You cant be a rich, without shady or dirty deals

Utajiri ni suala la Mungu, yaani akili; ni maarifa. Anayepata maarifa anakuwa tajiri; anayevumbua huyo ni tajiri.

Yesu ambaye ndiye sheria yenyewe amesema juu ya utajiri. Yeye alionya juu ya matajiri na sio utajiri. Maana yake ni kwamba utajiri sio huo mtoa mada anataka tukubaliane nae.
 
Sio kweli, huo ni mtizamo tu... Inawezs kuwa kweli kwa asilimia fulani ila haimaanishi utajiri unakuja kwa kufanya deals chafu tu
Deal chafu sio lazima kuuwa au wizi ,Bali kutumia vitu kama Sheria Kwa advantage Yako au kukwepa Kodi .
Imagine unalipa Kodi na mwenzio ana itumia hiyo Kodi Yako kuendesha V8 na kutunga Sheria aongezewe mshahara.
Fanya cilivil disobedient na utakuwa tajiri bila kumuumiza mtu.
 
Ukiona unafanya kazi husongwisongwi na polisi, TAKUKURU na vyombo vingine vya usalama jua hiyo kazi ni ya kimasKini kabisa. Nafanya kazi ambayo kwa siku naingiza zaidi ya 3m NJE YA MSHAHARA NA POSHO ila vyombo vya usalama washakuwa sehemu ya maisha yangu. nishawahi kuelezea humu japokuwa watu hawakuweza kunielewa
 
Ni Rahisi sana ngamia kupita katika Tundu la sindano kuliko tajiri....
 
Kwa hiyo group lako linatuwakilisha sote? Tutake radhi.
 
Wrong. Huu muono mzima ni one dimensional. Utajiri haupatikani kwa sababu ya kufanya dirty deals only bali mostly ni kwa kuangalia fursa na kuzitumia lakini first ni lazima uwe na akili na uwezo wa kuziona na kuzitumia. Mfano mzuri ni Maxence Melo na JF, Jeff Bezos na Amazon, Elon Musk -Zip2 na X.com, space X, Tesla, ambayo ni paypal, Mark Zuckerberg na Facebook, What'sApp, na Instagram.

You see, hizo zote ni fursa, kuna uuzaji wa bidhaa, kuna utumaji wa pesa, usafiri, na kuna communication. So, hizi za "hauwezi kuwa tajiri mpaka ufanye dirty deals" ni muono wa kimaskini uliokosa akili.
 
Acha uvivu wa kufikiri..utajiri ni mipango walichotuzidi hao kina bakhresa ni kusimamia misingi waliyojiwekea pamoja na kuwa na ndoto kubwa. Kuna mtu ndoto yake ni nyumba na gari na kuna mtu ndoto yake ni kuwa tajiri, kiufupi utajiri ni akili nyingi na sio kufanya uovu. Hata hizo dirty deals huwezi kufanya kwa mafanikio kama dishi lako limeyumba.
 
Maisha yana mambo mengi sana ninakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa sana. Hakuna binadamu anaweza akaweka siri zake zote hadharani. Safari ya kutafuta utajiri inahitaji roho ya ukakamavu sana. Ni safari inayohitaji Nguvu ya ziada katika kupambania ugali wako. Kuna maamuzi magumu mtu aliyesoma sana hawezi kufanya. Kitu kigumu na muhimu sana ni kufungua macho.
 
Hao wakina bakhresa wenyewe wasingefika hapo kama sio kuhujumu National Milling


Kafuatilie kisa cha mkemia mkuu kufa

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 

Mkuu naomba link ya huo uzi ulioelezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…