Yanayosemwa kuhusiana na Askari huyu yana ukweli?
Mtandao X umejaa wafata mkumbo .na uwabuluza sana mazombie kule kila mtu ni jasusi siku izi
 
Assistant Superintendent of Police (ASP) Fatuma Kigondo. Huyu ni afisa wa Jeshi la Polisi. Fatuma ndiye yule ‘afande’ aliagiza ‘JM’ abakwe na kulawitiwa.Assistant Superintendent of Police (ASP) Fatuma Kigondo ni msaidizi wa mkuu wa kituo cha polisi - Bunge (Dodoma). Ni afisa anayefahamika sana.

‘JM’ alikuwa mfanyakazi wake. ASP Fatuma Kigondo akahisi bwana wake (jina lake tunahifadhi kwa hatua za sasa) ana mahusiano na ‘JM’. Akaagiza atekwe.

ASP Fatuma Kigondo anamiliki grocery na liquor store Dodoma. JM ni mmoja kati ya wafanyakazi katika moja kati ya grocery au bar za ASP Fatuma Kigondo.

JM alikuwa anatoka kazini saa tano usiku, akavamiwa na pikipiki mbili, wakashuka watu watano wakiwa na visu mkononi. Wakamchukua na kuondoka naye.

JM amebakwa na kulawitiwa usiku huo hadi kesho yake asubuhi. Video ile imerekodiwa asubuhi wakati wahuni hao wanamaliza kufanya uhalifu.

Chanzo: Boniface Jacob Kupitia X na pia Martin Maranja kaandika

Pia soma: Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa

Pia, Kumbukumbu zinaonesha Askari Fatuma Kigondo aliwahi kutoa ushahidi Tarehe 18, Desemba 2017 akiwa shahidi wa upande wa Jamhuri kwenye Kesi dhidi ya JamiiForums, kwa kosa la kukataa kutoa “taarifa za mteja wao”.

Fungua kiungo hiki kusoma ushahidi huo: Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai waliomba taarifa za mteja bila kutaja ni kwa mujibu wa sheria gani
Mbona taarifa inachanganya!?
Binti ni wa Buza Dar es salaam au wa Dodoma!?
 
Hakuna kesi hapo , nawaambiaga Kesi ya wakubwa utanukumbusha kwamba waliizuga Zuga tu, wameshaichezesha kitambo! Wanasema wamekamatwa Kuna mwenye ushahidi kwamba kuna alokamatwa?

Uongo uongo tu

Britanicca
Hii ni kesi kubwa sana ishakuwa ya public interest na public relations nightmare kwa serikali, usiichukukie poa tu.

Kuna kesi nyingine zikishakuwa kubwa sana, hata mtu mkubwa anaondoka.

Kashitakiwa Ditopile Mzuzuri best man wa rais Kikwete, wakati Kikwete ni rais, na kafungwa.

Kwa nini? Issue ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba hata Kikwete aliona kuingilia kutamchafua yeye.

Tatizo hapa ni Polisi kuchunguza Polisi, na hawa wanajuana na wote wana madudu. Ila, walio juu wakitaka anaondoka na maji tu.
 
Mkuu,

Fatuma mume wake alishafariki siku nyingi. Na baada ya hapo hakuolewa tena.

Hata huyo anayesemwa mume wa mtu, si mume wa mtu.
 
Hii ni kesi kubwa sana ishakuwa ya public interest na public relations nightmare kwa serikali, usiichukukie poa tu.

Kuna kesi nyingine zikishakuwa kubwa sana, hata mtu mkubwa anaondoka.

Kashitakiwa Ditopile Mzuzuri best man wa rais Kikwete, wakati Kikwete ni rais, na kafungwa.

Kwa nini? Issue ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba hata Kikwete aliona kuingilia kutamchafua yeye.

Tatizo hapa ni Polisi kuchunguza Polisi, na hawa wanajuana na wote wana madudu. Ila, walio juu wakitaka anaondoka na maji tu.
Ditopile alifungwa?
 
Back
Top Bottom