Yanga yaingia mkataba wa Tsh Bilioni 34.8 na Azam Media

Hata kama simba watafatwa na Azam deal halita kamilika sababu yule mudi anataka mpaka akiwa na hisa zake 49 deal izo zikiingia ndani pindi na yeye tayar ni mwenyekit ngoma igawike
 
Za chini ya kapeti mmoja wa watoto wa bakhresa ni Yanga,so Yanga itakapoingia kwenye uwekezaji kati ya wawekezaji 3 mmojawapo anaweza kuwa ni mtoto wa bakhresa 😂
 
Lamine moro mpaka amerudi kwao ghana
Mbona wenzake wapo kambini wanacheza? Kwahiyo mshahara ajalipwa yeye tu wenzake wamelipwa?

Kwahiyo na chikwende pamoja na ajibu ambao hawapo kambini nao hawajalipwa mshahara?

Hebu fwatilia mambo kwanza
 
Imagine 34 kwa miaka 10 na itakuwa inaongezeka kila mwaka ila kuna watu wanatapeliwa huko 20B ndiyo thamani ya timu yao kwa mpaka dunia iishe
Hujui thamani ya club huwa ni ndogo kuliko inachoingiza?
 
Uwanja utajengwa tu
 
Azam wanasonga na watazidi kusonga mbele kwa moto mkali zaidi,kama Utopolo wamevuta huo mpunga basi mkataba wa Simba bingwa wa nchi na inayofatiliwa zaidi mpaka nje ya mipaka ya Tanzania watavuta mpunga mrefu zaidi.
Ndo ilivyo lazima Simba wabebe pakubwa, ni kama kwenye deal la Sportpesa, Yanga walivuna kuliko Simba sababu Simba hakuwa kwenye fomu
 
Ila huyu Jamaa Azam group kila kitu yeye hamna matajiri wengine jamani inamaana TANZANIA kuna tajiri mmoja tu mwenyewe idea za kutengeneza Pesa.

Sababu Azam media sifikiri hata inamiaka 10yrs lkn mambo inayo fanya na kujitanua kwenye media industry ni inakwenda speed ya ajabu.

MMUNGU aliye mpa kampa tu hawa jamaa wanaweza wakaja na idea ya kuuza hata MAVUMBI tu ya barabarani wakakamata soko vile vile.
 
Ndio hoja za Waswahili hizo Mkuu usishangae. Wao siku zote ni pangu pakavu tia mchuzi. MO ameisaidia sana Simba.
 
Azam wanasonga na watazidi kusonga mbele kwa moto mkali zaidi,kama Utopolo wamevuta huo mpunga basi mkataba wa Simba bingwa wa nchi na inayofatiliwa zaidi mpaka nje ya mipaka ya Tanzania watavuta mpunga mrefu zaidi.
Ahaa wapi. Labda Mo Dewji hasiwepo.
 
MO ni mwekezaji mzuri sana, tena sana hilo halina ubishi mkuu. Ila sisi ambao tumeangalia huu mpira na kuufuatilia kwa muda mrefu tunaona kuna tatizo la sustainability.
MO anaingia hasara kubwa, ila kwa mapenzi yake hilo siyo tatizo. Manji naye ilikuwa hivyohivyo, Hasanali Gulamali, Dewji wa Yanga, Mohamedi Virani etc nao wote wamepita na wametuachia wachezaji expensive tusioweza kuwalipa.

Mungu aepushe hili, ila naye MO akipita zake, akarithi mtu ambaye ni ukoo wake ila hayuko yari kujitolea kama MO, mtafanyaje?
Tatizo ni sustainability. Bilioni 20 kwa Simba siyo nyingi, simba itengenezewe mazingira ya kujiendesha yenyewe yaliyo mazuri.

Simba ingekuwa na miundombinu yake na mikataba yake mizuri na wachezaji wake wenye thamani kabla ya kutoa tenda ya uwekezaji. Ingekuwa timu moja kubwa sana.
Usiridhike na ubingwa uliotokana na Yanga kufungwa na Coastal. Siyo kwamba Simba kamfunika yanga 1 to 1.
 
Umeiweka kitaalamu sana
 
Wa Kwetu, MO hataki kutengeneza mazingira hayo! Anajua kabisa akishatengeneza mazingira ya Simba kujitegemea Basi yy kila kitu atalipia Tena kwa mikataba sio Kama ilivyo sasa.
 
Wa Kwetu, MO hataki kutengeneza mazingira hayo! Anajua kabisa akishatengeneza mazingira ya Simba kujitegemea Basi yy kila kitu atalipia Tena kwa mikataba sio Kama ilivyo sasa.
Umezungumza ukweli. Nadhani MO anapenda sana Power na asipokuwa nayo huwa mtu fulani wa kususa.
 
Kwa TUKIO la leo wapenzi na mashabiki wa Yanga tunatakiwa tujiskie FURAHA SANA zaidi ya Ushindi wa JUZI. Soon watatuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…