Uchaguzi 2020 Yanayojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA Mh Tundu Lissu Mkoani Songwe na Rukwa

Rukwa , Sumbawanga
 

Attachments

  • Subpost 2 - Mapokezi ya mgombea wetu wa urais wa JMT Sumbawanga. _v_️ Mmeeleweka ( 352 X 640 ).mp4
    1.7 MB
17 September 2020
Sumbawanga, Rukwa
Tanzania

Tundu Lissu - Kuna haja ya kushinda kwa namna ya kipekee

Sumbawanga hii yote lazima ijitokeze kwa kimbunga hiki maana umma utakuwa amesema. Kimbunga hiki kilinde kura na vyombo vyote vitakuwa upande wetu kutokana na kimbunga hiki.

Tundu Lissu anasisitiza kupitia CHADEMA agano lao 2020 na waTanzania wote bila kujali vyama ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu na ndiyo agenda yetu Kuu.

Waandishi wa habari, mapolisi, waalimu, manesi n.k hawawezi kudai Haki yao kwa kuwa hawapo Huru kuweza kudai haki yao. Hawapo huru kupitia vyama vya wafanyakazi kujiunga na kupeleka malalamiko ya stahiki zao za kifanyakazi kama nyongeza n.k zilizoainishwa katika ajira zao na mikataba yao kisheria.

Mikoa ya mpakani kama Rukwa, Kagera, Songwe , Mbeya, Kigoma wakulima hawaruhusiwi kuuza mazao yao nchi jirani lakini viwanda kama Mohammed Enteprise, Azam Group n.k vya Dar es Salaam wanaruhusiwa kuuza bidhaa zao Malawi , Zambia, DR Congo, Rwanda na Uganda kwa uhuru lakini wakulima wa mikoa ya mpakani hawana uhuru huo.

Sasa CHADEMA inataka waTanzania wote wawe wakulima, wafugaji n.k nao wawe huru kuuza popote kama makampuni ya waTanzania wengine wa Dar es Salaam wenye viwanda ili wafaidike na Haki zao wajiletee Maendeleo ya Watu kwa kujitajirisha kwa kuuza mazao yao kwenye bei kubwa ndani na nje ya Tanzania.

c.c Erythrocyte
c.c koyola
 
Asante sana mkuu
 
17 September 2020
Sumbawanga, Tanzania

Tundu Lissu azungumzia umuhimu wa Afya na Huduma za jamii kwa Maendeleo ya Watu


Afya, elimu , maarifa na ufundi stadi ili kuwapa wananchi nafasi wajipatie uwezo wa kufikia Maendeleo ya Watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…