Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Uongozi wa Klabu ya Young Africans umetoa taarifa ya kulaani vikali vitendo vya kupigwa, kuchaniwa jezi na kufukuzwa uwanjani kwa baadhi ya mashabiki wake katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika Mei 25, 2025 katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kupitia taarifa hiyo, klabu hiyo imeomba mamlaka husika kuchukua hatua kali dhidi ya waliohusika na imetoa pole kwa mashabiki walioathirika.
Vilevile, Yanga imewasihi mashabiki wake kuendelea kudumisha ustaarabu, kutolipiza kisasi, na kuendeleza mazingira ya amani na mshikamano katika viwanja vya soka.