Wana ccm na watu wengine mnaofaidika na uongozi uliopo mnapashwa kufanya haya;
1. Kwanza kumwambia rais ukweli, najua hili ni jambo ngumu sana na hatari kwenu,
2. Kutokutimiza amri na maagizo hasa yenye kukosa haki kwa raia, najua pia hili ni jambo ngumu sana kwenu,
3. Nyie wenyewe binafsi kutoshiriki vitendo vya kionevu, hili ni rahisi
4. Kushiriki katika harakati za kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa letu, hili linahitaji upeo mkubwa na kujitoa sadaka ila linawezekana
5. Tuendelee kukumbushana kuhusu Tanzania yetu iliyokuwa nzuri na umuhimu wa kuirudisha pepo ile ambayo kwa wengi imekuwa sasa historia tu
Watanzania tunapaswa kufikiri vizuri zaidi na kuacha ubinafsi na ugonjwa wa kumtukuza mtu. Tulitukuze taifa letu kwani kumtukuza mtu ni kumfanya awe na kiburi na kufikiri maovu yake ni upendo kwa watu wengine.