Yesu akirudi leo atasali wapi? Kwa Wayahudi, RC /Wasabato au Kwa Walokole? Au Mashahidi wa Yehova? Naomba majibu

Yesu akirudi leo atasali wapi? Kwa Wayahudi, RC /Wasabato au Kwa Walokole? Au Mashahidi wa Yehova? Naomba majibu

Uislamu ulikuwepo kabla ya ukristo, kwa sababu uislamu ulianza kwa adamu, Idrisa, nuh, Ibrahim,(Abraham) Issa (Yesu) , Muhammad hadi kutufikia sisi na wajao,.

Je ukristo ulianzia wapi kwa ushahidi wa maandiko ya biblia uiaminiyo???

Dini yenu ni ngeni zaidi, na imebebwa na shetani na ndiyo maana ninyi ni wengi sana kuliko waislamu na mtaingia motoni, kwa sababu hata hiyo biblia inasadiki kuwa wapotevu ni wengi sana kuliko waaminio kweli.

Fanya tathmini ya kweli kabla hujaamgamia,,,,,!!!!
Kwanza Tengua kauli yako huyo Issa mnaemzungumzia kwenye kitabu chenu sio Yesu.. na hizo stories mnazolishana uislamu ulianza kwa Adam mnaonekana kichwani mpo weupe muwe mnasoma historia

Uislamu umeanzishwa miaka 500 baada ya Yesu kuondoka .. tena kauanzisha Mohamad wenu ambaye mnamuita Mtume huyo ambaye baadae aliuliwa kwa kunywesha sumu labda nikumbushe tu

Baada ya Miaka 300 ya kuanzishawa kanisa la Roma huko mjini Makkah kuna mtaalam mmoja aliekuwa akiitwa MOHAMMAD ambae alikuwa akiabudu sanamu Kwa muda wa miaka 40 babayake na mama yake walikuwa ni wapagani kama ambavyo mfalme CONSTANTINE alikuwa
Naye siku moja akiwa amekaa pangoni akatokewa na mtu ambaye alimtaka asome maandishi fulan lakin Mohammad akamjibu kuwa siwezi kusoma yule mtu Alie mtokea akaendelea kumlazimisha asome Huku akimminya pale Mohammad anaposema siwez kusoma Mohammad alidhani mtu huyo ni shetani
MOHAMMAD aliporudi kwake akamsimulia mkewake kilicho mkuta mkewake HADIJA akamwambia uyo sio shetani ni malaika mke wa Mohammad akampeleka Mohammad Kwa mpwa wake aitwae Uzza. Uzza alipigilia msumali alio uweka hadija kuwa uyo ni malaika naww unatakiwa uwe mtu mkubwa apo ndipo ukawa mwanzo wa dini ya uislamu
Mohammad alichukua taratibu,Sheria na tamaduni nyingi sana kutoka Kwa wayahudi na kuzifanya ni tamaduni za dini yake hii ndio sababu ya ukristo na uislamu unafanana kiasi sana

na Mohammad alikuwa akitaka wayahudi waungane nae katika dini yake lakini wayahudi walikataa na hapo ndipo alipo kuwa akianzisha vita nao kutokana na vita kutoka Kwa Mohammad na Roma wayahudi walizidi kuyakimbia maeneo yao na kwenda maeneo mengine
Mohammad alifariki Kwa kupewa sumu na mmoja wa wayahudi ambao Mohammad aliua familia yake na nduguzake

Sitangia tena kwenye uzi huu inaonekana namjibu mtu ambaye si mfatiliaji wa mambo hadi anasema uislamu ulianza wakati wa Adam mara Issa ni Yesu

Hizo stori kawafundisheni huko madrasa
 
Ni sawa na kuuliza, hivi baba yako akiwa na watoto 20 na wote wana Imani tofauti ( wewe Kama baba) utamkubari yupi?
 
Naamini 100% Hatoenda Kanisani kama mimi

Yesu sio mnafki wakugombanisha watu.

Hatoenda Church am sure of it.
 
Nawasalimu wote.

Kumekuwepo na mjadala kuhusu ipi dini ya Kweli, huu ni mjadala wa siku nyingine. Leo nataka tumuongelee YESU KRISTU.

Wakati akiwa hapa duniani, Yesu alionekana hekaluni akihubiri injili, Wayahudi hawakupendezwa sana wakisema anakufuru na kupelekea kumsulubisha msalabani.

Baada ya kifo na ufufuo wake (Kama ilivyoandikwa) ndipo lilianza vuguvugu la kanisa la kwanza!

Ukiwauliza RC watakwambia, Papa wa Kwanza ni Mt Petro na alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Ukiwauliza Walokole nao watakwambia wao ndio wapo sahihi, Vivyo Hivyo kwa Wasabato au Mashahidi wa Yehova!

Kama biblia inayotumika ni moja inakuwaje kuna mgongano huu mkubwa?

Je, ni kitu gani hawatuambii?
Wakati anaondoka duniani, je alisema akirudi atarudi na kuingia kwenye nyumba ya ibada?
 
Wayahudi mbona hawamwamini Yesu? Aende kwao kufanya nini?
 
Nawasalimu wote.

Kumekuwepo na mjadala kuhusu ipi dini ya Kweli, huu ni mjadala wa siku nyingine. Leo nataka tumuongelee YESU KRISTU.

Wakati akiwa hapa duniani, Yesu alionekana hekaluni akihubiri injili, Wayahudi hawakupendezwa sana wakisema anakufuru na kupelekea kumsulubisha msalabani.

Baada ya kifo na ufufuo wake (Kama ilivyoandikwa) ndipo lilianza vuguvugu la kanisa la kwanza!

Ukiwauliza RC watakwambia, Papa wa Kwanza ni Mt Petro na alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Ukiwauliza Walokole nao watakwambia wao ndio wapo sahihi, Vivyo Hivyo kwa Wasabato au Mashahidi wa Yehova!

Kama biblia inayotumika ni moja inakuwaje kuna mgongano huu mkubwa?

Je, ni kitu gani hawatuambii?
we mbaguzi mbona hujawagusia waislam au ndo watakuwa wanakula faya muda huo?
 
Nimemuongelea Yesu Kristo, Mohammed SAW akirudi ataenda Mecca halina mjadala kabisa
 
Atakuja kuwachukua walio wake je watu Hawa wanapatikanaje? Wanasali wapi
walio wake anawajua kabla ya kuumbwa ulimwengu njia ni nyembamba iendayo uzimani na njia ni pana iendayo upotevuni pia ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu wenye nguvu ndo wanaouteka
 
Kanisa la Yesu sio majengo, ni watu. Mwili wake haujajengwa na "organization" Bali umejengwa na watu wanaomfuata.
na wanaomfata Yesu katika roho na kweli kwa kipindi hiki ni wachache sana maana Mungu anatautazama Moyo aangalii kama mwanadamu aangaliavyo
 
Nawasalimu wote.

Kumekuwepo na mjadala kuhusu ipi dini ya Kweli, huu ni mjadala wa siku nyingine. Leo nataka tumuongelee YESU KRISTU.

Wakati akiwa hapa duniani, Yesu alionekana hekaluni akihubiri injili, Wayahudi hawakupendezwa sana wakisema anakufuru na kupelekea kumsulubisha msalabani.

Baada ya kifo na ufufuo wake (Kama ilivyoandikwa) ndipo lilianza vuguvugu la kanisa la kwanza!

Ukiwauliza RC watakwambia, Papa wa Kwanza ni Mt Petro na alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Ukiwauliza Walokole nao watakwambia wao ndio wapo sahihi, Vivyo Hivyo kwa Wasabato au Mashahidi wa Yehova!

Kama biblia inayotumika ni moja inakuwaje kuna mgongano huu mkubwa?

Je, ni kitu gani hawatuambii?
Kanisa la kweli liko ndani ya moyo wako. Ukimwamini Yesu yeye anaingia humo na utamwona tu.
 
walio wake anawajua kabla ya kuumbwa ulimwengu njia ni nyembamba iendayo uzimani na njia ni pana iendayo upotevuni pia ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu wenye nguvu ndo wanaouteka
Naona unazunguka Sana, jinsi gani tunaweza kuwajua Hawa watu?
 
Haya mambo ya Dini mnayachukulia poa poa sanaa.

Wapi ulisikia Yesu akirudi anakuja kusali?

Kama huna cha kuandika kaa kimya pia inasaidia kupumguza kuonekana hamnazo
 
Hebu tupe ushahidi wa unachokisema

Yesu Mwenyewe alijua mipaka ya utume wake. Kwahiyo alisema:

1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).

2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli. “Akasema si vyema kukitwaa chakula cha
watoto na kuwatupia ’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).

3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 10:5-6).

4. Baadhi ya Wakristo mnadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe. Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu. Yeye amesema kwamba: “Lakini watakapo wafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).

5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba: “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).

6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49.)

Paulo ndiye aliyempinga Yesu kama biblia inavyosema

Biblia inasema kwamba: “Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na bila neno, aliwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo walipopingana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni safi; tangu sasa ninakwenda kwa watu wa mataifa. (Matendo 18:5-6).
 
Hebu tupe ushahidi wa unachokisema

Baadhi ya Wakristo mnayo shauku ya kugonganisha aya za Biblia. mnasema kwamba Bwana Yesu aliagiza kwamba “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19).

1. Najibu kwamba aya hii inapinga maagizo yote ya Bwana Yesu yaliyotajwa juu. Kwahiyo haiwezi kuwa agizo la Yesu wala aya ya Injili.

2. Ya pili aya hii imeandikwa mwishoni mwa Injili ya Mathayo, na nitathibitisha baadaye kidogo kwamba aya za mwanzo na za mwisho za kila kitabu ni za kuongezwa baadaye. Aya zile siyo aya sahihi za Biblia.

3. Ya tatu katika aya 28:19 ya Mathayo neno mataifa limetumika kwa maana ya mataifa ya Israeli. Kama Biblia inavyosema kwamba: “Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. (Luka 2:1). Kaisari Augusto alikuwa mtawala wa Roma tu. Hakuwa na mamlaka yoyote nje ya nchi yake juu ya ulimwengu.

Katika aya hii amri iliyotolewa kwa ajili ya ulimwengu na ya nchi ya Roma tu iliyokuwa chini ya utawala wa Kaisari wala siyo ulimwengu wote. Hivyo ndivyo inavyoeleweka kauli ya Bwana Yesu aliposema:

“Enendeni mkawafanye mataifa yote (ya Waisraeli) kuwa wanafunzi. (Mathayo 28:19).
 
Utume wa Yesu akiwa duniani ilikua ni wa wana wa Israel lakini alivyofufuka utume wake ulibadilika kuwa wa mataifa yote.
 
Utume wa Yesu akiwa duniani ilikua ni wa wana wa Israel lakini alivyofufuka utume wake ulibadilika kuwa wa mataifa yote.

Katika ufalme wa mbinguni Yesu ana yakini kuwa hatokuwa nao ila wana wa Israili tu. Injili ya Mathayo inasema:

Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

Mathayo 19.28

Hata katika maombi yake inaonyesha kuwa Yesu alikuwa anajua mipaka yake na uwezo wake.

Madai ya kuwa yeye ni mwombezi, mbali kuwa ni mwokozi, wa ulimwengu mzima ni kumsingizia jambo ambalo mwenyewe hakulidhania.
 
Back
Top Bottom