Mimi nakubaliana na wewe kabisa kuwa mkopo si mapato. Ila pia kutoendesha biashara kwa hasara haina maana lazima uwe na faida. Pia kuwa na mkopo haizuii taasisi kuripoti faida mwishoni mwa mwaka. Loan repayment itategemea walipata mkopo mwezi gani ili hizo repayment zionekane kwenye vitabu.
Sasa mkuu Yanga hawana faida.
Wamekusanya billion 12.5
Kwenye matumizi wakajikuta wanatumia billion 17.3
Kwa sababu kiasi cha matumizi hakitoshi wakakopa billion 4.8
Kiasi kiichobaki ni million 500
Hiki ni kiasi kilichobaki kwenye mkopo huwezi kuiita faida kwa sababu siyo sehemu ya fedha yao.
Wakiamua kukitumia ni wamekula mkopo na siyo faida.
Ila kama mkopo ungelipwa au unalipwa mwaka ujao hapo hiyo m 500 kuita faida ni sawa kwa muda huu.
Na jambo lingine ni kwanini walikopa kiasi kikubwa kuliko mahitaji..
Kwenye hesabu yao walihitaji billion 4.3 wao wakakopa billion 4.8.
Kiasi kilichobaki katika mkopo ndo wamekiita faida jambo ambalo katika hesabu za kifedha lazima kizalishe maswali.
Jambo lingine ni mkopo huu haujawekwa wazi kwetu mashabiki ili tujue aina ya mkopo wenyewe.
Kama ni kweli wama bajeti billion 20 mwaka ujao.
Na kwa mwaka huu vyanzo vyao vya mapato vimeweza kukusanya billion 12.6+5 tu ina maana mwakani itawalazimu kukusanya billion 20+ ili waweze kupunguza mkopo wao wa billion 4. 8 na kutumia fedha kwa ajili matumizi.