Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 1,628
- 2,720
Wote walishirikiana kumpa kipondo kikali mno ndugu yao.Hitler alipigwa na USSR pekee. Britain na France walikuwa wamechoka ile mbaya.
USA alikuwa akipambana na Japan.
Sorry
US licha ya kushughulishwa na Pacific Theater, lakini bado alikuwa committed na kuanza kumshinda kwanza mnazi kabla ya mjapan.
Muingereza nae alishiriki vizuri tu kumpa kipondo ndugu yake. Hali yake ilikuwa mbaya ndio, lakini hasa hasa 1940 mpaka 1942 au 43 baada ya hapo meza ilimgeukia mnazi. Kiufupi mnazi mambo alianza kuharibu baada ya kufungua front nyengine mashariki (uvamizi dhidi ya USSR/Operation Barbarossa) wakati bado alikuwa anamshughulikia muingereza.
USSR alibanwa nae na wanazi mwanzoni.
Ufaransa yeye alipokea kipondo na kibano na kukaliwa kimabavu mpaka majeshi ya washirika yalipokwenda kuikomboa mwaka 1944. Na USSR akawasukuma wanazi kutoka eneo lake.
Baada ya hapo ikawa ni zamu ya wanazi kuchakazwa.
Na walimchakaza.