Yanayojiri Bunge Maalum la Katiba leo Tarehe 7.3.2014.

Naam barabara kabisa ndugu wakatwa kodi wenzangu sasa bunge liko hewani kupitia Star TV, tuwemo. Wale maripota wetu endeleeni kutuhabarisha zaidi.

cc Chabruma
Pamoja sana Mkuu. Hata JF ilikuwa live tangu kitambo
 
Kodi zetu?! Well japo silipi kodi lakini hii tabia yao ya kutokwenda na muda inaonyesha hawako makini
 
Acha kuropoka mkuu. Kuna teknolojia rahisi kujua hizo picha zimepigwq muda gani. Tofauti zetu kisiasa zisiwachanganye wqnaofuatilia bunge hili. Hili ni bunge maalum na kila mmoja ana wajibu wa kumhabarisha mwenzake pale anapopata fursa. Wadau, epukeni upotoshaji unqofanywa na huyu jamaa. Ana malengo yake kisiasa. Sisi tunachapa kazi, wao ni majungu tu
 
 
Last edited by a moderator:
Sana tu mkuu. Ila kwa vile kazi iliyobqki ni ndogo, ni wazi kuwa kanuni zote zitapitishwa leo na kesho itakuwa ni uchaguzi wa Mwenyekiti tu

Kazi itakua ndogo endapo wajumbe watakua na nidhamu pia kuepuka jaziba. Kuna wajumbe wanakua na utovu wa nidhamu kupita kiasi kama Sendeka na Rage yaani wana utoto mwingi sana.
 
Wadqu, Mwenyekiti amemaliza kuzungumza na viongozi wa makundi ya bunge hili na sasa anaelekea kwenye kiti chake kukaa tayari semina kuanza. Sasa anaanza kuongea na anwakaribisha viongozi wa dini kusoma dua
 
 
Kati ya wewe na Chabruma nani ambaye anatupa habari za ukweli? Wewe unasema mnasubiri mwenyekiti aingie bungeni, wakati mwenzi anasema mwenyekiti aliingia saa 3 na dakika 50!!! Naanza kuwa na mashaka na uwepo wenu bungeni.
Mwenyekiti aliingia bungeni na kwenda kwenye chumba cha mashauliano siyo ukumbi wa bunge sasa anaketi kwenye kiti chake tayari kuanza kikao chetu twende pamoja sasa.
 
Sheikh Norman Thabit Jongo anasoma dua ya kuliombea Bunge
 
Mwenyekiti aliingia bungeni na kwenda kwenye chumba cha mashauliano siyo ukumbi wa bunge sasa anaketi kwenye kiti chake tayari kuanza kikao chetu twende pamoja sasa.
Mkuu, naona kuna watu hawaelewi tofauti yamukumbi wa Bunge na kuingia Bungeni
 
Sheikh Jongo amemaliza kusoma dua na Askofu Mstahafu mtetemela anasoma dua
 
Dua ya upande wa ukristo nayo inafuata make iliyoanza ilikuwa dua ya kiislamu twende pamoja.
 

Sio vizuri ku take advantage ya hamu ya watu kujua kinachojiri kwenye Bunge lao kwa kuwadanganya. Huo uadilifu wenu wa kusema ukweli umeanza lini? Wewe na huyo Simiyu Yetu kaeni kwenye Tv mkitaka kuripoti au kuacha shauri yenu, bado watu watapata habari za Bunge from reliable sources.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wakuu siku ya leo inaupekee wa aina yake ndiyo maana hata dua zinasomwa make kupita kwa kanuni hizi ndiyo mwanzo wa katiba njema.
 
Mgonjwa wewe katibiwe kwanza usiseme usiyojua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…