Ile world cup naikumbuka. Lakini yatupasa tufahamu kwamba kila kitu kina taratibu na sheria zake na uzuri mleta uzi kaziweka kwenye baadhi ya post zake kwenye huu uzi ikowa kama sintofahamu unayooelezea ikitokea busara za sheria ni zipi ili haki ipatikane.
Hivyo, si vizuri kusema GSM anawahadaa Yanga bure. Licha ya kuwa mashabiki wa timu ila tuwe mashabiki wa mpira vilevile. Tukiwa mashabiki wa mpira huu usimba na uyanga tutauweka pembeni na kuutizama mpira kama mpira wenyewe upoje.
Mimi ni shabiki wa Simba ila niwe mkweli; shuti alilopiga Aziz Ki ni goli lile. Tena la wazi kabis. Uzuri kwenye kurasa tofauti tofauti za mpira Afrika limezungumziwa hilo! Kuwa lile ni goli la wazi.