YANGA SC WANANCHI WAKO JUU SIO KITOTO
Sio siku nyingi taarifa ilitoka kuhusiana na klabu ya Yanga Sc ndio timu Bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na ni timu bora namba 3 Afrika watu kama wakawa na mashaka.
Unakuwaje na mashaka na klabu pekee Tanzania yenye medali ya CAF kutokana na kuwa finalist kwenye mashindano ya CAF INTERCLUBS?
Unakuwaje na mashaka na klabu ambayo ndio back to back domestic treble Winners ambayo msimu mmoja domestic treble ilisindikizwa na Unbeaten record?
THIS IS FACTS AND HERE WE SPIT FACTS ONLY LADIES AND GENTLEMEN
Yanga Sc wakiwa wanaendeleza ubabe wao msimu huu kwa 5G's na soka safi idara ya Habari na Mawasiliano pamoja na Maudhui nayo dunia ikaendelea kuwatambua kwa ubora wa contents zao na hamasa kwa vitendo na uthubutu ikiwemo zile Maxi na Aziz Ki Days pamoja na safari ya Rwanda Kigali katika mechi ya Kimataifa.
Kama haitoshi Klabu ya Yanga Sc ndio klabu pekee Afrika Mashariki kwa sasa iliyomo katika kinyang'anyiro cha tuzo zinazotambulika na Shirikisho la soka Afrika kama CAF AWARDS 2023 katika category ya klabu bora ya mwaka barani Afrika.
Yanga Sc hii hii ina mlinda mlango wake Djigui Diarra katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya kipa bora Afrika akichuana na makipa wenzako hodari kama Andre Onana, Yasine Bounou, El Shennawi na wengineo.
Nikuongezee hii ndugu Mgeni Rasmi..
Akiyafanya makubwa haya akiwa katika klabu ya Fiston Kalala Mayele yuko katika tuzo za kuwania mchezaji bora wa Afrika. Ndio, Mayele anachuana na akina Mane, Mahrez, Yves Bissouma na wengineo kwa tuzo hii.
Kama haitoshi Mayele na Djigui Diarra wako katika kinyang'anyiro cha kuwania mchezaji bora Afrika kwa ligi ya ndani wakichuana na miamba mingine kama Peter Shalulile, Percy Tau, Yahya Jabrane, Makabi Lilepo na wengineo.
We all know wachezaji wengi wa National team wanatoka klabu gani bongo right? Au Basi .
Je hii haitoshi kukiri nilichokisema kwa mara kadhaa huko kuhusu ubora wa klabu hii kongwe na kubwa zaidi Tanzania?
Yanga Sc kwa sasa ndio klabu bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati ndani.ya kiwanja na kidigitali na facts are wide open. HUU NI UKWELI MCHUNGU