Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread


JONESIA MWAMUZI SIMBA VS YANGA APRILI 16

Mwamuzi Jonesia Rukyaa kutoka mkoani Kagera ndiye atakayesimama kati kuamua mechi ya watani wa jadi Simba vs Yanga itakayopigwa kesho kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Bodi ya Ligi, Jonesia atasaidiwa na Mohamed Mkono pamoja na Janeth Balama watakaokuwa pembeni, huku tatu Malogo akiwa ni mwamuzi wa akiba (4th Official).
 
Kila la kheri Timu ya Wananchi. Tunachohitaji ni Points 3 ili kujiwekea asilimia nyingi zaidi za kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.

#DaimaMbeleNyumaMwiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…