Yanga SC yaingia mkataba na GSM wa miaka 5 kutengeneza vifaa vya michezo wenye thamani ya bil 9.1

Yanga SC yaingia mkataba na GSM wa miaka 5 kutengeneza vifaa vya michezo wenye thamani ya bil 9.1

Sasa hapa uto mnaaminije kwamba hiyo pesa kweli ataiweka GSM kwenye akaunti wakati mkurugenzi mwenyewe wa kampuni ndiye m/kiti wa klabu?Hamuoni kwamba hapa kuna mgongano wa kimaslahi?

Mwanafunzi wa darasa la 7 kajitungia mtihani mwenyewe, kaufanya mwenyewe kajisimamia mwenyewe , kajisahihisha mwenyewe, Matokeo anapanga mwenyewe , anasoma Matokeo mwenyewe , halafu anawalazimisha drs la 1 hadi 6 wamshangilie na kweli wanamshangilia .Maajabu hayaishi nchi hii.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Hata isipowekwa ila ilimradi timu inashinda ,inasafiri, wachezaji wanalipwa mishahara na posho kwa wakati na wanakaa Kambi nzuri hatujali.
 
Mkituoñyesha pia b.2 za vunja bei ziliingia account gani basi na yanga watawaonyesha wameweka benk gani
Sisi hatuna shida na uto pesa zenu mmeweka a/c gani mtajua wenyewe na utopolo wenu
 
Ni Lini Yanga Walitangaza Walitangaza Tender Kwa ajili ya Utengenezaji Wa Jersey na Kits Mbali²?.
.
Yanauliza hivi Sio Kwa Sababu napingana na Viongozi Wa Yanga Hapana Ili Kuondoa Maneno ni Bora Yanga Wangetangaza Tender ya Utengenezaji Wa Jersey na Kits mbali² za Team then Jiesiem Pia akawemo km Muombaji.
.
Kama Team yangu Ya Yanga inaongozwa na Wasomi Tena Vijana Basi wafuate utaratibu Wa Upatikanaji Wa Watengenezaji Wa Vifaa.
.
Nmeona Kuna Pahala Mtu Kaandika Gsm Yaingia Mkataba wa Utengenezaji Wa Jersey na Gsm
.
I stand to be Corrected [emoji120][emoji120][emoji120]
 
umaskini wa Timu zetu hisi ndugu yangu we acha tu.
Hata haijulikani kuwa ni lini ilitangazwa kuhitajika mtengenezaji wa jezi na vifaa vingine. Wanajichotea tu. Turejee kauli ya LUC EMELY na ile clip ya manara anayosema watu wa yanga akili zao zina fanana. Kutwa utawakuta wana mjadili Mo na simba bila kuangalia upande wao. Waswahili husema "nyani haoni kundule"
 
Hiyo tender ilikuwa na ushindani? if yes, GSM walishindanishwa na nani? if No, utopolo hamuoni kama Hersi na ndugu zake GSM wamewaweka mfuko wa nyuma wa suruali zao, tena wamewachanganya na leso kwenye mfuko huo huo?
 
Ndo nilitaka yule kilaza anijibu alafu aniambie wao kwa mwaka kwrnye b.2 wanapewa bei gani, maana nimeona kama vile dish lake limeyumba hivi
Mara zote simba anaongoza njia wewe unafata. Baada ya kuona ssc anapata b kwa mwaka wakati wewe unapata 13,500 kwa kila jezi kiongozi wenu akaona aongeze sifuri ili kuendelea kuwapumbaza, Nawaambia mtapigwa machanga ya macho mengi sana kwa jiesem
 
Hiyo tender ilikuwa na ushindani? if yes, GSM walishindanishwa na nani? if No, utopolo hamuoni kama Hersi na ndugu zake GSM wamewaweka mfuko wa nyuma wa suruali zao, tena wamewachanganya na leso kwenye mfuko huo huo?
na tishu ya kufutia kinyesi vyote wamechanganywa navyo
 
Hiyo tender ilikuwa na ushindani? if yes, GSM walishindanishwa na nani? if No, utopolo hamuoni kama Hersi na ndugu zake GSM wamewaweka mfuko wa nyuma wa suruali zao, tena wamewachanganya na leso kwenye mfuko huo huo?
Vunjabei alishindana na nani?
 
Mkuu wale jamaa Rage alishaga walaani, yaani akili zao ni nusu kijiko wanazo za kuvukia barabara tu utaangaika nao hapa utapoteza muda wako bure kuwajibu, msongo wa mawazo walionao ni mkubwa wanaitaji mtaalamu wa saikolojia haraka sana
,[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
HIVI tuulizane hapa,kabla ya Hawa wahindi sijui waarabu ambao mnasema wanazinyonya hizi club zetu,timu zetu hizi Simba na YANGA zilikuwa na thamani ambayo tunaiona Sasa!?

Mimi acha niseme ,anayejua Kula na kipofu hawezi kumstua kipofu,timu hizi zote zina uongozi na Wana malengo yao ambayo wameyaweka wazi na tukumbushane MPIRA NI MCHEZO WA WAZI KWENYE KILA IDARA IWE NDANI YA UONGOZI AMA UWANJANI KWA WACHEZAJI.

Itafikia wakati tutajua Nani kaliwa Nani kala,tuache kuangalia kwa kutafuta makosa.Sasa hivi hizi timu zinasajili wachezaji wenye ubora kwa gharama kubwa na mishahara mikubwa na hakuna Tena kelele za wachezaji kutokulipwa mishahara,kila kitu kinaendeshwa sawa,miundo mbinu ipo sawa,viwanja vinaanza kujengwa.Simba wanaanza ujenzi,Yanga na wao wapo njiani.Kuna ushindani chanya wa kutafuta MAENDELEO mazuri ndani ya soka let

Halafu ndg yangu unayesema hi mikataba ya B tunazoingiza kupitia wadhamini wetu hawa ni ndogo na unaongeza kabisa tumepigwa,hivi unadhani SIMBA NA YANGA Wana thamani sawa na MADRID,MAN U,BARCA AMA BAYERN!??tuache kulinganisha thamani za waliotuzidi Mara 10000000000 na sisi wa 10.

Wenye kunielewa point wataongezea ila nikitazama tulipotoka na hapa tulipo ,tupo sehemu Bora zaidi na tuendapo ni Bora Bora zaidi na zaidi

BANIYANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA[emoji120][emoji120]
 
hivi mnahisi Yanga au Simba ni klabu ambazo mtu akija anajifanyia TU yake!?hakuna watu wa kuhoji huko juu ila sisi humu ndio tuna uchungu na akili sana kusema haya yote!?

Bado sijaona ubaya wa GSM kuingia mkataba na YANGA hata Kama Raisi wa Yanga ni mshirika pia wa GSM ,amefanya kwa kusaidia pande zote mbili na kwa kutimiza maslahi ya pande zote,hata Kama ningekuwa Mimi ningeangalia maslahi mapana ya klabu,Kama Kuna maslahi kwa Nini nisiunganishe!?

halfu nyie Simba mnaowabeza yanga kwa kuingia mkataba na gsm ambao uko wazi na umetangazwa(siku moja mtu yyte anauwezo wa kuhoji zimeenda wapi maana tayari in uongozi na ipo kisheria) ,naonaga matangazo kibao ya mo kwenye JEZI za Simba,amewapa Bei gani mpaka Sasa kwa kubandika matangazo yake ya mo xtra na mo foundation!?mauzo ya mo xtra moja mnachukua Bei gani!?au ndio kwa sababu Raisi wa heshima!?

C'mon guys Kama NI utani tutaniane ila kwa kujengana sio kubomoana [emoji16][emoji16]
 
Huo mkataba ni makubaliano kati ya GSM kwa GSM wenyewe, ndio maana wajanja tunasema Club imeuzwa.

Huelewi nini hapo? Yani Hersi SAIDI ambaye ni Gsm kaingia mkataba na kampuni ya GSM, mwakilishi wa team asiyefungamana ma GSM ni nani??[emoji16][emoji23].

Ile tenda ya SIMBA SC kuhusu jersey angeichukua MO pasingekalika humu.
GSM NA YANGA,hyo GSM KWA GSM unasema wewe!au habari ilikuja GSM kwa GSM waingia mkataba blah blah!?
 
Mapunguani ni wale mbumbumbu wa Moo maana mnakomalia vitu msivyovielewa, kadadavueni mikataba yenu ya Mo extra, Mo viberiti, Mo biox, na Mo 26 kwanza ndio tunaweza kuwapima kama mnazo akili au zimo za kushikiwa
hawaangalii hili wako busy na ya Yanga
 
Nimesoma comment za wanasimba kwenye huu mjadala nimesikitika sana.

Lowassa hakukosea aliposemaga ELIMU! ELIMU! ELIMU!

Uelewa wa wanaSimba ni mdogo sana. Yaana kamakala kafupi kama haka ambako hakajazi hata ukurasa mmoja wa A4 wanashindwa kukaelewa.

Mikataba ni miwili. Lakini mtu anachanganya mkataba wa udhamini wa milioni 300 kwa mwaka, na mkataba wa jezi na vifaa vingine vya michezo kana kwamba ni mkataba mmoja.

Halafu mtu anadhani mkataba wa jezi ndo chanzo pekee cha mapato cha Yanga mpaka anaandika "Bilioni 10 kwa miaka mitano ni ndogo sana kwa Yanga."

Halafu kuna mtu sijui hata hesabu alipataga ngapi eti anadhani kwenye makala hii kuna taarifa ya kutosha kumsaidia kukokotoa kwamba ni "Tshs. 1,300/- kwa kila jezi"

Nikikutana na mwanaSimba mmoja mwenye akili ya kusoma na kuelewa nitampa hela akamchangie Vunjabei kwa kununua jezi.

ELIMU! ELIMU! ELIMU!
[emoji482]
 
Back
Top Bottom