Yanga ikitwaa Kombe la Shirikisho itapata Tsh. Bilioni 4.7, ikifungwa itapata Tsh. Bilioni 2.3

Huwa inafanyika katika kila hatua na mara nyingi huwa wanaita ni PESA ZA MAANDALIZI. Kwahiyo huwa kuna PESA ZA MAANDALIZI katika kila hatua ambapo timu itakuwa imefuzu.
 
Simba anapewa Dola 2.5m kujiandaa Tu Kwa CAF superleague
 
Ikiwa kila kitu kitabaki sawa halafu tupate na nyongeza ya mwamba mpambanaji Ranga CHIVAVIRO, Yanga hii utazidi kuipenda ndani na kimataifa.
Na huku ndani magolikipa watakuwa wanasingizia kuumwa vidole kila siku kukwepa lawama.
Kila mnayekutana naye mnataka wachezaji wao, hii ni dalili bado hamjapevuka kwenye mambo haya ya kimataifa.
 
Huwa inafanyika katika kila hatua na mara nyingi huwa wanaita ni PESA ZA MAANDALIZI. Kwahiyo huwa kuna PESA ZA MAANDALIZI katika kila hatua ambapo timu itakuwa imefuzu.
Hapana mkuu hiyo utapata kiasi cha pesa kulingana na unapoishia tu, ukisonga mbele pesa ya hatua ya mbele imejumuisha hatua zote za nyuma

Naomba nitolee mfano kiwango cha pesa kilichotelewa msimu uliopita kabla ya kuongezwa pesa kwa siku mbili hizi.

Jumla ya pesa waliyotenga CAF katika michuano ya klabu bingwa ni usd milioni 12 5
Sasa tukienda kwenye uhalisia/ mchanganua wa hizo dola milioni 12.5 ni kama ifuatavyo

Jumla kuna makundi manne na katika kila kundi lazima zitolewe timu mbili na kisha timu mbili ndio zinazonga mbele, hivyo kuna timu nane zitaaga mashindano, hawa wanaoga wanapewa dola 550,000
Hapo inakatika 8 x 550,000 = usd 4,400,000

Baada ya timu nane kuaga, timu nane zilizobaki zitakuwa zimefuzu robo fainali, lakini kwenye hii hatua kuna timu 4 zitaenda mbele na 4 zingine zitakuwa zimeaga mashindano na kuishia robo yao (wakina robo fc)
Hapo itakatika 4 x 650,000 = usd 2,600,000

Hapo juu kuna timu nne zimetolewa na nne zikasonga mbele na kucheza hatua ya nusu fainali hivyo kwa vyovyote vile lazima timu mbili ziage.
Hapo tena fungu la CAF linamegeka tena
2 x 875,000 = usd 1,750,000

Timu zilizobakia ni mbili tu ambazo zitacheza fainali na bingwa atapata usd 2,500,000 na mshindi wa pili anapata usd 1,250,000.

Ukijumlisha usd 4,400,000
usd 2,600,000
usd 1,750,000
usd 2,500,000
usd 1,250,000
Ukijumlisha utapata jumla ya usd 12,500,000 (usd 12.5M) ambayo ndio jumla ya mpunga unaotolewa na CAF kwenye michuano ya klabu bingwa kwa msimu wa nyuma
 
Yanga anamaliza mechi next wiki akienda kule anaushindi wa goli 3 please mark maneno yangu congratulations kwao
 
Nyanga pesa walizopata tokea makundi ni nyingi sana. Waanze kujenga uwanja sasa. Bajeti ya bln 10 unatosha uwanja
 
Ukiachana na zawadi ya UBINGWA, ina maana kwa lugha nyingine timu iliyofika fainali kwa ngazi ya SHIRIKISHO mpaka sasa hivi itakuwa imeshakusanya zaidi ya USD 2.0 MILLION kwa sababu kila hatua waliyokuwa wanavuka walikuwa wanapewa kitita cha pesa.
Huu utaratibu unaongeleqa sana mtaani. Ila mimi ninachofahamu, timu inapotolewa katika hatua fulani, ndiyo hupatiwa hicho kiasi. Ila ikitokea ikaendelea, haipewi.

Yaani mfano Yanga ina uwezo wa kupewa hela ya mshindi wa kwanza, au wa pili. Ila siyo hela za makundi, robo fainali, na nusu fainali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…