KERO Yard ya GSM Mbagala imeongeza tatizo la foleni

KERO Yard ya GSM Mbagala imeongeza tatizo la foleni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Niwe mkweli tu sisi waislam hatufai kabisa kushika madaraka ya nchi. tawala zetu zote kimeo tu. Muislam mwenye akili Dkt Mwinyi tu kwa hadhi ya urais
 
Niwe mkweli tu sisi waislam hatufai kabisa kushika madaraka ya nchi. tawala zetu zote kimeo tu. Muislam mwenye akili Dkt Mwinyi tu kwa hadhi ya urais
Dk Mwinyi alipoambiwa na Baraka Shamte 2020 awapishe kwa sababu hata vikao vya CCM Zanzibar hakuwahi kuhudhuria kabla ya kupewa uraisi.

Kilichompata Baraka, mzee wa zaidi ya miaka 80 hatasahau. Alitekwa na kuteswa kisha akaachwa msituni ajifie. Ni bahati tu alijikokota akafika barabarani akasaidika.
 
Mzizi wa kuondoa foleni kwenye hizi bandari kavu (ICD/CFS) ni kuzitenga ziwe na zone(ukanda) maalum. Hizi zilizo tayari katikati ya mji zibaki kuwa Container Freight Stations(CFS) kwa ajili ya kurahisisha export container zifike haraka bandarini bila delay.

ICD za container zilizokuja kama import za local na transit zone yake iwe nje ya mjini. Hizi zote zinasubiri kwenda kwa mtumiaji wa mwisho yeye ndio anamua akaitoe muda gani. Changamoto iliyopo kwenye container za local wafanyabiashara wengi awataki ziende ICD za nje ya mji kupunguza gharama za usafirishaji kumfikia yeye.

Container empty hizi zinatakiwa ICD zake ziwe nje ya mji wakijua kuna kupakia Container empty meli imekuja wajiandae mapema kuzipeleka bandarini.

Hizi ICD/CFS mjini haziwezi kutoweka ni massive investment hao wamiliki kiasi walichoweka kuwatoa kirahisi ni jambo gumu. Kwa sheria za Tasac ili upate leseni hizo ilikuwa minimum uwe na mtaji wa 500m mpaka 1Billion. Hapo bado eneo inatakiwa square metre za kutosha kuweka ofisi za Mamlaka tofauti,eneo liwe na uzio,kamera za ulinzi,vifaa vya kupakia na kushusha Container (Reach Stacker hii mpya ni kuanzia 300m, used 180m), Bado truck za kubeba container.
 
Ni kweli tunataka maendeleo ila kiukweli naona kabisa Yard ile kua pale jeshini sio sehemu sahihi. Kwa mtazamo wangu ilibidi isogezwe huko nje ya miji kuliko pale.

Mfano usiku huu malori yamefunga njia moja(yamepaki barabrani) magari yanapita kwa shida kutoka Sabasaba hadi Zakhem.

Mamlaka husika liangalieni hili vinginevyo mnazalisha tatizo kubwa siku zijazo.
Bilioni 10 zile
 
Back
Top Bottom