LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Yani hapo wakuteseka sio mda ni raia wa palestina kwa ujinga wa Hamas jamaa wataharibu Kila kitu. Hapo akina George soros wanaona na kufadhili hii vita
 
Hii ilikuwa ya mwisho,Hamas hawatakuja tena kufanya ugaidi maana hawatakuwepo kabisa kuazia leo
Ww jamaa buana hivi unadhani vita ni rahisi kiasi hicho?
Ebu uliza watu kilicho ikuta Israel mwaka 2014 baada ya kuivamia gaza kwa lengo la kuiangamiza Hamas.
 
Yani hapo wakuteseka sio mda ni raia wa palestina kwa ujinga wa Hamas jamaa wataharibu Kila kitu. Hapo akina George soros wanaona na kufadhili hii vita
Tayar naona raia wa Palestine hasa kina mama na watoto wanakimbia makazi Yao maana wanajua kinachofuata ni nini.
 
Hawa Hamas mbona wajinga sana, hawasomi Biblia agano la kale wakaona Israel sio watu wa kutingishiwa kiberiti. Sasa tuweke macho tuone nani atakubali hatari ya kuwasaidia.
Hamna! Nature ya muisrael ni mwoga!

Muisrael vita haiwezi! Ukitaka uone watakavyosumbuka Hamas wapigane mijini ndani ya miji yao kama Ukraine na Russia! Watakimbia!

Ila sijui nao Hamas wamejiamini kwa lipi kufanya hivi? Nguvu yao naiona ni ndogo sana kwa Israel.
 
Sasa si umesema Israel ni muoga na wao wameliona hilo?
Tusubiri Israel achakazwe
 
Hamna! Nature ya muisrael ni mwoga!

Muisrael vita haiwezi! Ukitaka uone watakavyosumbuka Hamas wapigane mijini ndani ya miji yao kama Ukraine na Russia! Watakimbia!

Ila sijui nao Hamas wamejiamini kwa lipi kufanya hivi? Nguvu yao naiona ni ndogo sana kwa Israel.
Vita yeyote ni ngumu awe mchina mmarekani mrussi vita ya ground tofauti na kwenye Tv, Hamas watasababisha raia wapate tabu zaidi
 
Ukanda wa Gaza: Makumi ya roketi yarushwa kuelekea Israeli

Makumi ya roketi yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyoheshimishwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kuwa limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Ufyatulianaji wa risasi, kuanzia maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza, ulianza kabla ya 6:30 asubuhi saa za Mashariki ya Kati na kuendelea karibu dakika arobaini na tano baadaye.

Nchini Israeli, ving'ora vya onyo vimesikika katika miji kadhaa karibu na Palestina, pia huko Jerusalemu lakini pia ndani zaidi katika eneo hilo, kaskazini na mashariki, kulingana na jeshi.

Roketi imeanguka kwenye mji wa Yavne, kusini mwa Tel Aviv, ambapo mtu mmoja amejeruhiwa kidogo, kulingana na Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel. Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini ameuawa "kwa pigo la moja kwa moja", na watu wengine 15 wamejeruhiwa kusini mwa Israeli, linasema shirika la Magen David Adom.

Jeshi la Israel limeripoti kupenya kwa "idadi isiyojulikana ya magaidi" kwenye ardhi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. "Wakazi katika maeneo jirani ya Ukanda wa Gaza wametakiwa kusalia nyumbani," jeshi limeongeza.

Mwezi Mei, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vita vya siku tano kati ya jeshi la Israel, Islamic Jihad na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, na kugharimu maisha ya Wapalestina 34 na mwanamke mmoja wa Israel.

Zaidi ya roketi elfu moja zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, nyingi zikiwa zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel. Israel kwa upande wake ilikuwa imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo dogo.

Hamas, ambayo ilichukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007, ilikuwa imejitenga na mzozo huu.

Imechapishwa: 07/10/2023 - 08:13 Na:RFI
View attachment 2774147
Wamepewa chai 😂😂😆

Hamas bwana wameona Dunia imepua wameamua kukiwasha tena huko na Sasa tutarajie mauaji ya zaidi ya Wapalestina Buku Hadi buku 2 wakati Kafiri Akilipiza Kisasi 🤪🤪
 
Netanyahu: 'We are at war and we will win'​

Israeli Prime Minister Netanyahu has just released a statement, saying that "we are at war and we will win".

In a statement released on his social media channels, he said Hamas would "pay a price the type of which it has never known".

The Israeli Defence Forces (IDF) are fighting Hamas in a number of locations, with an unknown number of casualties.

===========================

Mwishowe Israel itajibu kwa nguvu kubwa na atadhibiti maeneo mengi zaidi ya Wapalestina, hata Gaza huenda ikarudi kwenye udhibiti wa Israel........ardhi kubwa zaid ya Wapalestina itakaliwa na Israel kimabavu.

Raia wa kawaida wa Wapalestina wataishia kuwa wahanga wa huu uhuni uliofanywa na Hamas.

Israel-Gaza latest: Hamas fighters on the ground after '5,000 rockets' fired; 'We are at war', says Netanyahu
Kuidhibiti gaza hawa taweza maana walisha jaribu mwaka 2014 waka shindwa vibaya sana.
Kuhusu wahanga raia wa palestina wamekuwa wahanga bila kujali kwa makumi ya miaka bila kujali wanapigana au hawapigani.
 
Ww jamaa buana hivi unadhani vita ni rahisi kiasi hicho?
Ebu uliza watu kilicho ikuta Israel mwaka 2014 baada ya kuivamia gaza kwa lengo la kuiangamiza Hamas.
Tusishangaane kila mtu aandike maoni yake
 
Siku mbili zilizopita kilitokea na shambulio la Orthodox Jews kutemea mate wakristo katika lango la kabisa huko East Jerusalem.
Cha kujiuliza wakristo huwa mnajinasibisha na Hawa wayahudi mkisema ndugu zenu,je ndugu yako wa Imani anaweza temea mate lango la kuingia nyumba yako ya Ibada??!!
Hapo hapo ikumbukwe muandishi wa habari wa aljazeera Sherin Abu Akleh ni mkatoliki na alipigwa risasi mwaka jana kama sikosei na IDF.

View: https://youtu.be/qhWoKZl_CEA?si=gog-TETIuNIFV25_

Niliwahi kusisitiza humu kuwa waisraeli wao wanajijali wenyewe na hawautambui ukristo wala Yesu Kristo na jambo linalotokea katika nyanda yao sio jambo la kidini kati ya uislam na ukristo bali ni udhulumati kukandamiza wapalestina waislamu na wakristo kiujumla.

Hamna mkristo anayo itetea Israel,halafu huu mgogoro sio wakidini kabisa,hebu fuatilieni historia yake,huu ni mgogoro wa watu wanaogombania ardhi yao.

Kwa taatifa yako Israel waislam ni wengi kuliko wakristo na wakristo palestina wapo kibao na wengine wapo kwenye hilo viguvugu la hao Hamas na Waislam kutoka Israel wanatumika sana kuspy nchi za Kiarab.

Nyerere,Kwame Nkurumah,Mandela,Mashele nk hawa wakristo ila walikataa kulitambua taifa la Israel.

Husichanganye kabisa,huu mgogoro wa kulaumiwa ni UK na UN.
 
Waachieni Israel mji wao kwakweli , Jerusalem tunaijua yangu kale Ni ya wayahudi , inakuwaje Leo wapalestina wanasema Ni Yao? Ina maana wakina mfalme Daudi na kina Suleiman waliiosimamisha ngome kubwa Jerusalem walikuwa wapalestina? Tuache ujinga na wapalestina waache ujinga
 
Labda huijui Historia ya Israel na Ardhi hiyo.

Kabla ya vita ya pili ya Dunia, Hakukuwepi na wadudu wanaoitwa wapalestina.

Vita ya Pili ya Dunia, ambayo Hitler na wapuuzi wa Catholics Kwa lengo la kuwaondoa Waisrael, walifanikiwa kuwaondoa Waisrael wote katika Ardhi Yao , wakakimbikia mataifa mbalimbali.

Kuondoka kwao pale kwenye Ardhi Yao, kukatoa nafasi ya Jesuits wa Rumi, kupeleka wahamiaji kwenye Ardhi hiyo...wahamiaji hao ndo Leo wanaitwa wapalestina.

Baada ya Vita ya Pili, Waisrael wakajikisanya ili waanze kurudi kwenye Mother land Yao.

Ndipo walipokuta Kuna wahamiaji , na Vita ikaanzia hapo.

Mpaka Leo !!!!
Kasome tena historia umedanganywa,kabla ya vita ya kwanza ya dunia kulikuwa hamna taifa la Israel,kipindi kile wazungu wanagawana makoloni yao,UK aliamua kuigawa ardhi ya Palestina kwa Waisrael,nchi nyingi zililalamikia hili baadae UK akaona aibu akaamua kupunguza kumuunga mkono. Baada ya hapo Israel akawa anajiongezea ardhi ya Palestina atakavyo na baada ya vita ya dunia UN wakalazimisha mataifa mengine kuitambua Israel kama taifa kamili.

Nchi nyingi zilikataa mpaka Nyerere na wanaharakati wote wa Afrika walikaaa hili na ndio maana Nyerere mpaka anaondoka madarakani Israel hakuwa na ubalaozi Tz na nchi nyingine za Africa.

Ndio maana mpaka kesho nchi zote za Afrika zilikuwa zinamtambua Yassir Arafat kama Mwanaharakati na mpigania uhuru mwenzao na sio gaidi kama waiminivyo nchi za magharibi.

Catholics hausiki kabisa katika vita ya Israel na Palestina, wahusika wakuu ni UK ,UN na sasa hivi US ndio anawapa support sana Israel.
 
Mm Kuna Mda najiuliza Hawa ndugu zetu Mungu gani wanamwabudu ambaye hajui utu pamoja na Amani?? Kuna video naiona wanaua raia wasiokua na hatia na kuwatesa Huku walisema Allah Akibhar sjui kwann wanafanya.
Anyway watakacho enda kukutana nacho watajuta maisha yote. Maana Mungu aliapa Kuwa Kamwe Israel hakuna Taifa litakalo kuja kuinyanyasa akasema nitambariki yule atakae kubariki, nitamlaani yule atakae kulaani.

#westandwithIsrael
#PrayforIsrael🙏🙏🙏
#GodblessIsrael🙏
 
Netanyahu: 'We are at war and we will win'​

Israeli Prime Minister Netanyahu has just released a statement, saying that "we are at war and we will win".

In a statement released on his social media channels, he said Hamas would "pay a price the type of which it has never known".

The Israeli Defence Forces (IDF) are fighting Hamas in a number of locations, with an unknown number of casualties.

===========================

Mwishowe Israel itajibu kwa nguvu kubwa na atadhibiti maeneo mengi zaidi ya Wapalestina, hata Gaza huenda ikarudi kwenye udhibiti wa Israel........ardhi kubwa zaid ya Wapalestina itakaliwa na Israel kimabavu.

Raia wa kawaida wa Wapalestina wataishia kuwa wahanga wa huu uhuni uliofanywa na Hamas.

Israel-Gaza latest: Hamas fighters on the ground after '5,000 rockets' fired; 'We are at war', says Netanyahu
Unaandika kwa Mahaba ya Kiisraeli Israel.
 
Back
Top Bottom