1. Housemaid Mshahara wa chini ni Tsh 100,000/= kwa mwezi, wakulala hapohapo na mwenye elimu ya kawaida yaani kidato cha nne kurudi chini.

2. Housemaid mwenye taaluma mshahara kila cha chini Tsh 200,000/= Form six diploma na kuendelea.

3. Live-out Housemaid Mshahara Tsh 200,000/= huyo ni wakawaida.
Mwenye taaluma kuanzia Tsh 300,000/=

4. Wafanya Usafi (Housekeeping) kwenyw maofisi, Malls n.k Mshahara kima cha chini 250,000/=

5. Walinzi, Kima cha chini ni Tsh 250,000/= inategemea na mahali anapolinda, CV yake na majukumu.

6. Babysitter ( Yaya) wakukaa ni Tsh 160,000/= watoto wasiozidi wawili.
Babysitter wa kingereza chini kabisa 250,000/=

Mishahara hiyo ni zaidi ya mara mbili ya mishahara ya rate iliyowekwa na serikali.
Karibu
 
Bado pesa ndogo sana hio unayowalipa
 
Rate za serikali kima cha chini ni 250,000.00, hiyo zaidi ya mara mbili unayosema ni ipi?
 
Rate za serikali kima cha chini ni 250,000.00, hiyo zaidi ya mara mbili unayosema ni ipi?

Mshahara wa Maid wa kukaa ni 70,000/= kwa Mujibu wa serikali.
Maid wa kwenda na kurudi ni Tsh 120,000/=
Maid anayefanya kazi kwa wafanya biashara wakubwa ni 160,000/=
Maid anayefanya kazi kwa mabalozi, viongozi wa serikali ni Tsh 250,000/=

Viwandani rate yake ukisikia unaweza ukakimbia
 
Watakuja kushtuka ni watt wenu nyie mshafungwa mi nashangaa elf tano kwa siku watu wanaishije na anafamilia dahh hii sio fear kabisa, ilitakiwa min iwe angalau 10k per day, kuna watu waafaya kazi ktk viwanda hatarishi kwa afya yani akitoka apo ni tb au kansa dah inatia huruma sana
 
Kuna kiwanda cha sulphur ABC Temeke Tazara. Wanakufa na sumu ujira 10000 na kupata kazi mpaka utoe rushwa au chupi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…