Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Uko sahihi. Haya mambo bila kuwa na hizo groups ni bure. Serikali ndiyo ilaumiwe kwa sababu imewafanya watanzania wasijue ni nini maana ya vyama vya wafanyakazi.
Casual labour msisahau ni non formalized ector.. kuwa na vyama ni ngum. Hasa day worker mtawapatia wapi na kwa profeshino gan? Leo saidia fundi kesho unankuta mbeba magunia, kesho kutwa konda.
 
Sure mzee.
Ulijuaje mind zao ziko locked?

Na je wanafanya kaz kwa muda mfupi wakafanye issue zingine au wao ni kukaa hapo forever.

Wale wapo pale daima na hata ukapiga kazi huwezi kuikamata 10K so huwezi kuweka akiba ili upate mtaji.

Watu wamefungwa akili I speak from Experience

Doesn't make sense MTU Ana nguvu umbebeshe viloba from morning to evening na umpe 4000 hadi 3500 you need to know something wrong on their minds
 
Hao makanjibai wataendelea kutuburuza endapo kama nchi hatutabadilika. Serikali itimize wajibu wake na pia sisi watanzania tutimize wajibu. Kwa mfano unakuta kiongozi mkubwa kama Mbowe anaenda kuchangisha zaidi ya milioni 400 kumnunulia askofu gari la kifahari baada ya ku-boost vijana wajasiriamali ambao wameshaanza kupiga hatua. Kuna vijana wako vizuri kwenye ujasiriamali ukisema uwawezeshe angalau 50m kila mmoja wangeajiri vijana wenzao kibao. Cha kushangaza kiongozi wa chama kinachojiita cha ukombozi anaenda kutumia zaidi ya milioni 400 kumzawadia askofu asiye hata na shida ya hiyo pesa.
Tatizo ni sisi wananchi. Siku hizi hata CCM siwalaumu kwa sababu ni dhahiri wako kwa sababu ya matumbo yao na hawana hasara. Je, sisi wananchi tunafanya nini? Kwa nini hatukinukishi na ikibidi tuvamie Ikulu na kumwondoa huyu mama anayevaa maushungi ya kinafki? Bila sisi wananchi kuwa wakali ni bure. Tunaweza kuwa na chama kimoja tu eg CCM, lakini tukiwa wakali na kukataa upumbavu wa kiongozi aliyeshindwa kazi, na tukamtimua na kuweka mwingine, viongozi wote watawajibika kwa kuogopa.
 
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000, kazi masaa 12 yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku, hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena.
uvivu tu si uache kazi!!

Utumwani huna option ya kuacha.
Huku unaweza acha na kwenda kuuza karanga
 
Hii sio sababu ya kumefanya mtu akatae hiyo kazi. Mkuu hali ya maisha inatofautiana sana. Kuna watu wankimbia masimango na kuishi maisha yoyote bila kujali self investing Wala nguvu anayotumia

Cheap labour mda mwingine wanazalishwa na migongani katika familia hasahasa zile advanced marginalized, zenye sifa ya umaskin wa kutupwa na kukosa wasomi. Hili janga root cause yake ni hiyo.. that's good assumption kama utatumia nadharia flanflani hiv

Maisha yanahitaji MTU kuwa uwezo Wa kufikiri vyema wote hapa tumepitia maisha magumu Sana tunaelewa hata viwandani nimefanya kazi.

Lakini akili ikiwa locked nothing you can do.

Kinachowasumbua vijana ni akili kujifunga.

Unapoishi usikubali kuwa mtumwa wa MTU .

Wahindi na waarabu wanachofanya nikuzifunga Akili za hao vibariua
 
Kuna mambo ya hovyo yanafanyika sana hapa nchini..

Na shida ni kwamba hao watu wakilipwa hizo buku nne bado na kesho mapema tu wapo kwenye foleni ya kuingia mzigoni..sasa hapo utamlaumu nani??

Maisha ya kingese kabisa..sasa elfu nne si ni hela ya kula mchana tu na maji ya kunywa..Naamini elfu nne mtu unaweza kuipata kwa kutoteseka hivi aisee.
 
Kuna familia ukizaliwa mkuu huna jipya-... Ni mateso mpka kufa! Wanaofanya kazi hizo hapo bugurun wengi wanatoka vijijini wamekuja kusaka life. Wengine wa humuhum na Wana digrii wamekimbia masimango yanayoanzia ngazi ya familia...

Endelea kufanya utafiti uone kama ana option nyibgine. Hii iqe quantitative na methodology yako ibebe assumption ya kupima plight condition ya familia wanazotoka na life economic opportunities they can opt
Sure family background inamatter sana pia wengine awana option nyingine.

Ila mkuu vp hao wa degree nazan wanafanya na kupita.
 
Maisha yanahitaji MTU kuwa uwezo Wa kufikiri vyema wote hapa tumepitia maisha magumu Sana tunaelewa hata viwandani nimefanya kazi.

Lakini akili ikiwa locked nothing you can do.

Kinachowasumbua vijana ni akili kujifunga.

Unapoishi usikubali kuwa mtumwa wa MTU .

Wahindi na waarabu wanachofanya nikuzifunga Akili za hao vibariua
Una hoja nzuri lakin huvai context.. unasahau Kuna watu humu jf mitaji wanayo na wanatafuta mawazo ya biashara. Hao vijana waliofubgwa akili na wahindi unahisi wako katika levo gan ya maamuzi?

Life is too complex, wengi wanatusua kimungu mungu tu. Kuna jamaa yangu alisoma na digrii akaajiriwa taasisi flani hiv binafsi kwa mwez 600k. Hakuwez kusev hata laki 6 muda wa mwaka mzima aliofanya Kaz pale. Akaja kuajiriwa ulinzi, miaka miwili katoka na million 10 mpaka muda huu kajiajiri na kajenga. Ni mungu tu
 
Unahisi vibarua wa day worker china na India wanalipwa bei gani?
Kisha linganisha na per Capital yao ndio utaona mambo ni yale yale
Hivi hii tabia ya kuhalalisha jambo baya linalotokea Tanzania kwa kuonyesha kuwa linatokea pia sehemu nyingine mbona imekuwa ndiyo njia ya kuhalalisha kushindwa kwetu? Kwa hiyo kama hizi nchi ambazo ziko overpopulated na hazina raslimali nyingi zikifeli kufanya jambo basi na sisi tuige?
 
Kuna mambo ya hovyo yanafanyika sana hapa nchini..

Na shida ni kwamba hao watu wakilipwa hizo buku nne bado na kesho mapema tu wapo kwenye foleni ya kuingia mzigoni..sasa hapo utamlaumu nani??

Maisha ya kingese kabisa..sasa elfu nne si ni hela ya kula mchana tu na maji ya kunywa..Naamini elfu nne mtu unaweza kuipata kwa kutoteseka hivi aisee.
Uwez mlaumu mtu maana wanakuja wenyewe ila pia kuna sheria serikal inazembea kuifata.

kama mdau alisema kwa sasa kibarua per day katika act za sasa 5770/= ila viwanda vinalipa below iyo na wapo kimya.

Ila jaman kama unafanya kazi sehemu nzr mshukuru Mungu sana japo mshahara autoshi.
 
Sure family background inamatter sana pia wengine awana option nyingine.

Ila mkuu vp hao wa degree nazan wanafanya na kupita.
It cost time and energy.. wengi wanangalia fursa nyingine. Mm binafsi mkuu niliwahi kufanya mpaka ulinzi. Mshahara ilikuwa less than 200... Ila LINDO lilikuwa sehem flan flan za upigaji. ALHAMDULILAH nilipata mtaji wa kuanza safar mpya ya maisha
 
Una hoja nzuri lakin huvai context.. unasahau Kuna watu humu jf mitaji wanayo na wanatafuta mawazo ya biashara. Hao vijana waliofubgwa akili na wahindi unahisi wako katika levo gan ya maamuzi?

Life is too complex, wengi wanatusua kimungu mungu tu. Kuna jamaa yangu alisoma na digrii akaajiriwa taasisi flani hiv binafsi kwa mwez 600k. Hakuwez kusev hata laki 6 muda wa mwaka mzima aliofanya Kaz pale. Akaja kuajiriwa ulinzi, miaka miwili katoka na million 10 mpaka muda huu kajiajiri na kajenga. Ni mungu tu
Kwenye ulinzi alikuwa analipwa shingap?
 
Na kuna ujinga mwingi kupita maelezo mbaya zaidi wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe
Mf: unakuta mtu anachjiwa 50k ili apate kibarua ila kipengele kinakuja hyo nafasi unaipigania tena km shift inataka watu 60 na mliopigwa 50k mpo zaidi ya mia kunakuwa n kipengele cha kuwahi namba, unakuta mtu sa kumi alfjiri yuko getini mkitimiq 60 tu waliobki wanarudi wakati huo kiongoz anaendlea kuvuta 50 za vjana
 
Watz hawana furaha kabisa!

Hivyo viwanda pengine vingelipa vizuri tu lakini selikali nayo imekodolea macho huko inawakamua kodi kubwa vibaya mno.

Mwisho wa siku na wao wanawabana vibarua
Regulatory capture..
 
Una hoja nzuri lakin huvai context.. unasahau Kuna watu humu jf mitaji wanayo na wanatafuta mawazo ya biashara. Hao vijana waliofubgwa akili na wahindi unahisi wako katika levo gan ya maamuzi?

Life is too complex, wengi wanatusua kimungu mungu tu. Kuna jamaa yangu alisoma na digrii akaajiriwa taasisi flani hiv binafsi kwa mwez 600k. Hakuwez kusev hata laki 6 muda wa mwaka mzima aliofanya Kaz pale. Akaja kuajiriwa ulinzi, miaka miwili katoka na million 10 mpaka muda huu kajiajiri na kajenga. Ni mungu tu

Upo sahihi.

Unaweza kuwa haujasoma na hauna Elimu ,Ila ukiamua kuiseti Akili vizuri lazima utaona mwanga.

Wale vijana viwandani wanachohitaji kwa sasa hivi sio PESA Ila they need someone who can unlock their minds

Kila MTU anahitaji PESA ila pesa hata ukipata if something wrong on ur mind you will end up being broke with an endless hustles

So kabla hatujawalumu wamiliki wa viwanda tunbidi sisi wenyewe tujiulize je sisi hapa duniani tumekuja kuwa wabeba viloba vya unga?.

Mkuu ,nimefanya Sana kazi za nguvu naelewa usipopata MTU wa kuifungua Akili yako utajikuta unapoteza muda na unatoka umeharibika mwili na Akili.

Nchi haina fursa za kutosha Ila hiyo pekee sio sababu ya kwenda kuwa mtuma there's a lot things to do.
 
Tatizo ni sisi wananchi. Siku hizi hata CCM siwalaumu kwa sababu ni dhahiri wako kwa sababu ya matumbo yao na hawana hasara. Je, sisi wananchi tunafanya nini? Kwa nini hatukinukishi na ikibidi tuvamie Ikulu na kumwondoa huyu mama anayevaa maushungi ya kinafki? Bila sisi wananchi kuwa wakali ni bure. Tunaweza kuwa na chama kimoja tu eg CCM, lakini tukiwa wakali na kukataa upumbavu wa kiongozi aliyeshindwa kazi, na tukamtimua na kuweka mwingine, viongozi wote watawajibika kwa kuogopa.
Kuwa na adabu kwa Rais wa nchi. Mabadiliko hayaletwi kwa matusi. Kukinukisha sio suluhisho la matatizo kama mfumo utaendelea kuwa uleule. Kenya wanabadili vyama tawala kila mara ila mambo ni yaleyale... Zambia ndo wakali wa kubadili vyama ila wananchi wana shida afadhali ya sisi... unaitoa CCM unaiweka CHADEMA ambayo viongozi wake wanachangishana mamilioni kumzawadia Askofu mstaafu V8 huku chama kikiwa dhoofu kiuchumi??!!! Kwa sasa tutaendelea na CCM hadi pale mbadala wake utakapokuwepo.
 
Back
Top Bottom