Yanga yashikilia msimamo wake wa kutocheza derby ya Kariakoo 15/6/2025

Yanga yashikilia msimamo wake wa kutocheza derby ya Kariakoo 15/6/2025

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,566
Reaction score
3,234
TAARIFA KWA UMΜΑ
JUNI 09, 2025​

Uongozi wa Young Africans Sports Club, unapenda kuutarifu umma kuwa, tarehe 7 Juni, 2025 tulipokea barua kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria kikao maalum cha kujadili masuala yahusuyo mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC, YANGA dhidi ya Simba.

Uongozi wa Klabu yetu ulitii wito huo na kushiriki kwenye kikao kilichofanyika leo, Jumatatu Juni 9, 2025 kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Tanzania zilizopo jengo la NSSF Mafao House, Dar Es Salaam, kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Baada ya majadiliano ya saa kadhaa, Viongozi wa Klabu waliwasilisha msimamo wa Klabu yetu kuwa hatutashiriki mchezo namba 184 uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025 mpaka pale matakwa yetu tuliyoyawasilisha kwa maandishi kwao yatakapotimizwa.

Tunawatakia kila la heri Bodi ya Ligi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini katika kushughulikia matakwa yetu yenye mustakabali mkubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.

Imetolewa na
Kamati ya Utendaji
Young Africans Sports Club

Soma Pia: Ali Kamwe: Bodi ya Ligi ikisikiliza na kutekeleza mahitaji yetu tutacheza Kariakoo Derby ya Juni 15, 2025

IMG-20250609-WA0045.jpg

Soma Almas Kasongo: Tumekutana na Yanga, Derby ya Kariakoo iko palepale na hakuna kilichobadilika
 
Duh, Kamati Tendaji yote ndo imeandika .! Hakuna CEO wala Kiongozi mwingine anayejicommit na kuweka saini yake.! ama kweli 'Ugali Moto Mboga Moto'.....

Mpaka hii wiki iishe mengi tutayashuhudia
 
Mimi mwenyewe nipo pamoja na nyie hakikisheni mnasimamia huo msimamo mpaka mwisho.

Sisi tunataka kuona hizo point zetu 3 za tarehe 15 tunazipata katika mazingira gani.

Je hayo magoli matatu atapewa yote Ahoua au atapewa nani?
 
Back
Top Bottom