Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Kuna ajali za kutisha huko kwenye viwanda ,we acha tu , hata safety gears Tu ,Hamna
Kuna ajali nimewahi shuhudia mwanamke anagongwa na kuvunjwa mguu na yale meno ya fork lift za kubebea mizigo kutoka kwenye production line kwenda warehouse ,na hakupewa hata fidia au matibabu ya maana , ni ulemavu wa kudumu

Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
Inasikitisha sana Kimbukiko
 
Tumia akili. Hesabu ya darasa la kwanza.

Kama mwezi huu ukilipwa tarehe 10, na mwezi ujao ukalipwa tarehe 10. Hakuna mbaya hapo, siku 30 zimetimia.

Yaani ni hivi, mshahara wa February ukipata March 10, na mshahara wa March ukaupata April 10... Na salary ya April ukapewa May 10. Kihesabu ni siku 30 zimetimia.

Usikariri eti lazima mshahara upewe mwisho wa mwezi tarehe 30.
We jamaa fala kweli. Unadhan hesabu hiyo mm siijui?. Mshahara unasoma tarehe 30 net! Ukianza kazi tarehe 10 unakuja kupokea mshahara tarehe 10 wa siku 20 tu.

Kakojoe ukalale
 
Duh rushwa ni tatizo.Sufuria zina dhuru nn?
Inasikitisha sana

Mkuu,ndiyo maana magonjwa kama cancer yanaspidi kubwa katika jamii yetu,kuna kiwanda cha sufuria hapo Matumbi staki kukitaja jina,hali ni mbaya sana, OSHA wakienda wanaishia kwenye management tu wanachukua bahasha bila hata kufanya ukaguzi
 
Hali sio nzuri... Sio viwandani tu... Waoneni Hawa sales officers wanaozunguka barabaran muwaulize wanachopata.. kiufupi wengi tunafanya kazi ili kukamilisha kilichosemwa na kilichopo kwamba ufanye kazi ili ule. Na kula kwenyewe usipoangalia dah hutoboi kukuta mshahara mwingine
 
Hii nchi ngumu sana sema kweli viongozi awako seriously na maisha ya watu wanao waongoza kiujumla. Kwa maana aiwezekana maisha ya wanachi wanayajua vizuri kabsa iwe umesoma au ujasoma. Nachotaka kusema ni kuweka utaratibu juu ya malipo ya wafanya kazi viwandani ni kazi ngumu sana kama ulishawahi kufanya hiyo kazi alafu isitoshe unafanya kazi Masaa kumi na mbili, sijui mnaelewa kazi ya Masaa kumi na mbili non stop. Alafu Mtu analipwa 7000.


Nizungmzie pia kwa watu waliosomeshwa kwa mkopo na serikali alafu Mtu anamaliza mpaka chuo kikuu anabahatika kupata sehemu ya kazi analipwa hela hiyo hiyo kama kibarua na serikali inaona hilo na inakaaa kimya. Alafu mwisho wa siku Mtu huyo huyo anaanza kukatwa kwenye huo huo mshahara wa laki tatu kwa mwezi. Mnategemea kwa mshahara huo Mtu kama huyo atamaliza kulipa si chini ya miaka 20. Mnakaa kwenye vyombo vya habari mnasema mmeongoza ajira kwa kumlipa Mtu 4000 kwa siku na makato juu.

Cha muhimu kama serikali inabidi itoe maelekezo yanayo eleweka juu ya malipo ya wafanya kazi viwandani. Kwa watu wote.
 
Hawa watu wa chama cha wafanyakazi na wakaguzi kutoka serikalini walikuwa wakifika kiwandani nilikokuwa nafanya kazi, lakini hawakuwa wanaonana na wafanyakazi badala yake walikuwa wanaishia ofisi ya HR wanapiga stori na muhindi kisha wanasepa huku sisi tukiendelea kupigika. Mbaya zaidi kile kiwanda kilianza na tabia ya kunyonya malipo ya nssf ya wafanyakazi, na ikiwa mtu akienda kudai kule nssf basi anabambikiwa kesi na hakuna anachopata.
 
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000, kazi masaa 12 yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku, hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena.
Kima cha chini ni 346000TSh, hiyo 5000 kwa siku ni nyingi Sana,
Wabaya wako ni ccm, mbunge analipwa milioni 11 kwa mwezi, posho kwa siku 350K, baada ya miaka 5,anakula mafao yake, wakatunga kikokotoo, "kizuuuri" Kwa ajili ya "kutunza" Pesa za, wastaafu, ili wastaafu vzr,cha ajabu wao wabunge, wamejitoa kwenye uzuri wa kikokotoo,! Wao sio, watumishi wa umma! Mpunga wao wanauvuta mapeeemaaa! Kwenye hili la maokoto, si chadema, act wala ccm, anayeweza kusema kitu!
 
Tajiri Kuuona Ufalme Wa Mbingu Ni Sawa Na Ngamia Kupita Kwenye Tundu La Sindano.
Tajiri ndio anautumia mfanano wake na Mungu, anatoa ajira, Kodi za kusaidia serikali kulipa mishahara, maskini ye ye ni kunya na kuvuta pumzi tu!
 
Tutafute namna ya kuwasaidia hawa watu wetu,sio kila mtu anaweza kuwa na hilo shamba,tuishinikize serikali isikubali watu wake wanyannyaswe kiasi hiki,hawa ni nduguzetu na hii ni nchiyao,mbona Zanziber hakuna upuuzi huu??? Day works sio chini ya 20,000.
Acha kupotosha watu kwa Zanzibar gani labour analipwa zaidi ya 20,000?
Zanzibar kuna unyanyasaji mkubwa sana tena hata zaid ya bongo na kuna ukabila mkubwa sana kati ya mzanbari na mbongo huku tunaitwa Wanyamwezi
 
Mkuu hio upo dunia nzima, unaposikia Wazungu wanakimbilia china kwa ajiili ya cheap labor ndio kama hao, saizi wanatoka china wanaenda India kwa ajiili ya watu kana hao,
Unskilled labor dunia nzima mishahara yao ni mbuzi tu, mana wanakuwa hawana mikataba, day worker tu,

Kwa kusema hivyo tuhimizane ndugu zangu kusoma sanaa
Kusoma sio suluhishobkwa maisha ya sasa maana wasomi wapo na hawana hata pa kushika kikubwa ni kukituma na ubunifu katika kazi
 
Inabidi uchunguzi ufanyike vyakutosha na serikali ichukue hatua za kisheria, japokuwa Sheria wakati mwingine inaruuhusu pale ambapo mmiliki wa kiwanda ataomba asijumuishe kwenye employment standards na hapa ndipo tatizo lilipo kifungu Cha Sheria 100, "The Employment and Labour Relations Act [CAP. 366 R.E. 2019]" kifungu Cha Sheria hiyo kinasema kwamba "100.-(1) The Minister may exempt any employer or class of employers from any employment standard contained in sections 19, 20, 23 to 25, 27,31 to 34, 41, 42 and 43." sasa tatizo kubwa lipo hapa
 
Back
Top Bottom