Yaya Toure akosoa uwepo wa Fainali 2 kwenye Michuano ya Afrika

Yaya Toure akosoa uwepo wa Fainali 2 kwenye Michuano ya Afrika

Mashabiki sio wanaocheza mpira. Kipinsi cha CORONA timu zilikuwa zinacheza bila mashabiki na maisha yaliendelea.
CAF wanataka pesa pia ili mashindano yaendelee kuwepo, huwezi kutaka mashindano yawe bure kisha baadae utake mabilion kutoka CAF, maumivu ya kushindwa fainali yasiwatoe akili kiasi hicho.

Unazungumzia wakati wa Corona, huoni jinsi uchumi uliyumba?
 
Ujumbe wa nyota wa zamani wa Barcelona na Man City, Yaya TOURE juu ya uwepo wa fainali mbili kwenye michuano ya Afrika.

Wakati umefika kwa mashabiki wa soka wa nchi zetu barani Afrika kudai HAKI YA MICHEZO kwa kuitaka CAF kuwa na mechi moja pekee ya fainali kwenye uwanja wa usiofungamana na upande wowote (neutral) au fainali mbili kwenye Uwanja wa neutral.

Ni aibu kwa bara letu kuona unyonge wa mchezo bora pendwa wa fainali ya soka duniani (ukitazamwa na mamilioni ya watu duniani) kushuhudia udhalilishaji wa timu ya ugenini kukumbana na mashambulizi ya kuvizia kwa fataki nyakati za usiku wakiwa wamepumzika katika uwanja wao wakiwa hotelini.

Kana kwamba haitoshi, wakati wa mchezo tulishuhudia (vijana waokota mipira (ball boys) wakirusha mipira mingi kwa wakati mmoja ili kupoteza muda kwa ajili ya timu za nyumbani, zaidi ya fataki mbili nzito zilipigwa kiasi cha kupelekea mechi kusimamishwa (mara tatu) ili kuruhusu moshi huo kutoweka, yote haya yalifanywa mbele ya rais wa CAF na ulimwengu mzima wa mashabiki wa soka wakitazama.

Hii sio mara ya kwanza barani Afrika Basi aibu kwenu CAF & FIFA kwa kujua haya yote yatatokea na bila kufanya lolote ila kukaa tu na kutazama onyesho la kupendeza la uharamu na kumtawaza mpiga picha na kombe la ubingwa akiota na kufikiria kuwa hii ingekoma?

Natumai FIFA ingefanya soka kuwa mchezo mzuri tena.

Chanzo: Kitenge TV
CAF wangechukua hatua kuipoka timu ya algeria ushindi na kuipa yanga kutukona na vitendo vya mashabiki wao. Hii ingepeleka somo la nidhamu kwa waarabu wote kaskazini ya afrika. Nchi hizo ndio tabia yao kuzinyanyasa timu za kusini ya jangwa la sahara wanapokutana nazo kwenye mchezo wa mpira.
 
Kwahiyo ile game mliipoteza kwasababu ya dakika? Ile game hamukuwa na uwezo wa kufunga tena, plan yenu ya kushambulia ilikuwa imebanwa tayari ndiomaana ilifikia hatua kocha akaamua kujaribu bahati kwa kufanya sub holela.

Bila ile penalty sidhani kama kungekuwa na lolote la maana.
Ishu sio uwezo wa timu kufunga, muda wa nyongeza ni muhimu bila kuyajali hayo uliyoyaorodhesha hapo.
Ila waarabu na bongo Vita haitokaa iishe uwanjani tumekua na ushindani sana utakaokuza zaidi vilabu vyetu.
 
Motsepe aliwai kuifafanua hii kwamba ikiwa final mechi moja itapigwa uwanja wa neutral mashabiki wengi awana msuli wa pesa,Africa njaa waya mkali mashabiki watashindwa gharama za kukwea pipa,gharama za hoteli n,k

mfano final iwe Yanga Vs Usm Alger alafu mbungi ikapigwe Lagos mashabiki wangapi wataenda Lagos Nigeria kucheki game!
Ni kweli kwa nchi zetu hizi sjui serikali itatoa ndege ngapi
 
unasema kama umeshindwa kufunga dakika 90 tatu ndio utaweza? Ka angalie mechi ya KRC Genk Vs Royal Antwerp uone dakika 1 tu imenyima watu ubingwa, Real Madrid Vs Atletico Madrid final UCL, Manchester United Vs Bayern Munich UCL, kwenye mpira dakika moja ni kubwa sana na ina badili kila kitu
Tatizo la wengi wanatanguliza ushabiki, usimba na uyanga unatugharimu tushindwe kulitanguliza soka mbele.

Wanayanga tukichangia Kama hivyo inaonekana tunafanya hivyo kwa sababu tumeukosa ubingwa. Hii isiwe sababu ya kutufunga midomo kufichua madhaifu ya uwanjani.
 
Lakini mpira ilisimama vipindi vyote viwili. Ulivyosimama kipindi cha kwanza, muda uliopotea ulifidiwa kabla ya mapumziko. Dakika 5 sijui 6 zilizoongezwa kipindi cha pili ni fair kwa muda uliopotea kipindi cha pili kwa sababu nadhani haukusimama kwa zaidi ya dakika 2. Kama unashindwa kufunga kwa dakika 90 toka goli la kwanza, kulilia dakika 3 za nyongeza ni kutafuta kisingizio tu.

Kawaida mashindano haya, tegemea timu ya nyumbani kupata favour fulani. Hata Yanga game ya kwanza alipewa dakika 10 za nyongeza. Je alistahili? Na hili nililisema mapema msitegemee nyongeza za namna hiyo kule nikaonekana sina akili.
Hayo unayozungumza ndio maana watu hawayataki.
 
Mechi iwe bure uwanja utajaa popote pale hata Kwa Mkapa ukileta al-ahly Vs Wydad uwanja unajaa...
Mechi nyingi za bure tumeshushudia watu wakiwa wachache

Angalia Marumo walikuwa wanafanya bure lakini uwanja ulikuwa mtupu.

Hao ni mashabiki wenye interest na timu yao lakini hali ilikuwa vile.

Halafu pia mashabiki wataoingia bure hawtakuwa mashabiki tena, watakuwa watazamaji kwasababu timu zinazocheza hawana interest nazo.

Ni saaa na msanii ukafanye show kwenye hafla ya viongozi wa juu, hutapata ile sapoti ya kishabiki ambayo ukiwa Club unaipata.

Huwezi ukazima mic ukawaachia maofsa waitikie verse inayofuata, zaidi utaona wao wako bize na mambo yao.
 
Back
Top Bottom