Uchaguzi 2020 Yanayotokea Tanzania Leo yalitokea Indonesia 1998

Sawa naheshimu mawazo yako.
 
Media zinajipendekeza tu hakuna lolote. Kwa taarifa yako, media nyingi ziko hoi kwa sababu umma umepoteza imani nazo.
 
Kama wakoloni waliweza kubadili mind set zetu na kukubali ku slimu na kubatizwa na kuacha kutambikia mizimu. Tulianza kwenda hospitali tukiugua badala ya kuchemsha mizizi.

Tena siku hizi kuna mass media kuelimisha wananchi inawezekana.
Ndiyo hivyo jiwe anawabadili watu tabia lakini itachukua muda kufanikisha hilo.
Kelele 'mingi' sana, na usaliti mwingi mno.
 
Kamsalimie che nkapa huko aliko
 
Media zinajipendekeza tu hakuna lolote. Kwa taarifa yako, media nyingi ziko hoi kwa sababu umma umepoteza imani nazo.
Kwa sababu mabadiliko ya kiteknolojia kwa dunia nzima, na hapa kwetu kuna tatizo la ziada la kuhamishia zabuni za miradi mbali mbali na matangazo kwenye taasisi za umma.
Lakini siyo vitisho. Kwanini uogope kuandika au kurusha matangazo kama kinachotangazwa ni sahihi hakivunji sheria?

Mdororo wa vyombo vya habari ni knock-off effect ya zabauni zote kupewa taasisi za umma.
 
Sisi wa vijijini, mnatuchukulia pouwa ee? Unafikiri tunafuraia mipaka kufungwa na bei elekezi ya mazao tuliyo lima kwa gharama zetu!? Jidanganye kwamba sisi wa vijijini ni mtaji wenu! #sasabasi
 
Mengine sitakomenti. Ila unapoongelea zabuni kupewa taasisi za umma, hapa unaonyesha huna uelewa wa mambo ya kiuchumi wala biashara.
 

Kwahiyo kwa maelezo haya gazeti la Tanzania daima litafunguliwa kwakuwa sasa hivi waliolifungia wanaona aibu! Kwa hiyo hao cdm wangekuwa na vyombo vyao ambavyo vinaweza kufungiwa wakati wowote, lakini vinaweza kurusha matangazo wakati wa uchaguzi kisa kuna kundi la viongozi linaona aibu? Unajua kwanini unakuja na utetezi wa kuokoteza usiokuwa na mashiko, kwakuwa umeamua kutetea tabia binafsi za mtu zisizo kwenye utaratibu wowote.
 
Nikweli but just think Lisu Kuwa Rais? Or Member? Nadhan nibora tuongozwe na Jiwe Tu. Tunasafari ndefu Sana bado vyama vya upinzani Kuwa vyenye uwezo kutuongoza. Tutakuwa tumepoteza
Sijui kwa nini unaona waliopo ccm wataweza au unavyosema Magufuli afadhali aendelee kuliko upinzani?
Kwani wao wana nini
Huyo unayemtetea amewahi kuzungumza nini cha maana
Lissu/Membe sio walipa visasi ndio maana mahubiri yao hayawavutii
Huyu alivyoingia si wengi walisema haya
Safari bado ni ndefu lakini tunahitaji chama tawala kiwe upinzani hata kwa 5yrs Tutarekebishana ndipo tutaenda sawa
Usiwadharau waliojitoa kuleta mabadiliko kwani wana haki kikatiba
Au mna mpango wa kupoteza wengine kama Ben Saanane

Kuweni na utu kidogo mnazingua sana mjue
 
Nadhani hukusoma maelezo " vyombo vya habari vya chama siyo vya mwanachama "
Pia ningependa nikuambie hilo neno aibu limetumika kukwepa neno flani.
Nakuachia kitendawili.

Mwisho wa siku haya ni maoni tu siyo kusema nisemacho ndiyo sahihi.
Naheshimu maoni yako pia kwa leo niishie hapa mjadala huu.
 
Sisi wa vijijini, mnatuchukulia pouwa ee? Unafikiri tunafuraia mipaka kufungwa na bei elekezi ya mazao tuliyo lima kwa gharama zetu!? Jidanganye kwamba sisi wa vijijini ni mtaji wenu! #sasabasi
Bei elekezi umepewa na nani wakati kila siku Bashe amekuwa muumini wa soko huria, tena kaenda mbele zaidi na kupendekeza ‘price floor’ ikibidi serikali kufidia deficit pale ambapo bei za soko zikishuka sana yote hayo mkulima alindwe.

Wewe utakuwa sio mkulima wala mwanakijiji vinginevyo ungeona jitihada za serikali nina wasiwasi ni mkazi wa Dar maana ata hujui kinachoendelea mashambani.
 
Mkuu huyo ukimtajia Ben Saa8 tu, umemaliza!
 

Hapa naona unjivunia wanakijiji kwasababu ni rahisi kuwadhibiti wasipaze sauti zao kutokana na umasikini wao. Huko vijijini inajengwa taswira kuwa wanaikubali ccm, kwakuwa mifumo na mazingira haiwaruhusu kuweka hisia zao hadharani. Huku mjini kuna watu wengi wenye uelewa wa mambo, ndio maana ccm haijivunii, maana sio rahisi kuuongopea umma kuwa wanakubalika, hiyo ndio inayopelekea matumizi makubwa ya nguvu, ushenzi na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi maeneo ya mijini.

Laiti mazingira yangekuwa rafiki huko vijijini,hisia za wanakijiji zingekuwa wazi, lakini mazingira yaliyopo ni ngumu kwa wanakijiji kuweka hisia zao hadharani, zaidi ya wao kujifanya wanaikubali ccm kwa shingo upande. Na hata hiyo kuwa wanavijiji wanaokubali ccm sio kweli, maana wapinzani wakifika huko na kuwaamsha wote hujikuta hawaitaki ccm. Kisa cha Magufuli kupiga marufuku vyama vya siasa kuzunguka nchi nzima, ni kuhakikisha watu wa vijijini hawatoki kwenye gereza la ccm, ambalo huwa wanawatumia bila ridhaa yao.
 
😂😂😂😂 !! As you wish, ila ujue huku kijiji tuna akili pia!
 

Inaonekana una majibu yako mfukoni, nimekuambia iwapo vyama haviruhusiwi kufanya mikutano, wala kuzunguka nchi nzima, hivyo vyombo vyake vya habari ndio vitaruhusiwa kutangaza bila kufanyiwa figisu? Nakutakia mchana mwema baada ya kuishiwa hoja.
 
saivi acha kwanza tumalize na huyu alieshushwa kukomboa waja wake. BTW tunafikilia atawale milele.
 
Kwa upinzani wa GIA ZA ANGANI,KUZUNGUSHA MIKONO NA KUHAMAHAMA VYAMA HOVYO.


MTATOA MIFANO MPAKA YA MAIGIZO YA BONGO MOVIES
 
Inaonekana una majibu yako mfukoni, nimekuambia iwapo vyama haviruhusiwi kufanya mikutano, wala kuzunguka nchi nzima, hivyo vyombo vyake vya habari ndio vitaruhusiwa kutangaza bila kufanyiwa figisu? Nakutakia mchana mwema baada ya kuishiwa hoja.
Nakubali nimeishiwa hoja mkuu.
Mchana mwema pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…