Hii ni mojawapo ya sababu why wanaume tunakufa mapema sana..
Yaani ukienda before andaa urithi kwanza ndio uende .
Kuna mengi uyajue
Kujua kuendesha leo haimaanishi wewe ni mzoefu barabarani utakufa mkuu.
Kwanza hapo unatakiwa week 2 hadi tatu tembea mtaani kwenu ambako hakuna magari mengi ili uijue pikipiki vizuri .
Naweza sema wewe leo ukupakia mzigo au mtu lazima utamuangusha tu maana wewe bado learner.
Anyway ukoanguka ndio umejua, wewe bado hujajua mpaka uanguke🤣
Zaidi pikipiki ni hatari unatembea na roho mkononi.
Wewe usiende mjini na pikipiki ni tricky sana hata sisi expert tunapita ila kwa umakini mkubwa sana na Machale
Huwezi kubalance mafuta halafu unataka kwenda town halo jichunge
Vipi kwenye foleni na ukashindwa kubalance mafuta ikakuzimikia? Vipi ukiwa round about bado ukashindwa pia ikakuzimikia?
Vipi ukachelewa kushika break ukagonga mtu?
Jifunze kwanza week kama 2 usipakie mtu anza kupakia mizigo mfano mfuko wa cement na endesha huko mitaani kwanza kwenu.
BabaMorgan