benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
UONGOZI wa Young Africans Sports Club umetoa taarifa ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Me. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hafla ya kuipongeza klabu hiyo kwa kucheza mchezo wa Fainali ya Kombe la Shikirisho la CAF, Msimu huu.
Katika taarifa hiyo mbali na mambo mengine imemshukuru Rais Samia kwa kwa zawadi ya Tsh Milioni 40 aliyoitoa kwa benchi la ufundi na wachezaji kwa kucheza mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Pia ikumbukwe kupitia hamasa yake ya "Goli la Mama"Klabu yetu imeweza kujipatia kiasi cha Tsh Milioni 135 kwa jumla ya magoli 17 tuliyoyafunga kuanzia hatua ya Makundi hadi kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
Yanga pia imemshukuru Rais Samia kwa kutoa usafiri wa ndege kwenye safari mbili za kuipeleka timu, moja ikiwa ni nchini Algeria, kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho la CAF na nyingine ni mkoani Mbeya kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu ya NBC.
N.B
Kwa hesabu hizo Klabu ya Yanga imepata jumla ya Shilingi Milioni 175 kutoka kwa Rais Samia Suluhu
N.B
Kwa hesabu hizo Klabu ya Yanga imepata jumla ya Shilingi Milioni 175 kutoka kwa Rais Samia Suluhu