Hapana mkuu hiyo utapata kiasi cha pesa kulingana na unapoishia tu, ukisonga mbele pesa ya hatua ya mbele imejumuisha hatua zote za nyuma
Naomba nitolee mfano kiwango cha pesa kilichotelewa msimu uliopita kabla ya kuongezwa pesa kwa siku mbili hizi.
Jumla ya pesa waliyotenga CAF katika michuano ya klabu bingwa ni usd milioni 12 5
Sasa tukienda kwenye uhalisia/ mchanganua wa hizo dola milioni 12.5 ni kama ifuatavyo
Jumla kuna makundi manne na katika kila kundi lazima zitolewe timu mbili na kisha timu mbili ndio zinazonga mbele, hivyo kuna timu nane zitaaga mashindano, hawa wanaoga wanapewa dola 550,000
Hapo inakatika 8 x 550,000 = usd 4,400,000
Baada ya timu nane kuaga, timu nane zilizobaki zitakuwa zimefuzu robo fainali, lakini kwenye hii hatua kuna timu 4 zitaenda mbele na 4 zingine zitakuwa zimeaga mashindano na kuishia robo yao (wakina robo fc)
Hapo itakatika 4 x 650,000 = usd 2,600,000
Hapo juu kuna timu nne zimetolewa na nne zikasonga mbele na kucheza hatua ya nusu fainali hivyo kwa vyovyote vile lazima timu mbili ziage.
Hapo tena fungu la CAF linamegeka tena
2 x 875,000 = usd 1,750,000
Timu zilizobakia ni mbili tu ambazo zitacheza fainali na bingwa atapata usd 2,500,000 na mshindi wa pili anapata usd 1,250,000.
Ukijumlisha usd 4,400,000
usd 2,600,000
usd 1,750,000
usd 2,500,000
usd 1,250,000
Ukijumlisha utapata jumla ya usd 12,500,000 (usd 12.5M) ambayo ndio jumla ya mpunga unaotolewa na CAF kwenye michuano ya klabu bingwa kwa msimu wa nyuma
View attachment 2627782