Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Uchambuzi wako ni dhaifu sana.Leo Novemba, 5 mwaka 2024 wananchi wa Marekani wanapiga kura kuchagua rais wa nchi hiyo atakayeongoza kwa kipindi cha miaka minne
Mchuano mkali ni kati ya makamu wa rais wa sasa BI. Kamala Harris (60) wa chama cha Democratic na Bw. Donald Trump wa cha Republican
Trump ana nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huu kutokana na imani kubwa kwa wananchi wa nchi hiyo hasa wadhungu weupe na matajiri kuwa atainua uchumi wa nchi hiyo
Atamaliza vita kati ya Urusi na Ukraine pamoja na mipigano yanayoendelea Mashariki ya kati Israel na Palestine/Hisborrha
Pia wananchi wa USA wanaamini Trump akiwa madarakani atadhibiti wahamiaji haramu kuingia kiholela nchini humo sera ambayo amekuwa akiihubiri kwenye kampeni zake
Soma Pia: LIVE Yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu Marekani 2024: Nani kuibuka kidedea?
Aidha wanaamini mgombea huyo ataimarisha uhusiano wa kibiashara na China na Urusi na kwamba atapunguza migogoro ya kivita kati ya nchi hiyo na China na Rusia hivyo kuimarisha uchumi
Wamarekani wanaamini pia Trump atadhibiti ugaidi nchini mwao na kuwafurusha wahamiaji haramu na kuthibiti utoaji misaada kwa nchi masikini za dunia ya tatu
Karata yangu miye pia napa mwamba Donald Trump kushinda na kuibuka kidedea kwenye uchaguzi wa leo
Comasava
Umejenga hoja lakini umeshindwa kuitetea vyema, na baadhi ya sababu ulizozitaja kumpa kura Trump ni miongoni mwa sababu pia za kutumika kumnyima kura Trump.
Huwezi kusema Trump ana sera nzito dhidi ya wahamiaji, na wakati huo huo kuna wahamiaji wengi wanapiga kura za kuamua matokeo.
Huwezi kusema Trump akiingia madarakani atamaliza vita ya Ukraine na vita ya Gaza, lakini hapo hapo ushindwe kusema kivipi amepanga kufanikisha hilo.