Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Mubashara imeshindikana bwashee?!
 
Hii kitu itazidi kuwachanganya wakubwa pale magogoni
 
Unataka kutuambia Lowassa angeenda Chauma angepata kura milioni 6?
Uimara alioukuta Chadema ndio uliompa kura hizo na huo ndio ukweli.
Hivi unategemea Messi ukimsajili Singida united atakuwa mfungaji bora wa ligi?
All in all, nadhani Chadema kwa sasa ni imara sana kuliko awali. Na kama suala la tumehuru litasimamiwa kwa makini hadi lifanikiwe basi Ikulu yaweza kuondoka CCM au kama haiondoki lakini bunge haliwezi kuwa na 2/3 ya chama kimoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pasco kwa mazingira tuliyo Nayo ikitokea chadema wakaanzisha media watanyimwa usajiri na TCCRA, hata kama sheria inaruhusu, ikishindikana unaweza kupelekwa muswada kwa hati ya dharula kuzuia vyama vya siasa kumiliki Media

Lengo in kuhakikisha chadema haipati coverage na inakufa

Mkuu huwa unatoa ushauri kwa cdm kwa kejeli, nadhani uko kwenye mpago maalum wa kuidunisha chadema,
 
Hana tofauti na mwanakijiji, wako kikazi zaidi, uzuri wameshajurikana kitambo wala haisumbui watu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huwa unatoa ushauri kwa cdm kwa kejeli, nadhani uko kwenye mpago maalum wa kuidunisha chadema,
Pascal Mayalla namheshimu sana kwani kwa wengine kama sisi kupitia kipindi chake cha "Malumbano ya Hoja" ndio tulipata nafasi ya kuonekana kwenye TV kwa mara ya kwanza kutokea pale Simba Grill, Kilimanjaro Hotel.

Lakini Mayalla amekuwa kama maji ya vugu vugu siku za hivi karibuni ni kama anauma na kupuliza. Na yeye kama wengine huwa wanalaumu bila ya kuonesha njia ya utatuzi wa tatizo.

Kwa CHADEMA kumiliki vyombo vya habari ni wazo zuri sana kinadharia lakini siyo rahisi kiuhalisia. Leo Mayalla anataka kutuambia Tanzania hakuna Uhuru wa kujieleza ndiyo maana anataka CHADEMA wawe na "Media" zake chenyewe!

Mayalla anaona ni sawa kwa vyombo vya habari vya Tanzania kuonesha mambo ya CCM "live" wakati mambo ya CHADEMA wanayapa kisogo. Badala ya kuona aibu wao kama waandishi wa habari kuonesha woga wa dhahiri kwa CCM anaitoa kafara CHADEMA dhidi ya udhaifu wao.

Waandhishi wa habari wa Tanzania hujazana kwenye mambo ya CHADEMA lakini kesho yake ama siku hiyo hiyo vyombo vyao vya habari wanavyofanyia kazi haviwezi kutoa habari hizo.

Nimkumbushe tu ndugu yangu Pasco kwamba tatizo la CHADEMA si kuwa na vyombo vyake vya habari, bali tatizo la CHADEMA ni kuwa chama cha siasa kwenye nchi yenye "Media" zilizojaa watu goigoi na waoga!!

Hilo la kutumia "Social Media" CHADEMA wanajitahidi sana, na ndiyo maana utasikia CCM wanasema kazi ya wanachadema ni kushinda kwenye mitandao ya kijamii.
 
Yaani siku hizi huyu jamaa amekuwa na chuki ya ajabu na Chadema au ndiyo masharti aliyopewa kule mjengoni, siyo kwa kujitoa ufahamu huku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani siku hizi huyu jamaa amekuwa na chuki ya ajabu na Chadema au ndiyo masharti aliyopewa kule mjengoni, siyo kwa kujitoa ufahamu huku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana siyo masharti. Pascal Mayalla anajaribu kuwa "Satirist" lakini hapo hapo mapenzi ya "Home Boy" humuingia mara tena woga wa kuchukiwa na walioko madarakani humvamia.

Pasco ana "Multi Personalities syndrome" inayotokana na mambo mengi sana. Wakati mwingine tumsamehe baada ya kumuonesha kwamba alifanyalo lina athari kwake na vizazi vyake vijavyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…