Yanga msitolewe kwenye njia na mashabiki oyaoya, timu mnayo

Yanga msitolewe kwenye njia na mashabiki oyaoya, timu mnayo

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Kuna baadhi ya mashabiki oya oya na wale wa makoro koro FC wanataka kutumia mechi ya yanga ya jana kufungwa Kama kichaka cha kueneza propaganda ya kuwa yanga imesajili vibaya.

Watu hao nafikiri hawako timamu kwenye masuala ya kuangalia timu kiufundi bali wanasukumwa na mihemuko aidha ya chuki binafsi au kutokuelewa mpira wenyewe unaochezwa.

Yanga jana imecheza na timu bora inayotoka ligi bora nchini Zambia, yanga imecheza na timu iliyoanza preseason tokea tarehe 1/8 , wamecheza mechi za kirafiki 6 kujiweka sawa na iyo imechagizwa na logo yao kumalizika mapema kabisa mwezi wa 6.

Hivyo ni timu ambayo imeshajiset kimuunganiko na kimaandalizi pia, yanga yenyewe ndo mechi ya kwanza ya maana ya kirafiki ambayo imewapa mwanga waanzie wapi kurekebisha panapovuja,,mda wa maandalizi kwa yanga aukuwa rafiki kutokana na ligi yetu pia kuchelewa kumalizika.

Isingewezekana eti unaanza maandalizi moja kwa moja kwa kucheza mechi za kirafiki iyo kitu aipogo duniani kwa kocha yeyote, maana kuna wajinga wengine wamekomaa na yanga kutocheza mechi za kirafiki wakati kitaalam lazima uanze na mazoezi ya viungo, utimamu wa mwili na mazoezi mengine magumu ya kuuandaa mwili vizuri kwaajili ya mechi zenyewe, hivyo kwa muda huo yanga isingeweza kucheza mechi yoyote ya kirafiki kabla awaajamaliza program husika.

Tayari jana tumeona yanga imefanya usajili bora kabisa kinachofata ni muunganiko na match fitness kwa wachezaji watakuwa wameiweka timu sawa kwa ajili ya mashindano, timu wanayo tena kabambe wasitolewe kwenye njia na wapuuzi wachache wanaotumika na wasiojielewa.
 
Yanga inahitaji muunganiko tu,ile game ya jana wachezaji wenyewe hata wiki hawajakaa pa1,wachezaji waliobaki morocco walifika juzi Tz kujiunga na wenzao,yale matokeo ya kufungwa yameisaidia sana Yanga kwa kujua wanatakiwa wawe serious kinamna gani
 
Kuna baadhi ya mashabiki oya oya na wale wa makoro koro fc wanataka kutumia mechi ya yanga ya jana kufungwa Kama kichaka cha kueneza propaganda ya kuwa yanga imesajili vibaya,,,watu hao nafikiri awako timamu kwenye masuala ya kuangalia timu kiufundi bali wanasukumwa na mihemuko aidha ya chuki binafsi au kutokuelewa mpira wenyewe unaochezwa,,,yanga jana imecheza na timu bora inayotoka ligi bora nchini Zambia, yanga imecheza na timu iliyoanza preseason tokea tarehe 1/8 , wamecheza mechi za kirafiki 6 kujiweka sawa na iyo imechagizwa na logo yao kumalizika mapema kabisa mwezi wa 6, hivyo ni timu ambayo imeshajiset kimuunganiko na kimaandalizi pia, yanga yenyewe ndo mechi ya kwanza ya maana ya kirafiki ambayo imewapa mwanga waanzie wapi kurekebisha panapovuja,,mda wa maandalizi kwa yanga aukuwa rafiki kutokana na ligi yetu pia kuchelewa kumalizika,,isingewezekana eti unaanza maandalizi moja kwa moja kwa kucheza mechi za kirafiki iyo kitu aipogo duniani kwa kocha yeyote,, maana kuna wajinga wengine wamekomaa na yanga kutocheza mechi za kirafiki wakati kitaalam lazima uanze na mazoezi ya viungo,utimamu wa mwili na mazoezi mengine magumu ya kuuandaa mwili vizuri kwaajili ya mechi zenyewe,, hivyo kwa muda huo yanga isingeweza kucheza mechi yoyote ya kirafiki kabla awaajamaliza program hu sika,, tiyali jana tumeona yanga imefanya usajili bora kabisa kinachofata ni muunganiko na match fitness kwa wachezaji watakuwa wameiweka timu sawa kwa ajili ya mashindano, timu wanayo tena kabambe wasitolewe kwenye njia na wapuuzi wachache wanaotumika na wasiojielewa

Kwani wewe unajielewaa mkuu?

Siku zote hizo bado mnafanya mazoezi ya viungo tu? Mkaenda hadi Morroco[emoji23]

Njooni mjiunge na jogging club tu[emoji23]
 
Screenshot_20210830-081325_Gallery.jpg
 
mnatumia nguvu kubwa kupaka rangi uchafu lakini hata mechi ya jana inatosha kutoa picha kwamba kuna kazi ya kufanya,tena kubwa tu

wiki mbili zijazo timu ina game ya mtoano club bingwa africa halafu leo tunaona sawa tu kufungwa na tunatoa excuse ya hakuna muunganiko

huo muda wote kocha alikua anafanya nini,timu imeenda morocco hata sijui kufanya nini sababu sijawahi kuona pre season ya siku sita jamani hata siku moja,unamaliza pre season bila hata mechi moja ya majaribio..kwanini!?

tuseme ukweli..timu yetu sisi bado,uwekezaji unaofanywa hautakiwi kupigiwa kelele kwamba mwaka huu utaleta matokeo kama wanavyotujaza viongozi

gsm waseme ukweli...siyo kuongea kaa anavyoongea manara,hivi kweli jwa akili zetu,yanga inaweza kuchukua makombe yote itayoshiriki msimu huu!??

manara halafu hatuheshimu...kule simba alikua anasema watachukua ligi na FA,club bingwa alikua anasema kabisa kwa hatua ya sasa simba haiwezi kubeba..labda kwa fluke

ila leo anasema yanga itabebaa kila kombe including champions league...hizi ni dharau
 
Mwisho wa siku musimu unaisha mkiwa hamjapata muunganiko...sijui ni Muunganiko mwingine wa Tanganyika na Zanzibar?

Halafu anayewaambia kila mwaka muwe mnasajiri kikosi kizima kipya ni nani? Hiyo Chemistry sijui Bookkeeping mtaipata lini?

Mna maandalizi mabovu ya pre-season na bado mkawahi kuvunja kambi ili mumuwahi fundi Michael awashonee suti? Wenzenu Simba wamestay longer kule,halafu wakianza kukinukisha muanze kulialia Simba wanabebwa.

Kwa maandalizi mabovu mliyoyafanya, mbwembwe nyinyi with poor strategy nawaona mkiondoshwa mapema Klabu Bingwa. Hilo hata Koffi Olomide analijua na ndo maana alikuwa desperate kupiga show ya maana, aligundua alijishusha too low kukubali kuwanengulia Uto.
 
Kuna baadhi ya mashabiki oya oya na wale wa makoro koro fc wanataka kutumia mechi ya yanga ya jana kufungwa Kama kichaka cha kueneza propaganda ya kuwa yanga imesajili vibaya,,,watu hao nafikiri awako timamu kwenye masuala ya kuangalia timu kiufundi bali wanasukumwa na mihemuko aidha ya chuki binafsi au kutokuelewa mpira wenyewe unaochezwa,,,yanga jana imecheza na timu bora inayotoka ligi bora nchini Zambia, yanga imecheza na timu iliyoanza preseason tokea tarehe 1/8 , wamecheza mechi za kirafiki 6 kujiweka sawa na iyo imechagizwa na logo yao kumalizika mapema kabisa mwezi wa 6, hivyo ni timu ambayo imeshajiset kimuunganiko na kimaandalizi pia, yanga yenyewe ndo mechi ya kwanza ya maana ya kirafiki ambayo imewapa mwanga waanzie wapi kurekebisha panapovuja,,mda wa maandalizi kwa yanga aukuwa rafiki kutokana na ligi yetu pia kuchelewa kumalizika,,isingewezekana eti unaanza maandalizi moja kwa moja kwa kucheza mechi za kirafiki iyo kitu aipogo duniani kwa kocha yeyote,, maana kuna wajinga wengine wamekomaa na yanga kutocheza mechi za kirafiki wakati kitaalam lazima uanze na mazoezi ya viungo,utimamu wa mwili na mazoezi mengine magumu ya kuuandaa mwili vizuri kwaajili ya mechi zenyewe,, hivyo kwa muda huo yanga isingeweza kucheza mechi yoyote ya kirafiki kabla awaajamaliza program hu sika,, tiyali jana tumeona yanga imefanya usajili bora kabisa kinachofata ni muunganiko na match fitness kwa wachezaji watakuwa wameiweka timu sawa kwa ajili ya mashindano, timu wanayo tena kabambe wasitolewe kwenye njia na wapuuzi wachache wanaotumika na wasiojielewa

Mkuu umeandika mengi lakini ukienda kwenye msingi wa tatizo la Yanga ni maandalizi mabovu ya kikosi. Wewe ndio utakuwa mmoja wapo wa mashabiki wasiojua sayansi ya mpira. Badala ya kupiga kelele kipindi cha pre season timu yako iwe serious na maandalizi ya kikosi unakuja kutetea ujinga hapa.

Kalenda ya CAF ilitoka mapema sana, timu yenye malengo na mikakati imara ingefanya mambo yake kwa kujali muda uliopo ili kufanya maandalizi thabiti kuelekea kwenye msimu mpya lakini ujinga wa waendeshaji wa timu na viongozi wakaona ni heri kuwekeza kwenye siasa, propaganda, na biashara kuliko kuandaa timu matokeo yake ndio hayo. Mpira sio maneno mkuu bali ni maandalizi mazuri ya kikosi. Muda uliokuwepo ilikuwa unatosha sana kuandaa timu mbona Simba wameweza kufanya mazoezi yote ya viungo na kucheza mechi za majaribio.

Leo hii mechi ya Zanaco inaionekana kama kipimo cha kuanza na upya kuelekea kwenye mechi ya klabu bingwa wakati ilipaswa mechi ya leo itumike kwaajili ya kuziba vinyufa vidogo vidogo. Mbaya zaidi unaenda kucheza mechi ya klabu bingwa pasipokujua kama makosa yamerekebishika au lah. Timu haina muunganiko wala hauna match fitness hata iwe na wachezaji wazuri kiasi gani ukikutana na timu iliyokuwa organised lazima tu wafungwe.

Swala la kusema muda haukuwepo nakukatalia muda ulikuwepo mwingi sana wa kujiandaa ila waendeshaji wa timu wamefeli.
 
Yanga kwa matukio ya kuwapa furaha mashabiki wana PhD, ila uwanjani tu ndio changamoto.

Yanga inaendeshwa na kiki.
 
Back
Top Bottom