Mkakati wao wa kushinda mechi ya leo ulianzia airport jana, sisi tunaojua fitna za nje tuliona, hakuna aliyeona hii, mganga wao aliwaambia mechi vs Kagera ni ngumu cha kufanya pale airport kila mtu atoke kwake kivyake mkutane pale, msipande basi la pamoja, mitego inaanzia airport, ndo maana kila mchezaji jana kaenda kivyake, aziz alienda na gari yake, Dube na kuna walioenda na bodaboda.
Msimu uliopita walidroo kaitaba na walijua walikosea wapi, msimu huu wamewaua, Kaitaba kugumu sana kwa Yanga na Simba, hasa Simba pale labda msimu huu, leo kagera wameupiga mwingi sana lkn wanacheza na timu ambayo nje wamejipanga haswaaa.
Rais wao anahakikisha mkoani hawaachi point, wanajua mkoani ndio kwenye ubingwa, Simba tuangalie hili.
Rais wao anaenda mkoani kila mechi kuwaunga mkono, labda awe na ziara nje ya nchi.
Hii timu hapa kwetu sijui, wanaangalia na wameshajiandaa kubeba ndoo ya Afrika na wanaweza.Hatari sana hawa jamaa.